Dunia imebadilika, acheni kupost post mapicha yenu huko mitandaoni

Na huo muda unautoa wapi?
nina Muda mwingi sana wa kushinda na Computer mbele yangu

kuliko muda hata wa kutembea kwenda toilet au muda ninao jipa break kwenda Kula

na kunyoosha viungo kidogo,nikisha jinyoosha tu Narudi kwenye screen.
 
Sawa Privacy and Security ni kwa nyie watu wenye maisha yetu bana, mboga saba usafiri VI 8 - hamtaki watu wawajue zaidi ili wasije kuwadhuru maisha yenu ama biashara zenu kubwa kubwa..

Sasa mimi kapuku wali maharage dona dagaa kwa mbali maji ya kandoro hiyo picha yangu mtu aitafute ya nini kwa mfano? Au ampeleleze mwanangu wa nini anayesoma kayumba.... kial kukicha ni TZ 11 kwenda na kurudi home nauli ya daladala ni ntiani...
 
Castr,
your very right definetly right

mimi sikuombi namba ya simu (maisha)

labda uamue kunipa yako, na ukinipa yako,sikutafuti kwa namba yangu

mpaka naku save kwenye simu yangu ujue umetimiza vigezo na masharti

Thank God siku hizi nina simu ya OFISI ndio kabisaaaa mpk upate namba yangu (private)

labda uwe mwenye nyumba wangu au mlinzi wa ofisi zangu.

"namba ya simu sitoi asee hata uwe nani sikupi" kama ni mdada nakutaka

nipo radhi nikae ofisini hadi saa tano usiku nihakikishe umelala ndipo nirudi home,ila sio nikupe namba yangu.
 
Nilishtuka siku naambiwa kuna mtu Instagram amefungua akaunt lakini picha zooote almost 50 ni zangu, kwa kua sipo IG ikanibidi ni install na kwenda kujionea mwenyewe, kuja kupeleleza na bestie wa karibu... nilimind sana akaifuta akaunt.

Sioni tabu kujipost popote au kupiga picha na yeyote, sijui kwann hua napata furaha.
that's your life bro.

fanya kile hukufanya uwe na amani na furaha.
 
Kwa sasa hivi mtu ukiwa na FB account halafu friends list yako inaonekana na watu, halafu una urafiki na watu usiowajua vizuri, hapo unasubiri kuwa cloned tu.

Kwa usalama zaidi.

1. Lock friends list asione mtu zaidi yako.
2. Lock mtu asipost kwenye profile yako bila approval.
3. Lock groups zako zisionekane na mtu zaidi yako.
4. Kumbuka hizi security settings ni kwenye profile yako tu, ukipost kwenye group au profile ya mtu zinaweza zisi apply.
5. Kumbuka mtu hahitaji password yako, anaweza ku copy picha tu na kutengeneza profile nyingine kwa jina lako na kujifanya ni wewe, na kuomba urafiki kwa rafiki na ndugu zako kwa nia mbaya.
social network zote natumia ila siweki picha zangu "never"

siamin katika mapicha picha binafsi,naonaga kama ni tambo flani hivi (watu wanaringishiana)

maisha yao, wako wapi, wako na nani, wanakula nini ''that's all"
 
Si lazima picha ziwe tambo.

Kuna watu wako mbali na familia zao na marafiki wanaona ni aina nzuri ya kujumuika.

Kuna wengine wanaadhimisha maisha ya ndugu, jamaa na marafiki waliofariki.

Kuna wengine wanaongeza awareness kwenye mambo ya afya, siasa, ujasiliamali.

Kuna wengine wanabadilishana mawazo katika mambo wanayopendelea pamoja kama michezo, muziki, habari nk.
 
Sawa Privacy and Security ni kwa nyie watu wenye maisha yetu bana, mboga saba usafiri VI 8 - hamtaki watu wawajue zaidi ili wasije kuwadhuru maisha yenu ama biashara zenu kubwa kubwa..

