Mdakuzi
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,293
- 6,901
Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe alikuwa na yake kwenye jukwaa la Malaika Band ndani ya ukumbi wa Mango Garden, IJumaa iliyopita (16 January 2015).
Zitto alipanda jukwaani wakati Christian Bella akiimba wimbo wake wa Nani Kama Mama, Mheshimiwa akachotwa na hisia za wimbo huo hadi mchozi mwembamba ukamtoka (bila shaka ni kwa kumbukumbu ya msiba wa mama yake mzazi uliotokea mwaka jana), lakini baadae akaimarika na kuthubutu kuuimba wimbo huo.
Mheshimiwa Zitto akaucheza pia wimbo huo, mashabiki wakamiminika jukwaani kupiga naye picha, kwa muda wa takriban dakika 20 alizosimama jukwaani, mbunge huyo akadhihirisha kuwa ni mtu wa watu, Mango Garden ilisimama kwa muda.
Kama kuna mapedeshee waliokuwepo Mango Garden, basi jana walizima ngebe zao, Zitto alifunika, alitunza pesa nyingi sana. Christian Bella peke yake alipokea zaidi noti 50 za elfu kumi kumi kutoka kwa Zitto huku zingine zikiwa ni dola za Kimarekani. Watu wanatumia pesa bwana!
Chanzo: Blog ya Saluti5
ZITTO KABWE AFANYA âKUFURUâ MALAIKA BAND MANGO GARDEN â¦awatia wazimu mashabiki, alizwa na wimbo âNani Kama Mamaâ, maelfu ya pesa zamtoka jukwaani