snowhite
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,422
- 25,322
Hahaha ngoja akupashe na upashike na mvuke tuuone...
sasa kama wewe bouncer wangu wa mineno ukiniacha nyikani hivi si nahama mji mie!lol
Hahaha ngoja akupashe na upashike na mvuke tuuone...
Hivi unajua watengeneza vipindi huchagua kile wanachoamini kwamba kitavutia katika masikio ya wasikilizaji?
Kwanza mie sisikilizi hiyo redio kabisa.
sasa kama wewe bouncer wangu wa mineno ukiniacha nyikani hivi si nahama mji mie!lol
Kuna mambo madogo madogo yanayowahusu wanaume huwa watu wengi hawayaoni na kufanya tafakuri. Katika makuzi yangu nimegundua udhaifu ambao wanaume wengi wanao lakini hausemwi kwa sababu ya mfumo dume kutawala. Nimegundua kwamba sifa ndio inayowauwa wanaume wengi, kwa kutaka kwao, kuimarisha mfumo dume walionao (ego)
Nitajaribu kueleza kidogo kuhusu maana ya hili neno ego, kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, naomba munirekebishe kama sitapatia. Kwa mujibu wa nadharia za wanasaikolojia ego ni yale tuliyofundishwa na jamii kwa ujumla, yaani yale tuliyoambiwa kwamba ni mabaya au mazuri kwa mujibu wa jamii. Kwa mfano wanaume wamefundishwa kwamba wao ni kichwa cha nyumba, wao ndio wenye maamuzi sahihi, hawakosei, wana akili kuliko wanawake, wana mamlaka juu ya wanawake, wao ndio wanaotakiwa kuchumbia kulipa mahari na kuoa, na mambo mengine mengi tu unayoyafahamu.
Kwa hiyo ndio sababu utakuta wanaume wanapenda sana sifa, wanataka wanawake wawaone kwamba wao ndio bora kabisa na wasioshindwa na jambo lolote. Ukitaka mwanaume akuchukie basi mkosoe. Adui mkubwa kabisa wa mwanaume ni kukosolewa, lakini sio kwamba wanawake hufurahia kukosolewa, naomba nieleweke hapa, kwa kawaida mwanamke anapokosolewa haimpi shida, kama ilivyo kwa mwanaume, kwani kutokana na mfumo dume, wanawake wamekuwa wakikosolewa tangu miaka milioni iliyopita na kutupiwa lawama hata kama kosa ni la mwanaume.
Hebu soma Mwanzo 3 fungu la 11 mpaka la 13, naomba ninukuu:
Akasema ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala. Mwisho wa kunukuu.
Kwa mujibu wa maandiko Eva alidanganywa na Nyoka ale tunda la mti wa katikati naye akamdanganya Adamu ili ale lile tunda, hivi hapo kosa ni la nani? Yule aliyedanganywa au aliyedanganya? Kwa nini Adamu asikatae kula lile tunda? Si alikuwa anajua kabisa kwamba walikatazwa na Mungu kutokula hilo tunda la mti wa katikati? Kwa nini asihoji sababu ya kutakiwa kula hilo tunda na Eva? Ukichunguza sana utagundua kwamba yote hiyo ilikuwa ni kutaka sifa, alitaka awe na uwezo kama wa Mungu ili ajiridhishe, kwani alipewa kila kitu katika ile bustani ya Edeni lakini hakuridhika akautaka Umungu! Halafu leo analaumiwa mwanamke!
Mpaka hapo nadhani umeona ni kiasi gani wanawake wamekuwa wakikosolewa na kulaumiwa tangu enzi na enzi, na umeona hata Biblia imekiri hilo. Ndio maana Mwanaume akikosolewa na mwanamke huumia sana, kwa sababu ya mazoea. Humfanya mwanaume kuona kama vile amenyanganywa uanaume wake, hana thamani tena na hastahili. Kama wewe ni mwanamke ukitaka kumuathiri mwanaume kisaikolojia basi mkosoe.
Kwa kawaida kukosolewa au kukosoa siyo jambo lenye kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanaume, kwani mfumo dume yaani ego ndiyo inayotawala kichwani mwake. Tunashuhudia hata huko mashuleni tuliposoma, kama ukimzidi mwanaume kwa alama katika mitihani hasa kama anasifiwa kuwa ana akili sana, hiyo inaweza kumuathiri kisaikolojia, na anaweza kukosa raha au hata kujenga chuki.
Kwa upande wa sisi wanawake, nimejifunza jambo moja, kama umeolewa au uko kwenye uhusiano na mwanaume, basi kuwa makini sana unapomkosoa mwenzi wako. Kwani unapomkosoa mumeo au mpenzi wako mara kwa mara unaweza kumfanya kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa sababu maumivu ya kukosolewa huendelea hadi kitandani. Kwa bahati mbaya wanawake wengi hatujui na tunadhani wanaume ni kama sisi, kwa hiyo tunapowakosoa wanaume zetu tunaamini kwamba tunaweza kuwabadili kitabia kumbe ndio kwanza tunaelekeza uhusiano wetu au ndoa zetu shimoni.
