Dunia ina mambo hii

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,351
Hawa alipata alipata danga, w alikutana kwenye kijiwe cha chips kwakua alitoka kazini na kukumbuka nyumbani gas imekwisha aliona ni kheri ale chakula cha jioni na ya gas ata ya solve kesho yake.

Bwana yule alipomuona Hawa alianza kumuangalia kwa macho yenye uchu na kumlipia oder yake akisisitiza ongezeko na vipande vya kuku. Hawa akitaka chips egg confused, mishkaki miwili pamoja na soda.

Danga lilikaa meza moja na Hawa na waliongea na kukutana, alimfahamisha kuwa yuko pale kwa safari ya kibiashara akitokea mikoani. Danga liliomba kuonyeshwa mji, waliondoka pale na kwenda kupata bia baridi ufukweni mwa bahari.

Mwisho safari iliishia hoteli aliyofikia Danga, hoteli ya nyota nne kando ya bahari. Hawa alihitaji kuoga apunguze jasho la mchana kutwa. Alivua nguo zake na kuziweka vizuri kwani hakuwa na nyingine za kubadili.

Alipotoka bafuni danga liliamia kuoga pia, wakati danga likiwa bafuni, Hawa aligundua briefcase ya danga haijafungwa. Alishawishika kuifungia ndipo alipopata hamtaki. Alikuta pichu za wanawake ikiwemo ya kwake zimejaa kwenye briefcase. Hawa alibeba pochi viatu na nguo zake alitoka mbio akiwa na taulo kifuani.

Inawezekana danga anatumia pichu za kina dada kishirikina ili kupata pesa. Dunia ina mengi lakini Hawa alifanikiwa kubeba pichu yake.
 
Story zako huwa za kweli au unatunga tu usiku ndoto za ki director director.
 
Wanawake wasipo acha tamaa ya pesa hayo yote yataendelea kutokea.
 
Akili za baadhi ya wanawake huwa zikoje sijui, hapo jamaa angejilia kwa vipande vya kuku tu πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Pichu tu hawa kakimbia angekutana na vumbi si angesanda kabisa,

ila ata hivyo mie huyo hawa nilimmendea sana wakati namuhudumia viepe yai na tukuku tukuku, sema tu jamaa aliniwahi
 
Ila Hawa ni mwizi,kwanini apekue pekue vitu kwenye mikoba ya watu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…