MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 31,663
- 48,440
Baada ya mzungu kuchora mpaka wake katikati ya jamii ya Wamaasai na kusema wa huku waitwe Wakenya na walio upande wa pili waitwe Watanzania, ndugu kwenye hii jamii hawajawahi kubaguana, na hushirikiana sana kwenye baadhi ya mambo, maana hapo mpakani utakuta kunao watu wa koo moja, hata babu wao mmoja, ila mpaka wa mzungu umesababisha akitaka kwenda kumsabahi mjomba lazima avuke kwenda upande wa pili.
Huwa ni kawaida sana kuwakuta Wamaasai wa pande zote mbili wamekaa vikao vya kijamii wakishirikiana hata kwenye hafla yoyote ikiwemo harusi hata kwenye misiba.
Juzi akina mama wa hii jamii waliotokea upande wa Kenya walikamatwa na kutozwa faini ya mamilioni upande wa Tanzania, nimeshangaa sana maana nilijua ni akina sisi wa Nairobi waliosafiri na kuingia nchi ya watu kufanya biashara.
Hapo sasa nawaza mkao wa hiyo jamii mpakani, namna wataanza kutazamana, unakuta mtu mnaongea lugha moja, mila moja, hata mashuka mliovaa yanafanana labda hata tohara mumefanyiwa pamoja mlikwenda jando moja na mlichangia hadi ngariba mmoja ila kuanzia hapo ni mwendo wa kubaguana....mzungu balaa kweli katuachia hili na tukalipokea kichwa kichwa.
============================
Kenyan women who were jailed in Tanzania in March 2021
DAILY NATION
Kajiado Governor Joseph Ole Lenku hired a chopper and flew to the border town of Ilasit, Kajiado where he secured the release of 26 women who were jailed in Tanzania.
The Kenyan nationals were accused of illegally entering the neighbouring country without passports or other relevant documents. They were sentenced to 1 year jail term or a fine of Ksh23,600 (TSh 500,000) each.
Ole Lenku paid a total of Ksh1 million and secured their release, four days after they were sentenced.