Duka la Dawa Muhimu za Binadamu (Pharmacy): Utaratibu wa Kufuata na Mtaji wa Kuanzisha Biashara

Ninalotaka kuanzisha ni duka la dawa baridi. Laut

Nasikia wakitangaza kuwa siku hizi ni siyo duka la dawa baridi ila ni duka la dawa muhimu.

Kwa hisani ya watu wa Marekani.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Ili kuanzisha duka la dawa Muhimu (zamani duka la dawa baridi, siku hizi yamefutwa, unayoyaona hayatafika July), kwanza ni lazima Iwe nje ya Mji.

Mahali ambako hakuna Maduka makubwa (Pharmacy), pia ni lazima uwe umepata mafunzo ya namna ya kuendesha Duka la dawa Muhimu yanayotolewa na TFDA on behalf of Ministry of Health and social Welfare (hiyo ni lazima).

Kumbuka pia kuwa watoa dawa wako (wauzaji) ni lazima wawe wamepitia Mafunzo ya utoaji sahihi wa dawa yanayotolewa na TFDA, ukikamilisha hayo nenda ofisi ya Mganga Mkuu (pharmacy Department) Kwenye halmashauri au Manispaa inayohusika utasaidiwa.
 
Kuna ukiritimba mkubwa sana kama huna pesa ya kuhonga mfamasia wa wilaya usitegemee kupata leo.Ila kama ni famasi unatafuta cheti cha mfamasia unakilipia si chini ya sh.milion kila mwezi alafu unatafuta mtu yoyote anayejua majina ya dawa anakaa dukani kuuza dawa!

Uzuri hawa jamaa ukishaweka cheti cha mfamasia tu dukani hilo duka wataliheshimu sana!Ole wako uwe afisa tabibu alafu ufungue duka la dawa baridi halafu wakukute unauza antibiotic, utadhalilishwa kama hujaenda shule ingawa ukiwa hospitali yoyote wewe ndo unawaandikia dawa hizo wagonjwa!

Kifupi tu funguka mkwanja kwa mfamasia hata kama huna cheti huwa wanajua jinsi ya kufanya utapewa hata kopi ya mtu aliye dedi.
 
Habadi wana JF

Nina mtaji wa Tshs. 20M na nimefikiria kuanzisha biashara ya duka la Dawa za Binadamu hapa Dar Es Salaam.

Kwa wataalamu na wenye uelewa wa hii biashara, naombeni mnisaidie mnyambulisho wa nini kinachotakiwa kufanyika ili hii Biashara iwe na mafanikio na maendeleo zaidi.

Taaluma yangu ni Mwalimu wa sekondari na ninataka kufanya biashara katika eneo hili linalooneka kuwa na mahitaji makubwa sana kwa Watanzania.

Naombeni msaada wenu wa mawazo na kama kuna mwongozo naweza pia kuupata, naomba upost humu kwa manufaa wa watu wengine pia.

Shukrani na mapumziko mema nyote
 
Pale karibu na Mkapa International Market kuna taasisi ya serikali kuna kitengo cha uthibiti wa biashara hiyo, watakuelekeza aina gani za dawa zinazoruhusiwa na wapi source ya kuzipata. Kama utaleta nje ya source zinazokubalika kitaifa itabidi kila dawa aina ya dawa uipeleke kwa wahusika na maelezo ya manufacturer na kila dawa utailipia $100 kisha utakuwa huru to import.
 
Basat na Candid, nashukuruni sana kwa michango yenu.

WanaJF, mwenye ideas na views tofauti! Location gani kwa Dar ni nzuri, Risks involvedvi, Opportunity, Strategews.

Advise please
 
Hiyo biashara inalipa sana kitu cha muhimu ni kupata location ambayo ina flow ya watu kwa wingi.Vitu vya kuzingatia ni
  • Location
  • Competitors
  • Wafanyakazi waaminifu
  • Vifaa (frame,Ac,)
  • Kibali toka TFDA
Kwa maelezo zaidi tembelea website ya TFDA
 
Kwavile biashara yako ni pharmacy unatakiwa uende katika pharmacy council ya wilaya yako utapata maelezo yote hapo.
 
Shukrani sana Bela na Basat

Michango yenu ni muhimu sana na nitaifanyia kazi kwa umakini kwa kufanikisha malengo yangu
 
Maria, inamaana askari ambaye hana fani yeyote asifungue biashara yeyote katika maisha yake au ndo afungue biashara ya kampuni ya ulinzi?
 
Kwa 20 m, ni zaidi ya duka la dawa mhimu, bali hata phamacy! good business idea, but needs a good ROAD MAP, (BUSINESS PLAN), andaa au tafuta mtaalamu akuandalie ili iwe njia yako ya kufanya monitoring and evaluation kwa muda wote wa business yako. Very important! unaweza ni PM pia kwa kazi hiyo.
 
Ninalotaka kuanzisha ni duka la dawa baridi. Laut

Ndugu yangu, naomba na mimi nikupe mwanga zaidi kwa faida ya wengine.

