• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

Duh! Wanaume kwa kupenda sifa!

vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
245
Points
195
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
245 195
Kuna mambo madogo madogo yanayowahusu wanaume huwa watu wengi hawayaoni na kufanya tafakuri. Katika makuzi yangu nimegundua udhaifu ambao wanaume wengi wanao lakini hausemwi kwa sababu ya mfumo dume kutawala. Nimegundua kwamba sifa ndio inayowauwa wanaume wengi, kwa kutaka kwao, kuimarisha mfumo dume walionao (ego)

Nitajaribu kueleza kidogo kuhusu maana ya hili neno ego, kwa tafsiri yangu isiyo rasmi, naomba munirekebishe kama sitapatia. Kwa mujibu wa nadharia za wanasaikolojia ego ni yale tuliyofundishwa na jamii kwa ujumla, yaani yale tuliyoambiwa kwamba ni mabaya au mazuri kwa mujibu wa jamii. Kwa mfano wanaume wamefundishwa kwamba wao ni kichwa cha nyumba, wao ndio wenye maamuzi sahihi, hawakosei, wana akili kuliko wanawake, wana mamlaka juu ya wanawake, wao ndio wanaotakiwa kuchumbia kulipa mahari na kuoa, na mambo mengine mengi tu unayoyafahamu.

Kwa hiyo ndio sababu utakuta wanaume wanapenda sana sifa, wanataka wanawake wawaone kwamba wao ndio bora kabisa na wasioshindwa na jambo lolote. Ukitaka mwanaume akuchukie basi mkosoe. Adui mkubwa kabisa wa mwanaume ni kukosolewa, lakini sio kwamba wanawake hufurahia kukosolewa, naomba nieleweke hapa, kwa kawaida mwanamke anapokosolewa haimpi shida, kama ilivyo kwa mwanaume, kwani kutokana na mfumo dume, wanawake wamekuwa wakikosolewa tangu miaka milioni iliyopita na kutupiwa lawama hata kama kosa ni la mwanaume.

Hebu soma Mwanzo 3 fungu la 11 mpaka la 13, naomba ninukuu:

"Akasema ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. Bwana Mungu akamwambia mwanamke, Nini hili ulilolifanya? Mwanamke akasema, Nyoka alinidanganya nikala". Mwisho wa kunukuu.

Kwa mujibu wa maandiko Eva alidanganywa na Nyoka ale tunda la mti wa katikati naye akamdanganya Adamu ili ale lile tunda, hivi hapo kosa ni la nani? Yule aliyedanganywa au aliyedanganya? Kwa nini Adamu asikatae kula lile tunda? Si alikuwa anajua kabisa kwamba walikatazwa na Mungu kutokula hilo tunda la mti wa katikati? Kwa nini asihoji sababu ya kutakiwa kula hilo tunda na Eva? Ukichunguza sana utagundua kwamba yote hiyo ilikuwa ni kutaka sifa, alitaka awe na uwezo kama wa Mungu ili ajiridhishe, kwani alipewa kila kitu katika ile bustani ya Edeni lakini hakuridhika akautaka Umungu! Halafu leo analaumiwa mwanamke!

Mpaka hapo nadhani umeona ni kiasi gani wanawake wamekuwa wakikosolewa na kulaumiwa tangu enzi na enzi, na umeona hata Biblia imekiri hilo. Ndio maana Mwanaume akikosolewa na mwanamke huumia sana, kwa sababu ya mazoea. Humfanya mwanaume kuona kama vile amenyang'anywa uanaume wake, hana thamani tena na hastahili. Kama wewe ni mwanamke ukitaka kumuathiri mwanaume kisaikolojia basi mkosoe.

Kwa kawaida kukosolewa au kukosoa siyo jambo lenye kuweza kumpa mtu jazba. Lakini hivi sivyo ilivyo kwa mwanaume, kwani mfumo dume yaani ego ndiyo inayotawala kichwani mwake. Tunashuhudia hata huko mashuleni tuliposoma, kama ukimzidi mwanaume kwa alama katika mitihani hasa kama anasifiwa kuwa ana akili sana, hiyo inaweza kumuathiri kisaikolojia, na anaweza kukosa raha au hata kujenga chuki.

