Duh! Wanaume kwa kupenda sifa!

Duh! Wanaume kwa kupenda sifa!

Kuna mambo madogo madogo yanayowahusu wanaume huwa watu wengi hawayaoni na kufanya tafakuri. Katika makuzi yangu nimegundua udhaifu ambao wanaume wengi wanao lakini hausemwi kwa sababu ya mfumo dume kutawala. Nimegundua kwamba sifa ndio inayowauwa wanaume wengi, kwa kutaka kwao, kuimarisha mfumo dume walionao (ego)

Nitajaribu kueleza kidogo kuhusu maana ya hili neno ego, kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, naomba munirekebishe kama sitapatia. Kwa mujibu wa nadharia za wanasaikolojia ego ni yale tuliyofundishwa na jamii kwa ujumla, yaani yale tuliyoambiwa kwamba ni mabaya au mazuri kwa mujibu wa jamii. Kwa mfano wanaume wamefundishwa kwamba wao ni kichwa cha nyumba, wao ndio wenye maamuzi sahihi, hawakosei, wana akili kuliko wanawake, wana mamlaka juu ya wanawake, wao ndio wanaotakiwa kuchumbia kulipa mahari na kuoa, na mambo mengine mengi tu unayoyafahamu.

Kwa hiyo ndio sababu utakuta wanaume wanapenda sana sifa, wanataka wanawake wawaone kwamba wao ndio bora kabisa na wasioshindwa na jambo lolote. Ukitaka mwanaume akuchukie basi mkosoe. Adui mkubwa kabisa wa mwanaume ni kukosolewa, lakini sio kwamba wanawake hufurahia kukosolewa, naomba nieleweke hapa, kwa kawaida mwanamke anapokosolewa haimpi shida, kama ilivyo kwa mwanaume, kwani kutokana na mfumo dume, wanawake wamekuwa wakikosolewa tangu miaka milioni iliyopita na kutupiwa lawama hata kama kosa ni la mwanaume.

Hebu soma Mwanzo 3 fungu la 11 mpaka la 13, naomba ninukuu:

“Akasema ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala”. Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa maandiko Eva alidanganywa na Nyoka ale tunda la mti wa katikati naye akamdanganya Adamu ili ale lile tunda, hivi hapo kosa ni la nani? Yule aliyedanganywa au aliyedanganya? Kwa nini Adamu asikatae kula lile tunda? Si alikuwa anajua kabisa kwamba walikatazwa na Mungu kutokula hilo tunda la mti wa katikati? Kwa nini asihoji sababu ya kutakiwa kula hilo tunda na Eva? Ukichunguza sana utagundua kwamba yote hiyo ilikuwa ni kutaka sifa, alitaka awe na uwezo kama wa Mungu ili ajiridhishe, kwani alipewa kila kitu katika ile bustani ya Edeni lakini hakuridhika akautaka Umungu! Halafu leo analaumiwa mwanamke!

Mpaka hapo nadhani umeona ni kiasi gani wanawake wamekuwa wakikosolewa na kulaumiwa tangu enzi na enzi, na umeona hata Biblia imekiri hilo. Ndio maana Mwanaume akikosolewa na mwanamke huumia sana, kwa sababu ya mazoea. Humfanya mwanaume kuona kama vile amenyang’anywa uanaume wake, hana thamani tena na hastahili. Kama wewe ni mwanamke ukitaka kumuathiri mwanaume kisaikolojia basi mkosoe.

Kwa kawaida kukosolewa au kukosoa siyo jambo lenye kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanaume, kwani mfumo dume yaani ego ndiyo inayotawala kichwani mwake. Tunashuhudia hata huko mashuleni tuliposoma, kama ukimzidi mwanaume kwa alama katika mitihani hasa kama anasifiwa kuwa ana akili sana, hiyo inaweza kumuathiri kisaikolojia, na anaweza kukosa raha au hata kujenga chuki.

Kwa upande wa sisi wanawake, nimejifunza jambo moja, kama umeolewa au uko kwenye uhusiano na mwanaume, basi kuwa makini sana unapomkosoa mwenzi wako. Kwani unapomkosoa mumeo au mpenzi wako mara kwa mara unaweza kumfanya kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa sababu maumivu ya kukosolewa huendelea hadi kitandani. Kwa bahati mbaya wanawake wengi hatujui na tunadhani wanaume ni kama sisi, kwa hiyo tunapowakosoa wanaume zetu tunaamini kwamba tunaweza kuwabadili kitabia kumbe ndio kwanza tunaelekeza uhusiano wetu au ndoa zetu shimoni.

Just nature.... Hata jogoo yuko ivo...
 
we ni jinsia gani?...wanipa wasiwasi

hahaha wewe usiwe na worries bana.... ukweli ndio huo bwana wanaume full egos tuu hamna lolote. ata tukiwa tunagegeda mademu twapenda kusikia wakilia na kuguna ili tupate ego boost kuwa am nailing ittttt!!!!!
 
wanawake ni jeshi kubwa ila hawana akiri ya kujitambua na kufanya maamuzi so lazina awepo kamanda (mwanaume) wa kuwafanyia maanuzi, we huoni mwanamke anaweza kufukuzwa hata na ngedere nyani ndo usisema mavi na mikojo kwenye chupi
 
Kuna mambo madogo madogo yanayowahusu wanaume huwa watu wengi hawayaoni na kufanya tafakuri. Katika makuzi yangu nimegundua udhaifu ambao wanaume wengi wanao lakini hausemwi kwa sababu ya mfumo dume kutawala. Nimegundua kwamba sifa ndio inayowauwa wanaume wengi, kwa kutaka kwao, kuimarisha mfumo dume walionao (ego)

