vukani
JF-Expert Member
- Dec 30, 2009
- 244
- 166
- Thread starter
- #41
Hodi kwenye Jukwaa hili wakuu. Naomba na mimi nichangie kidogo. Hili suala la kujisifu kwa wanaume (ego) limeletwa na Mungu mwenyewe katika Mwanzo 3:16 ambayo inasema kwa sehemu kama ifuatavyo: "...tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." Kwa hiyo mtawala ndani ya nyumba ni mwanaume tu hata kama ni maskini namna gani, utakuta mwanaume anajitutumua tu!
Kwa hiyo hapa asilaumiwe mwanaume kwa kitu alichopewa na Mungu!
Jambo jingine ni logic tu, kwamba nyumba haiwezi kuwa na viongozi wawili, lazima kuwepo na mwenye maamuzi ya mwisho! Bahati nzuri Mungu alishamteua mtu huyo kama nilivyosema hapo juu!
Hewala mkuu.
Lakini mbona pamoja na kupewa mamlaka hayo na Mungu, lakini pale itokeapo mwanamke akam- criticize mwanaume japo kidogo tu, yeye anaishiwa na nguvu kabisa. mimi nilitarajia atatumia maguvu hayo kujitutumua na kuonyesha kwamba hayuko hivyo kama navyofikiriwa.
Hebu chukulia mwanaume anaambiwa na mpenzi wake mara baada ya game kuwa hajaridhika kwa sababu jamaa ana kibamia na hajamfikisha kileleni,....
Unatarajia huyu mwanaume atajona vipi mbele ya wanawake na wanaume wenzie?
Kwa mwanamke is not a big deal kukosolewa, inaweza kumuuma lakini sio kwa kiwango kama cha mwanaume, kumbuka huyu mwanaume ndiye aliyepewa mamlaka na Mungu! halafu akosolewe na kiumbe alichoambiwa kwamba yeye ndiye kichwa cha hicho kiumbe!
Je, una maoni gani juu ya hilo mkuu?