Sasa umejua hilo, mpe atakacho. Msifie, mfanye ajisikie kiongozi na anaetumainiw. Hata Yesu tu akiwa duniani alikuwa anawauliza wanafunzi wake 'watu wanasema mimi ni nani?' na nyie mnasema mimi ni nani. What do you think that was? Hata Mungu anasema mimi ni Mungu mwenye wivu, usiwe na miungu mingine ila mimi.
Kazi yako ni kumwaga misifa tuuu. Baby that, honey this, sweetheart those. Hata kama unamkosoa unaanza na sifa, 'mpenzi, nashukuru sana unavyotuangalia mimi na watoto na kuhakikisha tuko vizuri saa zote. Kitu kimoja tu kinanisumbua, najua kiko ndani ya uwezo wako. . . . . '
Ni hivi bi dada, afanyayo mwanaume ambayo wewe umeitafsiri kama "ego" ni hulka ambayo tumeumbwa nayo, na ndio maana hapo awali nimekudokezea kuwa, tulipewa mamlaka ya kutawala na wala sio kutawaliwa, ushawahi jiuliza kwa nini Yesu alikuwa mwanaume na si mwanamke, vivyo hivyo kwa manabii na mitume wengi waliopita...
Sifa huambatana na yule zinayempasa kuwa nazo.
Hii mada bana! Eti kisa ego!!
Mwanamke akiwa rais taifa simu zote linakuwa weak! Na maendeleo yanakua ovyo! Mataifa yooote kama yangekuwa na marais wanawake, basi kungekuwa na mabifu kila kona! Hebu wasikilizeni wanawake wa CLOUDS FM, umbea tuuuuuuu ndo sifa kubwa ya wanawake, wanawake hawatizami mbali, wanatizama short term effects! Inshort wanawake ni wa chini ya wanaume!
Na kuhusu uyo Adam, mama, mapenzi ya adam kwa mkewe ndo yamemfanya ivo! Sisi mtume wetu ametwambia kuwa, hapa duniani anaondoka akiwa ameacha shari 3, wanawake, mali na watoto!
Mwanamke anaweza akakugombanisha na mama yako!!!
Hewala mkuu.
Lakini mbona pamoja na kupewa mamlaka hayo na Mungu, lakini pale itokeapo mwanamke akam- criticize mwanaume japo kidogo tu, yeye anaishiwa na nguvu kabisa. mimi nilitarajia atatumia maguvu hayo kujitutumua na kuonyesha kwamba hayuko hivyo kama navyofikiriwa.
Hebu chukulia mwanaume anaambiwa na mpenzi wake mara baada ya game kuwa hajaridhika kwa sababu jamaa ana kibamia na hajamfikisha kileleni,....
Unatarajia huyu mwanaume atajona vipi mbele ya wanawake na wanaume wenzie?
Kwa mwanamke is not a big deal kukosolewa, inaweza kumuuma lakini sio kwa kiwango kama cha mwanaume, kumbuka huyu mwanaume ndiye aliyepewa mamlaka na Mungu! halafu akosolewe na kiumbe alichoambiwa kwamba yeye ndiye kichwa cha hicho kiumbe!
Je, una maoni gani juu ya hilo mkuu?
Mnataka mpaa mdanganywe ndo mnaona raha sio, hamtaki wanaume wanao sema ukweli :biggrin1:Umeshindwa kuificha hiyo ego hata kwa leo tu?
nakubaliana na wewe kuhusu kufukuzia mabinti, lakini wengine hata hazisimami au huishia kumaliza haraka hivyo ili kuficha udhaifu wao huishia kuhonga hela nyingi kutunyamazisha tusitoe siri zenu nje.
Unadhani hawa wanaotangaza kuuza dawa feki za nguvu za kiume wanazuka hivi hivi, wanajua soko lipo kwa sababu wanaume wengi ni dhaifu,
Ukikutana nao kelele nyiiingi, kwenye game tembele!
Kwahiyo uliotumenshen ndio tuna upungufu wa nguvu za kiume?
Kwahiyo uliotumenshen ndio tuna upungufu wa nguvu za kiume?
hakyanani tutake razi!!
heri ni wewe uliyekubali kukaa kwenye nafasi yako amin amin nakwambia hutopata shida na mambo ya beijing!mi nilishajikubalia uanamke wangu na uanaume wa wanaume!wawe na ego idi in naona sawa tu!ah!inanisave vitu kibao mie!LOL!
yaani leo ndo umemwaga booooonge la point.....
Haya mukuje wanaume msome hukuuuu