Kwa upande wa sisi wanawake, nimejifunza jambo moja, kama umeolewa au uko kwenye uhusiano na mwanaume, basi kuwa makini sana unapomkosoa mwenzi wako. Kwani unapomkosoa mumeo au mpenzi wako mara kwa mara unaweza kumfanya kukosa nguvu za kushiriki tendo la ndoa kwa sababu maumivu ya kukosolewa huendelea hadi kitandani. Kwa bahati mbaya wanawake wengi hatujui na tunadhani wanaume ni kama sisi, kwa hiyo tunapowakosoa wanaume zetu tunaamini kwamba tunaweza kuwabadili kitabia kumbe ndio kwanza tunaelekeza uhusiano wetu au ndoa zetu shimoni.
 
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
15,975
Points
2,000
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
15,975 2,000
mama yangu ngoja waje hapa!
 
M

mzabzab

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2011
Messages
8,820
Points
2,000
M

mzabzab

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2011
8,820 2,000
unastahili pongezi!!! kweli kabisa wanaume sie ni ego tuu...wee tuachie sie ego zedtu wala hutapata shida....ata hii mambo ya kugegeda wanawake wengi ni ego tuu ya kuonyesha u hot power over women...kwamba unaweza wafanya wakuvulie chupi hahaha......sex is a power thing...nothing else!!!
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
53,060
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
53,060 2,000
We mwanadamu umetumwa na nani kuja kufanya ufukunyuzi?
 
fazaa

fazaa

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2009
Messages
2,985
Points
0
fazaa

fazaa

JF-Expert Member
Joined May 20, 2009
2,985 0
We wacha kukuleta maneno mengi tumeisha wazowea wanawake, FYI men are more powerful na wana better judgment, and can handle themselves better in tough situation kwa hio wana haki ya kujisifia :biggrin1:
 
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
53,060
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
53,060 2,000
Last edited by a moderator:
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
15,975
Points
2,000
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
15,975 2,000
We mwanadamu umetumwa na nani kuja kufanya ufukunyuzi?
kisu kimegonga mfupa enh! vukani go girl!
mi nakulinda hapa!
 
Last edited by a moderator:
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
245
Points
195
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
245 195
unastahili pongezi!!! kweli kabisa wanaume sie ni ego tuu...wee tuachie sie ego zedtu wala hutapata shida....ata hii mambo ya kugegeda wanawake wengi ni ego tuu ya kuonyesha u hot power over women...kwamba unaweza wafanya wakuvulie chupi hahaha......sex is a power thing...nothing else!!!
nakubaliana na wewe kuhusu kufukuzia mabinti, lakini wengine hata hazisimami au huishia kumaliza haraka hivyo ili kuficha udhaifu wao huishia kuhonga hela nyingi kutunyamazisha tusitoe siri zenu nje.

Unadhani hawa wanaotangaza kuuza dawa feki za nguvu za kiume wanazuka hivi hivi, wanajua soko lipo kwa sababu wanaume wengi ni dhaifu,

Ukikutana nao kelele nyiiingi, kwenye game tembele!
 
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
15,975
Points
2,000
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
15,975 2,000
tukutishe kwani siye vinyago vya mpapure au siye twang'ata?
hahahahahhahahhah jibu hoja au ndo ego zenyewe hizo!
ahahhahahahahhaa pana chezeya makitu ya men's pride hivi hata kugegeda vishi=tobe wengi ni mradi tu mjisikie raha ya kiume!ahahahhaahha leo mtajibeba hapa na vukani alijua mtabisha mmewekewaje vifunguu nani anaweza kubishana na vifungu jumapili yote hii!
NAPENDAGA KWELI MIMI MKIBANANISHWA NAMNA HII!
 