Sasa mimi kapuku wali maharage dona dagaa kwa mbali maji ya kandoro hiyo picha yangu mtu aitafute ya nini kwa mfano? Au ampeleleze mwanangu wa nini anayesoma kayumba.... kial kukicha ni TZ 11 kwenda na kurudi home nauli ya daladala ni ntiani...
umeshawahi jiuliza kwanini wenye albinism hawaji post ovyo??

lazima unajua kwanini, sasa kwakua unajua hvi unajua mimi nikienda kwa mganga leo

akaniambia nitafute mtu mwenye kitu flani,then pita pita kwenye mtandao naona kile kitu kipo kwako au kwa mwanao

unafikiri kitakachofuata ni nini? unafikiri watu wote wanaopotea hutekwa kisa PESA?? fikiria upya mkuu
 
Si lazima picha ziwe tambo.

Kuna watu wako mbali na familia zao na marafiki wanaona ni aina nzuri ya kujumuika.

Kuna wengine wanaadhimisha maisha ya ndugu, jamaa na marafiki waliofariki.

Kuna wengine wanaongeza awareness kwenye mambo ya afya, siasa, ujasiliamali.

Kuna wengine wanabadilishana mawazo katika mambo wanayopendelea pamoja kama michezo, muziki, habari nk.
ni kweli,sijapinga.
 
Hongera zako kwa kujitambua mapema

wengine ndo tumejitambua siku ya tatu saivi
Tangu social media zianze sijawahi weka picha na kuna mazingira nilikuwa tayari nilikuwa nimepata elimu juu ya hasara ya kufanya ivyo kabla hazijashika kazi na ujio wake,nashukuru umeeleza mengi vizuri sana
 
Nilikuaga sielewi kwanini kuna sehemu ukipita huruhusiwi kupiga picha, nilikuwa hata sijui kwanini. Nilikuwa sifahamu kwanini familia flani flani hasa za kifalme sio watu wapenda mapicha picha, kujionyesha onyesha.Nilikuwa sitambui kwanini yote hayo ni "marufuku" kwa aina flani ya watu nilidhani tu sababu ya vyeo na nyadhifa zao.

Lakini sasa nimeelewa kwanini yote hayo yalikuwa yanafanyika, na ninakubaliana nao kuwa walikuwa na wapo sawa hata na sasa. Wote ni mashahidi jukwaaa la MMU watu wakitafuta wapenzi, kwenye social networks tofauti watu wakitafuta wapenzi. Picha nyingi zimekuwa zikitumika huko, na nyingi kati ya picha zinazotomika si za wahusika wenye picha wenyewe na wala wao hata hawajui.

Kama kuna jitu lipo huku linatumia picha yake kudanganya watu, matukio ya namna hiyo ni mengi sana. Umeshawahi kukaa chini ukajiuliza hizo picha wanazitoa wapi? Jibu najua unalo ni humu humu mitandaoni kwenye hizi social media. Ndugu zanguni yawezekana hujawahi ona picha yako ikiandikiwa tangazo ndio mana unaona kama hii haikuhusu ila nataka tu kukwambia "ipo siku".

Ipo nini nimesema? (in teacher mpamire's voice)

Nataka kukwambia nini wewe dada wewe kaka hebu leo kata mazoea ya kujipost post huko kwenye mitandao, kama unapenda picha fanya kama walivyokuwa wanafanya wazazi wetu zamani, nenda studio piga picha safisha weka kwa album, kwa kuwa unapenda show off (wageni wakija wape waangalie).

Wakiondoka si wataacha album nyumbani fresh "You are safe" ila usije ukajidanganya kwamba wewe utaendelea kupost picha tu kwasababu haupost picha mbaya.

Unajipa moyo kuwa unavaa kiheshima kwahiyo huoni uoga kujipost (my dear upo hatarini) hivi umesahau tuko ulimwengu wa teknohama eeeh umesahau.

