Dunia imebadilika, acheni kupost post mapicha yenu huko mitandaoni

Dunia imebadilika, acheni kupost post mapicha yenu huko mitandaoni

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,087
Reaction score
23,870
Nilikuaga sielewi kwanini kuna sehemu ukipita huruhusiwi kupiga picha, nilikuwa hata sijui kwanini. Nilikuwa sifahamu kwanini familia flani flani hasa za kifalme sio watu wapenda mapicha picha, kujionyesha onyesha.Nilikuwa sitambui kwanini yote hayo ni "marufuku" kwa aina flani ya watu nilidhani tu sababu ya vyeo na nyadhifa zao.

Lakini sasa nimeelewa kwanini yote hayo yalikuwa yanafanyika, na ninakubaliana nao kuwa walikuwa na wapo sawa hata na sasa. Wote ni mashahidi jukwaaa la MMU watu wakitafuta wapenzi, kwenye social networks tofauti watu wakitafuta wapenzi. Picha nyingi zimekuwa zikitumika huko, na nyingi kati ya picha zinazotomika si za wahusika wenye picha wenyewe na wala wao hata hawajui.

Kama kuna jitu lipo huku linatumia picha yake kudanganya watu, matukio ya namna hiyo ni mengi sana. Umeshawahi kukaa chini ukajiuliza hizo picha wanazitoa wapi? Jibu najua unalo ni humu humu mitandaoni kwenye hizi social media. Ndugu zanguni yawezekana hujawahi ona picha yako ikiandikiwa tangazo ndio mana unaona kama hii haikuhusu ila nataka tu kukwambia "ipo siku".

Ipo nini nimesema? (in teacher mpamire's voice)

Nataka kukwambia nini wewe dada wewe kaka hebu leo kata mazoea ya kujipost post huko kwenye mitandao, kama unapenda picha fanya kama walivyokuwa wanafanya wazazi wetu zamani, nenda studio piga picha safisha weka kwa album, kwa kuwa unapenda show off (wageni wakija wape waangalie).

Wakiondoka si wataacha album nyumbani fresh "You are safe" ila usije ukajidanganya kwamba wewe utaendelea kupost picha tu kwasababu haupost picha mbaya.

Unajipa moyo kuwa unavaa kiheshima kwahiyo huoni uoga kujipost (my dear upo hatarini) hivi umesahau tuko ulimwengu wa teknohama eeeh umesahau.

Si eti, unataka jitoa ufahamu hujawahi ona editing wanazofanyiwa watu (acha ni assume hujawahi). Sasa nikwambie kitu, achana na kupost mapicha kwenye masocial media, ipo day moko utanikumbuka nakwambia tena.

Wengine mnawapost watoto zenu aseee mnakosea nasema mnakosea (mnawaonea hao watoto mnajua) subirini wakikua wajiamulie maisha yao.

Usimpost mwanao wewe mama, usimpost mwanao wewe baba kaa na mwanao ndani jaribuni kuelewa hata kwa ufupi somo lile la "privacy and security".

Mimi leo hiii kuna picha zangu nilizipost kwenye akaunt zangu mahali mahali flani, sasa nimesahau password ya kule, bwana wee shida ninayopata kuzitoa zile picha kule zilipo si ndogo.

Sikulazimishi unielewe kama kawaida yangu mimi naandika ila uamuzi ni wako.

Ukiamua kusoma tu ukiamua kusoma na bila kuchukua hatua ni wewe, ila mpaka siku utakapokutana na picha ako imeeditiwa vilivyo ndio tutakumbukana.

Nime Finish.
 
Picha kuhifadhi kwa hardcopy ni primitive sana
Unaweza kuhifadhi kwa njia hata ya email bila mtu mwingine kuziona. Hata fb unaweza ukazipiga pin vilevile zisionekane
ni kweli ila kuzihifadhi kwa FB si salama wengine tuna assignement zetu tunaa ambiwa Hack akaunt ya flani

unafanya attempt kitu kimo,sasa wanafunzi wengine hutumia mafunzo hayo tofauti na lengo

labda uzihifanyi kwenye hard disk,flash,memory,online drives,nk ila sio huko kwenye ma social networks
 
Yani mtu atumie nguvu zake na muda wake kumhack mtu ili achukue picha tu? Halafu akafanyie nini hiyo picha?