Kama baadhi walivyosema, kutokana na mabadiliko ya sheria, Tanzania kwa sasa hakuna maduka ya dawa baridi. Tuna maduka ya dawa muhimu (DLDM). Maduka haya yameanzishwa kutokana na utafiti uliofanywa na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) mwaka 2001, na kubainisha mapungufu mengi ambayo yalikuwa yanafanywa katika maduka ya dawa baridi (DLDB). Mojawapo ni kuuza dawa zisizoruhusiwa kisheria kwa kutumia watoa dawa wasio na sifa; kugeuza maduka kuwa maabara na dispensaries na kadhalika.

Kwa ufupi tu, kutokana na hali hiyo, na kwa kuwa Tanzania ilikuwa ina huduma duni ya dawa kwa wananchi walio wengi, (ambao wanapatikana na vijijini na miji midogo), serikali ikaamua kuanzisha mpango wa DLDM kwa lengo la kuondoa matatizo yote yaliyobainishwa kwa utafiti. Pili ilikuwa kuruhusu dawa chache za msingi (few essential medicines) ziwepo kwenye maduka hayo, na watoa dawa wake wapate mafunzo maalumu, ili huduma ziwe bora na za uhakika katika maeneo ya rural, periurban na maeneo maalum yaliyoruhusiwa ambayo hakuna duka la Famasi.

Ili kuweza kuhakikisha haya, ngazi zote za utendaji, yaani ngazi ya kijiji au mtaa, ngazi ya kata, ngazi ya wilaya na mkoa wanahusishwa moja kwa moja katika utekelezaji wa mpango huu.

Sasa utaratibu ni huu:

1. Chukua fomu ya kuanzisha fomu ya kuanzisha DLDM kwa mfamasia wa wilaya unayotaka kufungua duka. Ijaze sehemu A, ukiwa umeambatanisha vyeti vya kuhitimu mafunzo maalumu yaani mmiliki na mtoa dawa, mkataba wa kazi baina ya mmiliki na mtoa dawa, pia commitment letter ya mtoa dawa katika duka hilo. Kama wewe ni mmiliki na pia ni mtoa dawa, huna haja ya kukusanya mkataba huo.

2. Fomu ipeleke ofisi ya kijiji au mtaa ambao duka litakuwepo. Wao watajaza sehemu B.

3. Fomu itapelekwa kwa ofisi ya Kata, watajaza sehemu C. Wakaguzi zaidi ya mmoja watakuja kufanya ukaguzi wa eneo na jengo kama linakidhi vigezo.

4. Fomu itapelekwa ngazi ya wilaya, na kabla hawajajaza sehemu D, watatakiwa kufanya ukaguzi tena kwenye eneo na jengo lako, na kuhakikisha mtoa dawa wako amepatiwa mafunzo. Kama kuna marekebisho utaelezwa na uyafanyie kazi. Lakini kwa kupitia kamati yao ya Chakula na Dawa inayoongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Manispaa, itakaa kikao na kuyapitia taarifa za ngazi zote, na za ukaguzi. Maduka yaliyokidhi vigezo, yanapendekezwa sasa kwenda Baraza la Famasi (Pharmacy Council) waweze kutoa vibali. Ukishapata kibali unatakiwa urudi tena kwenye halmashauri au wilayani ukapate Leseni ya Biashara.

Nahisi nimekupa mwanga kidogo zaidi, ila kama ningekuwa na email yako, ningekutumia Kitabu cha mwongozo kinachosimamia mpango huu.

Thank you

Mwananchi mwenzenu.
 
Biashara mpya mara nyingi huwa inakula sana mtaji na changamoto zake huwa ni kubwa kidogo maana ndo unaanza from the ground. Mimi nipo kwenye biashara hiyo ya maduka ya dawa toka mwaka 2005, hadi sasa ninayo mawili. Ninakushauri usitumie mtaji wako wote kuanzisha biashara hiyo, anza kidogo kidogo huku ukiisoma biashara na kuizoea ukiwa na akiba ya kukabiliana na changamoto zake.
 
Na mimi pia nilikuwa naomba msaada kwa phamacy. Minimum capital kwa ajili ya dawa tuu ukiachana na mambo ya. A.C., matengenezo ya ofisi na usajili. Inaweza akifikia mpaka kiasi gani kwa kuanza na dawa ambazo ni major.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Heshima mbele waungwana,

Mimi ni mjasiliamali aambye Nimekuwa nafanya biashara mbalimbali kwa muda sasa, pamoja na kuwa nimeajiliwa, lakini bado namudu kufanya biashara na kusimamia kwa kiasi kikubwa. Baada ya kufanya utafiti mdogo nimegundua kwamba kuna maduka makubwa machache sana ya kuuza madawa yenye kiwango cha Pharmacy, na kwa kuwa kazi kubwa ya mjasiliamali ni kubeba Risk na Ku - Capitalise on Discripancies, nataka kujaribu biashara hii.

TafadhaLI WAUNGWANA, kwa mwenye UELEWA wa:

1. Mtaji unaohitajika
2. Namna ya kusimamia
3. Taratibu za kisheria zinazotakiwa
na mambo mengine mengi ambayo yanaweza kunisaidia kufanya biashara hii.

Nawasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom