Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Mkuu singida na Mbeya ni jirani sana via Chunya road! So waweza nunulia pale Maranatha Mwanjelwa Branch, wana bei nzuri sana!
 
Hongera kwa wazo lako ziri.

1. Tafuta eneo unalokusidia kufanya hiyo bishara.
2. Nenda ofisi za TFDA hapo Singida, kachukue form ya maombi utaijaza utakapoijaza na kuirudisha ukirudisha watakupangia siku yakuja kuangalia na kuikagua, kama utakidhi vigezo utapewa kibali, kama haitakuwa na vigezo watakufahamisha hayo mapungifu.

Kuhusu maduka yajumla. pia kuna tofauti ya vigezo kati ya pharmacy na duka la dawa muhimu.

Ahsante Sana nimekuelewa nashukuru nimepata mwanga
 
Awe na cheti toka chuo cha afya kinachotambuliwa na serikali. Labda kama unahtaj dawa muhimu ni mpaka awe na TFDA
 
Mtaji utategemea na namna ya duka unalotaka kuanzisha lakini ili duka lionekane hasa ni duka si chini ya 20M.

Taratibu za kisheria ni lazima uwe na cheti cha mfamasia ambacho ndy utatumia kufungua hilo duka,pia uwe na muuzaji
ushauri mzuri

au wauzaji waliosoma kozi za maduka ya dawa muhimu na pia kozi hiyo ipo pia kwa wamiliki wa maduka pia inatakiwa

usomee,hizo kozi zilikuwa zinafanyika wilayani na mikoani kuanzia mwaka jana sijui sasa kwa ambao hawakusoma mwaka

jana utaratibu ukoje na pia sina uhakika kama imeshaisha tanzania nzima.

Walikuwa wanasisitiza hivyo ndiyo vitakuwa vigezo hasa sijui lakini tofauti na hapo inakuwaje,watakuja wengine kukujuza

zaidi.

Kuhusu usimamizi sijaelewa unamaanisha usimamizi wa namna gani?..

Ili mali yako isipotee wengine wanauza mtu wako unayemwamini kazi yake ni kupokea pesa.

Ni biashara inayolipa sana ukiwa sehemu nzuri na wahudumu wazuri bila kusahau kuwa kidigitali zaidi..
Ushauri mzuri
 
Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa wana jamii forum kwa misaada ya kimawazo tunayopeana,pili naomba kufahamishwa vigezo muhimu vya kufata wakati wa kufungua duka la dawa muhimu maana nasikia kuna masharti mengi sana pamoja na kujuana.naomba msaada wenu wandugu.
 
Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu kwa wana jamii forum kwa misaada ya kimawazo tunayopeana,pili naomba kufahamishwa vigezo muhimu vya kufata wakati wa kufungua duka la dawa muhimu maana nasikia kuna masharti mengi sana pamoja na kujuana.naomba msaada wenu wandugu.

Kwa baadhi ninazojua mim ni kwanza lazima hilo duka lako lazima liwe na store ninamaanisha hicho chumba uweze kukigawa na upate na store,pia uwe na makabati ya vioo,kabla ujafungua ukishaandaa unaenda TFDA wanakuja kukagua ili wakupe cheti hapa tofauti na muuzaji hizi ni hatua za awari tu,kama kuna za ziada ngoja niwaachie wengine.
 
angalia hii habari iliyotoka 2012 nadhani itakupa mwanga...

TFDA yanadi maduka dawa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];mseto'

By Leonce Zimbandu
21st August 2012

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA)

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imesema ni ruksa Mtanzania yeyote mwenye umri unaozidi miaka 18, kufungua duka la dawa muhimu za Binadamu na Mifugo (DLDM), hasa katika maeneo ya Vijiji na Miji midogo ambapo upatikanaji wa dawa muhimu ni wa matatizo.

Ofisa Uhusiano wa TFDA, Gaudensia Simwanza, aliwaambia waandishi wa habari mwishoni mwa wiki iliyopita kwamba watakaofungua maduka Vijijini watapewa kipaumbele kwani watu wengi yamejikita kufungua maduka hayo maeneo ya mijini.

