Dunia haitendi haki kabisa

Peculiar

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
821
689
Maisha haya bhana acha tu, kila mtu anatembea akiwa na yake kifuani,kichwani na moyoni! Hasa kwenye swala la kuoa/kuolewa.

Unampenda John ila utaolewa na Juma, kwa sababu Juma ana maisha mazuri. Inauma sana!

Huwezi kumuoa Hawa kwa sababu sio dini moja, na ukibadili dini "wewe sio ndugu yetu! Inachanganya sana!

Inauma sana kusikia unayempenda anaolewa/anaishi na mtu. Kisa WAZAZI/PESA/DINI/ELIMU. Mnaishia tu kumezeana mate. DUNIA haijataka muwe pamoja.

Unaishia kumuoa/kuolewa na mtu ambaye si aina yako, miaka na miaka humzoei. Hupati faraja kutoka kwake. Hujisikii hata muwe na familia, moyo haupo kwenye ndoa zaidi ya kutimiza majukumu tu!

Inauma!!
 
Mbona umejaa hofu na maahaka?
Hutupati tutakayo ila tunapata tuliyojaliwa.
Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu ila jawabu la ulimi hutoka kwa Bwana.
 
10522144_10154515378203009_3989148787714674990_n.jpg
 
ah ukitakamambo ya ndoa ndio utaona world sio fair ila ukiwa mzee wakugegeda wala hupati tabu...wewe watafuta pesa kisha unajigegedea tuu warembo utakao
 
Vipi mrembo na wewe tiyare ushaolewa.??

Au bado unasubiri man of your dream??
Si kwamba hauoi au hauolewi! No!!ila mtu unaoa/unaolewa.lakini unaemuoa/anaekuoa hajazi moyo wako,hata ukimuangalia daa! Unajitahidi tu asijue kuwa haupo mahala sahihi,licha ya kuwa na watoto pengine na kila kitu.
Lakini faraja na amani yako hauipati kwa mumeo/mkeo.
 
Back
Top Bottom