Nitajaribu kueleza kidogo kuhusu maana ya hili neno ego, kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, naomba munirekebishe kama sitapatia. Kwa mujibu wa nadharia za wanasaikolojia ego ni yale tuliyofundishwa na jamii kwa ujumla, yaani yale tuliyoambiwa kwamba ni mabaya au mazuri kwa mujibu wa jamii. Kwa mfano wanaume wamefundishwa kwamba wao ni kichwa cha nyumba, wao ndio wenye maamuzi sahihi, hawakosei, wana akili kuliko wanawake, wana mamlaka juu ya wanawake, wao ndio wanaotakiwa kuchumbia kulipa mahari na kuoa, na mambo mengine mengi tu unayoyafahamu.

Kwa hiyo ndio sababu utakuta wanaume wanapenda sana sifa, wanataka wanawake wawaone kwamba wao ndio bora kabisa na wasioshindwa na jambo lolote. Ukitaka mwanaume akuchukie basi mkosoe. Adui mkubwa kabisa wa mwanaume ni kukosolewa, lakini sio kwamba wanawake hufurahia kukosolewa, naomba nieleweke hapa, kwa kawaida mwanamke anapokosolewa haimpi shida, kama ilivyo kwa mwanaume, kwani kutokana na mfumo dume, wanawake wamekuwa wakikosolewa tangu miaka milioni iliyopita na kutupiwa lawama hata kama kosa ni la mwanaume.

Hebu soma Mwanzo 3 fungu la 11 mpaka la 13, naomba ninukuu:

"Akasema ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala". Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa maandiko Eva alidanganywa na Nyoka ale tunda la mti wa katikati naye akamdanganya Adamu ili ale lile tunda, hivi hapo kosa ni la nani? Yule aliyedanganywa au aliyedanganya? Kwa nini Adamu asikatae kula lile tunda? Si alikuwa anajua kabisa kwamba walikatazwa na Mungu kutokula hilo tunda la mti wa katikati? Kwa nini asihoji sababu ya kutakiwa kula hilo tunda na Eva? Ukichunguza sana utagundua kwamba yote hiyo ilikuwa ni kutaka sifa, alitaka awe na uwezo kama wa Mungu ili ajiridhishe, kwani alipewa kila kitu katika ile bustani ya Edeni lakini hakuridhika akautaka Umungu! Halafu leo analaumiwa mwanamke!

Mpaka hapo nadhani umeona ni kiasi gani wanawake wamekuwa wakikosolewa na kulaumiwa tangu enzi na enzi, na umeona hata Biblia imekiri hilo. Ndio maana Mwanaume akikosolewa na mwanamke huumia sana, kwa sababu ya mazoea. Humfanya mwanaume kuona kama vile amenyang'anywa uanaume wake, hana thamani tena na hastahili. Kama wewe ni mwanamke ukitaka kumuathiri mwanaume kisaikolojia basi mkosoe.

Kwa kawaida kukosolewa au kukosoa siyo jambo lenye kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanaume, kwani mfumo dume yaani ego ndiyo inayotawala kichwani mwake. Tunashuhudia hata huko mashuleni tuliposoma, kama ukimzidi mwanaume kwa alama katika mitihani hasa kama anasifiwa kuwa ana akili sana, hiyo inaweza kumuathiri kisaikolojia, na anaweza kukosa raha au hata kujenga chuki.

Kwa upande wa sisi wanawake, nimejifunza jambo moja, kama umeolewa au uko kwenye uhusiano na mwanaume, basi kuwa makini sana unapomkosoa mwenzi wako. Kwani unapomkosoa mumeo au mpenzi wako mara kwa mara unaweza kumfanya kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa sababu maumivu ya kukosolewa huendelea hadi kitandani. Kwa bahati mbaya wanawake wengi hatujui na tunadhani wanaume ni kama sisi, kwa hiyo tunapowakosoa wanaume zetu tunaamini kwamba tunaweza kuwabadili kitabia kumbe ndio kwanza tunaelekeza uhusiano wetu au ndoa zetu shimoni.

sio sisi ni testosterone tu,,,
 
Nilikuwa na majibu tofauti kabla ya kusoma paragraph ya mwisho ila nitayaweka pia (chonde chonde haya yaishie huku JF kwani ukiyaingiza ktk nadharia ya maisha yatakusumbua). Mtazamo wa kawaida pamoja na yote uliyosema bado ukweli haupingika nature ya wanaume woote ni kuona uzaidi na wanawamke ndio maana mwanamke mwenye elimu/tajiri hawezi kuolewa na mwanamme asiye na elimu/masikini ila tofauti yake ndio mpango mzima...Mungu hakukusudia mwanamke waonekane watumwa aliposema Msaidizi aliyetoka ubavuni mwa mwanamme ila ambacho wanaume wengi hatukijui ni tafsiri ya MSAIDIZI tena sehemu katika mwili wetu..Sehemu ya mwili wa binadamu inapopata hitilafu ni wazi kwamba mwili mzima unapata maumivu sasa basi mwanamke kuwa sehemu ya mwanamme ni yule yule ktk namna tofauti. Ndio maana wanawake ndio washauri wetu wazuri na hata ikadhihirika kwamba kila familia yenye maendeleo ni taa ya kuonyesha kuna mke bora ndani...Ni hayo tu wapendwa.
 
Back
Top Bottom