Dully Sykes: wasanii wa Bongo Fleva wamekuwa kama Kaa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515

060002049508127_0.jpg

Msanii wa Bongo Fleva, Dully Sykes amewalalamikia wasanii wadogo kiumri kwenye muziki wa Bongo Fleva kwa kukosa upendo na umoja baina yao kwa kutokupeana sapoti kwenye kazi zao.

Dully amesema Wasanii wanaofanya vizuri kwa sasa kwenye muziki ambao amewaita madogo hawana upendo wala umoja katika kusapotiana na kudai kuwa sio tu kwa wasanii wakongwe bali hata hao wenyewe kwa wenyewe na kuwafananisha na mdudu Kaa.

“Vijana wa sasa hivi wanatakiwa wajifunze kupendana, vijana wa sasa hivi hawapendani yaani hawana mapenzi, hawana ule upendo wamekuwa kama Kaa, Mimi nilijaribu kutuma posti yangu (ya wimbo mpya) juzi nikitegemea kupata nguvu nyingi kutoka kwa vijana lakini imekuwa tofauti na nilivyofikiria kwani wazee wenzangu ndio wamenipa sapoti akina Rich One, akina Mwana FA ndio walinisapoti na ndio walikuwa na furaha, kuna vijana wengine mpaka wanasema kwamba nimetoa wimbo lakini hawajui kama mimi nimetoa wimbo, wengine wanasema nitakupostia lakini hawaposti.“amesema Dully Sykes kwenye mahojiano yake na Radio Free Afrika Kwenye kipindi cha New Chapter na kuwapa ushauri wasanii hao

“Sasa mimi naomba tu kuwambia wale vijana ambao wanahisi labda muziki ni wa kwao peke yao hapana.. Unajua Mungu sisi wengine sisi ametupa utofauti mimi nakula majani kama Twiga wakae watulie, hao watakula majani chini kama Mbuzi, mimi nitakula ya juu, Wakae watambue kuwa wasishindane na Tembo wataumiza makalio.”


Muungwana
 
Hao Vijana wengi ni Watumwa wa Umaarufu jambo ambalo linawapelekea kuwa na Kiburi hadi kwa wale waliochangia wao kufika hapo..,
 
Ungemwambia Jay Moe akusaidie kushare...
Hivi Dully Sykes ni mtu wa kulialia eti wasanii hawajampost kweli?? Kama kashindwa kutengeneza fan base asimlaumu mtu, ni uzembe wake mwenyewe!!
 
Dully kama ukiona haupewi support ujue ndo haulipi kweny soko la sasa.Tafuta tu kazi nyingine,mziki ulishakuacha kitambo
 
Dully komaa na uproducer usanii umekupita mkuu....mammbo ya kuimba henkehe ehenhehe yamepitwa ..sahivi ni aga kokolo
 
Back
Top Bottom