Si eti, unataka jitoa ufahamu hujawahi ona editing wanazofanyiwa watu (acha ni assume hujawahi). Sasa nikwambie kitu, achana na kupost mapicha kwenye masocial media, ipo day moko utanikumbuka nakwambia tena.

Wengine mnawapost watoto zenu aseee mnakosea nasema mnakosea (mnawaonea hao watoto mnajua) subirini wakikua wajiamulie maisha yao.

Usimpost mwanao wewe mama, usimpost mwanao wewe baba kaa na mwanao ndani jaribuni kuelewa hata kwa ufupi somo lile la "privacy and security".

Mimi leo hiii kuna picha zangu nilizipost kwenye akaunt zangu mahali mahali flani, sasa nimesahau password ya kule, bwana wee shida ninayopata kuzitoa zile picha kule zilipo si ndogo.

Sikulazimishi unielewe kama kawaida yangu mimi naandika ila uamuzi ni wako.

Ukiamua kusoma tu ukiamua kusoma na bila kuchukua hatua ni wewe, ila mpaka siku utakapokutana na picha ako imeeditiwa vilivyo ndio tutakumbukana.

Nime Finish.
Nahisi Instagram wakitoa kitengo cha like ndipo wana JF watakuelewa mkuu
Binafsi nimekuelewa
 
Kuna mmoja nilimsikia akisema wachawi hutumia picha kwenye mambo yao,anaweza kukushughulikia kwa kutumia picha yako,watoto wako wanaweza kupigwa kombora kwa kuwa mtu mmoja yeye hajaganikiwa kupata watoto sasa hapendi kukuona una watoto
 
nina Muda mwingi sana wa kushinda na Computer mbele yangu

kuliko muda hata wa kutembea kwenda toilet au muda ninao jipa break kwenda Kula

na kunyoosha viungo kidogo,nikisha jinyoosha tu Narudi kwenye screen.
BA's sawa mzee
 
Kuna mmoja nilimsikia akisema wachawi hutumia picha kwenye mambo yao,anaweza kukushughulikia kwa kutumia picha yako,watoto wako wanaweza kupigwa kombora kwa kuwa mtu mmoja yeye hajaganikiwa kupata watoto sasa hapendi kukuona una watoto

Hatari
 
umeshawahi jiuliza kwanini wenye albinism hawaji post ovyo??

lazima unajua kwanini, sasa kwakua unajua hvi unajua mimi nikienda kwa mganga leo

akaniambia nitafute mtu mwenye kitu flani,then pita pita kwenye mtandao naona kile kitu kipo kwako au kwa mwanao

unafikiri kitakachofuata ni nini? unafikiri watu wote wanaopotea hutekwa kisa PESA?? fikiria upya mkuu
Kaka kama unaamini uchawi na ushirikina wa kutumia picha hilo ni lako....mimi navyojua ni kwa sababu ya Security na Privacy ya mtu...sasa hoja yangu mimi kapuku naishi chini ya dola moja kwa siku nahofia nini juu ya Privacy yangu...nina nini mimi hadi eti nifikirie kupost ka picha ka kangu ka birthday pale Facebook in risk?
 
Kuna mmoja nilimsikia akisema wachawi hutumia picha kwenye mambo yao,anaweza kukushughulikia kwa kutumia picha yako,watoto wako wanaweza kupigwa kombora kwa kuwa mtu mmoja yeye hajaganikiwa kupata watoto sasa hapendi kukuona una watoto
Ujinga, Kama ni hivyo picha za matajiri amina MO wangekuwa wanazisaka balaa na hadi sasa hivi wangeshamfanya msukule....nyie ndiyo huwa mnaogooa hata kujenga makwenu vijijini kisa kuogopa kurogwa!!
 
Miezi minne iliyopita alichwa madada sababu ya Facebook, sasa anahangaika ila ndiyo hivyo milango ya neema ishafungwa.

Back
Top Bottom