Unaweza kuhifadhi kwa njia ya album halafu mchwa wakazipitia zote
 
Wazo nzuri ila sometimes kuna faida zke kwa upande mwingine tuchukulie kama yule dogo mtanzania aliye pigwa risasi south africa amby mshana jr kapost picha yake juz ili kuwa tafuta ndugu na jamaa zake bila ya kua na picha ambzo kapost mtandaoni watu wange mjuaje? Kwa kutumia jina tu na tuna fahamu fika kwamba now dayz kuna baadhi ya watu wana fahamika zaid kwa A K A kuliko hata majina ya kuzaliwa nayo
 
ni kweli kwa condition ya namna hiyo nakubaliana na wewe kuna faida

ila tuangalie kwenye faida na hasara wapi penye faida sana na wapi hasara.
 
Picha kuhifadhi kwa hardcopy ni primitive sana
Unaweza kuhifadhi kwa njia hata ya email bila mtu mwingine kuziona. Hata fb unaweza ukazipiga pin vilevile zisionekane
Niliwahi kusikia watu wakilalamika kuhack a/c zao kidogo labda hiyo e-mail yaweza kuwa siri yako pekee mbona kuna app inaitwa photo huifadhi picha,videos yenyewe hata ukifuta files bado hubakia vlvl hata ukipoteza simu
 
Bado huwezi kuzuia.. Ndomaana kwenye account za social media kuna sehemu ya Ku report pale inapotokea kuna MTU kapost kitu usicho pendezwa nacho..

Kumbuka mficha uchi hazai.. Sasa wewe uwe na social media bila picha yako itatusaidia nini sasa wengine muda wakutafuta wapenzi hatuna at I.. May be through social net inaturahisishia kidogo..
 
Huwezi kuzuia social media kufanya kazi zake. Ulimwengu huko mbali sana na mawazo ya mtoa mada ambayo ni ya kizamani. Kuna njia nyingi sana za kutafuta furaha na mojawapo ambayo ni ya kisasa ni social media. Dunia ya sasa ina upweke sana ndio maana watu wanatumia social media kujichangamsha na at least kuwa social

Wewe utakuwa mtu Fulani wa mwaka 47 hivi unataka kuleta issue za albam za picha za hardcopy kipindi hiki cha maendeleo ya sayansi na teknolojia. Usishindane na wakati dunia inaenda kasi sana, nyie ndio mnahifadhi hela kwenye mabegi ndani hamziamini hata benki
 
Niliwahi kusikia watu wakilalamika kuhack a/c zao kidogo labda hiyo e-mail yaweza kuwa siri yako pekee mbona kuna app inaitwa photo huifadhi picha,videos yenyewe hata ukifuta files bado hubakia vlvl hata ukipoteza simu
yeah uko sahihi

kuhifadhi kwa njia ya kupost kwenye social media,bado si salama

solution ni kufanya kama ulivyoshauri,au kutafuta namna nyingine.
 
Amigoh,
we mjamaaa una faida na hizo picha huko unaonyesha

😂 😂 😂
 
Wewe hiyo avatar ungeipata wapi kama Huyo jamaa angekuwa na old fashioned perception ka hizi !?

Fanya yako usiamulie watu maisha.

Mimi Picha ya Kells ningeitoa wapi!??
una uhakika huyu jamaa ni yeye kama unavyoiona hiyo avatar yangu?

wewe umeamua kuweka picha za watu na huo sio ujanja bali ni kinyume cha sheria

usilete pigo za kusema old fashion,so wewe ulie updated unaona sawa kutumia picha za wengine bla kibali?
 
Back
Top Bottom