Last edited by a moderator:
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
245
Points
195
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
245 195
kisu kimegonga mfupa enh! vukani go girl!
mi nakulinda hapa!
hawaliwezi hili Jaramba, acha waje hata milioni, nawachora tu nikisoma tambo zao humu JF nikiwa kama guest, mara nyingi naishia kucheka tu
 
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
15,975
Points
2,000
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
15,975 2,000
nakubaliana na wewe kuhusu kufukuzia mabinti, lakini wengine hata hazisimami au huishia kumaliza haraka hivyo ili kuficha udhaifu wao huishia kuhonga hela nyingi kutunyamazisha tusitoe siri zenu nje.

Unadhani hawa wanaotangaza kuuza dawa feki za nguvu za kiume wanazuka hivi hivi, wanajua soko lipo kwa sababu wanaume wengi ni dhaifu,

Ukikutana nao kelele nyiiingi, kwenye game tembele!
AHAHAHAHAHHAHHAHAHHAHHAAHHAHHAHA vukaniiiiiiiiiiiiiiiiiii duh tembele?ahahhahahahha usinikumbushe uuuwih mtani leo ndyo leo wapi Asprin, HorsePower The Boss Dark City BAK platozoom Kaizer Erickb52 mkiva Mtambuzi St. Paka Mweusi Boflo
na wengine wooote wa mrengo wa kulia
MUKUJE HUKU!
 
Last edited by a moderator:
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Messages
53,060
Points
2,000
Watu8

Watu8

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2010
53,060 2,000
hahahahahhahahhah jibu hoja au ndo ego zenyewe hizo!
ahahhahahahahhaa pana chezeya makitu ya men's pride hivi hata kugegeda vishi=tobe wengi ni mradi tu mjisikie raha ya kiume!ahahahhaahha leo mtajibeba hapa na vukani alijua mtabisha mmewekewaje vifunguu nani anaweza kubishana na vifungu jumapili yote hii!
NAPENDAGA KWELI MIMI MKIBANANISHWA NAMNA HII!
unajua mpaka sasa sijamwelewa anataka nini, kakasirishwa na yeye kuwa mwanamke au hataki kuwa mwanamke!!!
 
Last edited by a moderator:
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,232
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,232 2,000
unastahili pongezi!!! kweli kabisa wanaume sie ni ego tuu...wee tuachie sie ego zedtu wala hutapata shida....ata hii mambo ya kugegeda wanawake wengi ni ego tuu ya kuonyesha u hot power over women...kwamba unaweza wafanya wakuvulie chupi hahaha......sex is a power thing...nothing else!!!
yaani leo ndo umemwaga booooonge la point.....

Haya mukuje wanaume msome hukuuuu
 
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
245
Points
195
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
245 195
We wacha kukuleta maneno mengi tumeisha wazowea wanawake, FYI men are more powerful na wana better judgment, and can handle themselves better in tough situation kwa hio wana haki ya kujisifia :biggrin1:
Naamini wewe ushawahi kungalia Movies za kipelelezi au kijasusi..
Hivi ushaona mwanaume kubwa la maadui akipindua kwa kachero mwanamke?

Huyo Samson na miguvu yake alishia wapi,
Delilah alimaliza mchezo just like eating piece of delicious cake
 
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Messages
15,975
Points
2,000
snowhite

snowhite

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2012
15,975 2,000
hawaliwezi hili Jaramba, acha waje hata milioni, nawachora tu nikisoma tambo zao humu JF nikiwa kama guest, mara nyingi naishia kucheka tu
ahahahhahaha mi mbona nilishasema mwanzo kabisa kuwa nakuaminia!GO GIRL!
mi washaniteka kwenye ego yao nawakubaliaga tu kila kitu sa nikikutana na fellow anawaput in a corner like this weeeh!naonaje raha!
 
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2009
Messages
245
Points
195
vukani

vukani

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2009
245 195
yaani leo ndo umemwaga booooonge la point.....

Haya mukuje wanaume msome hukuuuu
Nilikuwa nawangalia wanavyochonga hapa.
Kila siku wanawake wamefanya hivi, wanawake wamefanya vile mweh!
 
Forum statistics

Threads 1,403,288
Members 531,177
Posts 34,419,801
Top