Alisema mwombaji anapaswa kuwa tayari kupitia mafunzo ya mwezi mmoja ili kujua sheria na kanuni za uendeshaji wa maduka hayo, ili kuonyesha utofauti wa uedeshaji duka la dawa baridi na moto ambapo wamiliki wake walikuwa hawana uelewa.

Simwanza alisema kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa DLDM, mmiliki na mtoa dawa wanalazimika kuingia mkataba wa kazi kwa lengo la kusimamia utendaji, kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kulinda maslahi ya pande zote mbili.

Alisema DLDM ni maduka ya kutunza na kuuza dawa zisizohitaji cheti cha daktari na baadhi ya dawa hizo kuhitaji cheti cha daktari.

Mtoa dawa katika maduka hayo ni lazima awe na sifa za awali kama fundi sanifu, ofisa muuguzi, tabibu na mhudumu wa afya au wawe wasaidizi katika ngazi hizo.


SOURCE: NIPASHE
 
Nahitaji kufanya hiyo biashara , lakini ningependa kujua start up capital pamoja na gharama za kumlipa mfanya kazi na mahitaji mengine ya msingi kama vibali kutoka tfda maana leseni ya biashara nitaipata haina shida.
Biashara hii nataka niifungulie DSM

Hapo kwenye heading ni dawa muhimu

Nitashukuru kwa msaada wenu
 
Hivi 'duka la dawa baridi' maana yake ni nini hasa?

Kuna dawa baridi na za moto, au?
 
Hivi 'duka la dawa baridi' maana yake ni nini hasa?

Kuna dawa baridi na za moto, au?

Mkuu mimi sio doctor lakn kwa uelewa wangu ni dawa ambazo ziepitia kiwandani tofauti na dawa za miti shamba sasa siku hizi wamebadili wanaita dawa muhimu sasa sijui waje wataalam watuambie. Maana mimi nataka kufungua hiyo biashara
 
Kwanza nikupongeze kwa uamuzi wa kuamua kufanya biashara.
ushauri wangu ni kwamba jaribu kudadisi kwa wauzaji wa hizo pharmacy waliotangulia ambao wana moyo na nia ya kukusaidia japo kwa mawazo. kwa msaada zaidi wasiliana na mawakala wa Msd hapo mjini wapo wengi.

Wish u all the best.
 
Kwanza nikupongeze kwa uamuzi wa kuamua kufanya biashara.
ushauri wangu ni kwamba jaribu kudadisi kwa wauzaji wa hizo pharmacy waliotangulia ambao wana moyo na nia ya kukusaidia japo kwa mawazo. kwa msaada zaidi wasiliana na mawakala wa Msd hapo mjini wapo wengi.

wish u all the best.

Thanks mkuu nitafuata ushauri wako
 
Nokla;9631004 said:
Thanks mkuu nitafuata ushauri wako
Nikushauri yafuatayo:

1. Duka la dawa baridi, limefutwa kisheria na sasa yapo maduka ya dawa muhimu. Dawa muhimu ni dawa za msingi zilizoruhusiwa kuuzwa kwenye maduka haya, kwa cheti cha daktari. Dawa baridi ni zile dawa zisizohitaji cheti cha daktari.
2. Duka la dawa muhimu linaruhusiws kufunguliwa pembezoni mwa mji sehemu zisizo na huduma ya dawa.Yapo maeneo yaliyoainishwa kwa DSM.
3. Nenda ofisi za Baraza la Famasi mabibo external zilizopo pia ofisi za TFDA kwa ufafanuzi zaidi.
 
Kama kichwa kinavyodai hapo juu

Nahitaji duka la dawa muhimu, kwa kuwa kufungua/kuanzisha ni ngumu kwa sasa nimeamua kutafuta la kununua yaani kibali na jina, hata likiwa location yoyote kwan lengo langu ni kulihamisha.

Angalizo; lisiwe limetiwa doa na TFDA yaani kama kupewa onyo la kufungiwa ama kukiuka taratibu za mamlaka ya chakula na dawa.

OFFER capital 2.5mil inaweza kupanda kulingana na makubaliano ama kushuka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom