6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 3,670
- 8,023
Niaje waungwana
Nafikiri mashambulizi ya mwaka jana kati ya Iran na Israel, yalimpofusha sana Netanyahu kwa kuamini kwamba Iran ilikuwa na silaha chache, na dhaifu kwa kuweza kufanya maangamizi katika ardhi ya Israel.
Ikumbukwe kwamba katika mashambulizi yale Iran alitumia makombora ya kawaida na ya masafa mafupi, hivyo hata madhara na uharibifu wake huko Israel haukuwa mkubwa kivile, hali iliyomfanya Netanyahu aamini kwamba Iran haina silaha za maana za kupambana nae, lakini pia aliamini kwamba Iron dome na Thaad zikiongezwa na kurekebishwa vizuri, basi muajemi atachapika vizuri bila kurusha au kuingiza chochote katika ardhi ya Israel.
Masikini, jamaa hakujua kwamba Ayatollah alikuwa anampimia upeo wake wa akili ulipoishia. Akaenda Marekani kuonana na Trump kisha wakapanga namna watakavyoivamia Iran, kutawala anga, na kuzuia kombora kurushwa nchini kwao Israel.
Waswahili wanasema usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Neta akaanza uvamizi kwa mashambulizi ya kushtukiza huku wakiwa wameshajipanga na Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na washirika wengine kuzuia mashambulizi ya Iran kwenda Israel. Mpaka hapo walikuwa wanajua Iran haina silaha au makombora ya maana ya kupenya ulinzi wao. Kwa bahati mbaya hali ikawa tofauti na walivyotarajia.
Vinu vikaanza kutumwa Israel katika speed na nguvu ya ajabu kiasi ya kwamba Iro dome na Thaad zao zikabaki kama maonesho tu au mavyuma ya kukamatia kumbi kumbi. Iron dome balada ya kuzuia kombora, inazuia nzi na upepo.
Netanyahu akaona maji yamezidi unga, kinachozuiwa hakionekani, akamwambia baba yake Trump aingilie kati. Baba na yeye kuingilia kati kaishia kupiga hewa, huku mzigo ukiwa umeshahamishwa zamani. Baada ya hapo wakafikiri hilo tukio linamfanya muajemi aogope au kusalimu amri, badala yake ikawa kama vile wamempeleka mzaramo mkoleni. Yani ndo amezidisha mashambulizi na kuigeza Tel Aviv kama Mogadishu.
Baada ya plan kushindwa eti wameamua kuomba poo kwa kutaka vita isimame. Muajemi hataki kusikia hilo, bado anaendeleza kipondo tu huko Israel. Japo wao ni mabingwa wa kuficha taarifa, lakini ukiona Trump anakimbilia kutaka mapigano yasitishwe au vita iishe basi ujue ameona madhara makubwa mno yaliofanywa na Iran huko Israel. Maana ni yeye ndio alikuwa anasema eti waachwe waendelee kuchapana. Sasa imekuaje tena kutaka vita isimame. Za kuambiwa changanya na zako.
Vita sio poa. Nina imani Netanyahu anajuta kuanzisha huu mzozo na vita ikisimama naamini hatokuja tena kuigusa Iran kindezi ndezi vile.
Ukiona mtu mzima analia ujue kuna jambo. Fikiria leo hii Trump anapambana ili vita iishe. Ujue kuna jambo kubwa limetokea huko Israel halitakiwi kusemwa 🤣🤣🤣