Dunia ina mambo mengi ya kushangaza

Kwahiyo hizi kafara, misukule, mali za kitajiri, kusababisha uchizi kwa watu na malimbwata ni vitu vya uongo? Mbona vina matokeo na tunaona watu wakivipitia..
we si umeona mtoa mada vitabu tu alivyosoma kashavicha na anasema ni vya hatari, ila anataka tusikilize story yake na kuikubali 🤣

story za uchawi ni kama za chuma ulete ambavyo hazifanyi kazi benki mkuu
 
naunga mkono
 
Ni kweli kabisa unachokisema...kama wewe hujawahi kuwaona albino haimaanishi kwamba albino hawapo, hata kama utaamini wapo kwa shingo upande basi utaona ni jambo lenye utata sana kwasababu kwa hali ya kawaida binadamu hawezi kuwa albino
Hapa kuna kitu umesema ukweli mimi nilikua sijawahi kumuona mtu ana vidole 6 vya mikono yote kuna siku nikiwa kwenye gari nilikaa na Mzee mmoja nilipoangalia mikono nikaona ana vidole 6 mikono yote sio vidole 5 kuna sehemu nilikua napenda sana kwenda kuweka hela kwa wakala siku hio naenda nikakuta wakala mwingine sio yule wa siku zote wakati anabonyeza simu kuhesabu vidole alikua na vidole 6 sio 5
 
we si umeona mtoa mada vitabu tu alivyosoma kashavicha na anasema ni vya hatari, ila anataka tusikilize story yake na kuikubali 🤣

story za uchawi ni kama za chuma ulete ambavyo hazifanyi kazi benki mkuu
Bank penyewe kuna mazindiko ya hatari wanasema🤣

Wewe lax hujapigwa na kitu kizito naona! Haya mambo yasikie tu!
 
Hao wapo hakuna cha ajabu hapo
 
Naomba kufahamu je Uwepo wa mungu upo kweli?
Na Mungu yupi ni wa kweli hapo Allah, wa walokole au wa wakatoliki?.
MUngu kweli yupo na tatizo linakuja tunaamini kwamba sisi tumetokea tu na hakuna kitu kilichofanyika na nguvu fulani ya nje iliyotufanya tuwepo. Ila tambua ulimwenguni hakuna kitu kilichojizukia tu chenyewe ni lazma ipo nguvu fulani imetupa kitu tunachokiita kanuni za asili

Mpaka leo suala la dark matter limekuea gumzo kidogo ila linaleta picha fulani ya ulimwengu ambao upo zaid yetu(kwa wale wasioamini muumba)

Kuhusu muumba yupi nadhani jibu ni rahisi tu sio biblia wala quran vyote vinaonesha hukumu ya mtu itafanyika kwa haki ya matendo yake mwenyewe.....wapo wakristo wasio waislam wataonja pepo kwa matendo yao na wapo waislam wataonja pepo kwa matendo yao wenyewe
 
Kuna binadamu wanazaliwa na vidole vya ziada, ni disorder tu.
 
we si umeona mtoa mada vitabu tu alivyosoma kashavicha na anasema ni vya hatari, ila anataka tusikilize story yake na kuikubali 🤣

story za uchawi ni kama za chuma ulete ambavyo hazifanyi kazi benki mkuu
Sawa kwa mtazamo wako umewaza hivyo ila mimi sifundishi njia za giza nimeweza uzi kufungua macho kwa wale ambao wanautata kuhusu uwepo wa mungu, na hapo juu nimeshaeleza kuna baadhi ya vitabu vipo direct sana na kwa mazingira na maisha yetu ni rahisi sana mtu atamani kujaribu

Shuhuda za watu ambao wamepata side effect ya kujua hayo mambo zipo nyingi sana na zingine huwa hazisemwi tunaziona tu kupitia mabadiliko hasi ya mtu
 
Bank penyewe kuna mazindiko ya hatari wanasema🤣

Wewe lax hujapigwa na kitu kizito naona! Haya mambo yasikie tu!
naam sasa wewe jibu hilo unaona linaleta mantiki? maana ndo jibu lao kwamba bank sasa ndo kuna uchawi mkubwa kuliko wote, au kuingia bungeni lazima uwe umejipanga haswa maana sio poa hata kidogo --- kumbe ni mambo ya kwenda sawa na wenye system tu.
au story za kuibiwa mazao shambani kwa njia za kichawi ila njia hizohizo hazifanyi kazi kwenye maghala ya mazao
hii ni michezo mkuu

mkuu shinda tunapitia nyingi sana, na tiba moja wapo ni kuzikataa story za namna hii.

we unaamini hizo mambo?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…