Duh! Kumbe Wakenya waliokamatwa upande wa Tanzania walikuwa wanawake wa jamii ya Kimaasai, ndio washachonganishwa hivi hivi

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
31,523
47,762
Baada ya mzungu kuchora mpaka wake katikati ya jamii ya Wamaasai na kusema wa huku waitwe Wakenya na walio upande wa pili waitwe Watanzania, ndugu kwenye hii jamii hawajawahi kubaguana, na hushirikiana sana kwenye baadhi ya mambo, maana hapo mpakani utakuta kunao watu wa koo moja, hata babu wao mmoja, ila mpaka wa mzungu umesababisha akitaka kwenda kumsabahi mjomba lazima avuke kwenda upande wa pili.

Huwa ni kawaida sana kuwakuta Wamaasai wa pande zote mbili wamekaa vikao vya kijamii wakishirikiana hata kwenye hafla yoyote ikiwemo harusi hata kwenye misiba.

Juzi akina mama wa hii jamii waliotokea upande wa Kenya walikamatwa na kutozwa faini ya mamilioni upande wa Tanzania, nimeshangaa sana maana nilijua ni akina sisi wa Nairobi waliosafiri na kuingia nchi ya watu kufanya biashara.

Hapo sasa nawaza mkao wa hiyo jamii mpakani, namna wataanza kutazamana, unakuta mtu mnaongea lugha moja, mila moja, hata mashuka mliovaa yanafanana labda hata tohara mumefanyiwa pamoja mlikwenda jando moja na mlichangia hadi ngariba mmoja ila kuanzia hapo ni mwendo wa kubaguana....mzungu balaa kweli katuachia hili na tukalipokea kichwa kichwa.

============================

d

Kenyan women who were jailed in Tanzania in March 2021

DAILY NATION
Kajiado Governor Joseph Ole Lenku hired a chopper and flew to the border town of Ilasit, Kajiado where he secured the release of 26 women who were jailed in Tanzania.

The Kenyan nationals were accused of illegally entering the neighbouring country without passports or other relevant documents. They were sentenced to 1 year jail term or a fine of Ksh23,600 (TSh 500,000) each.

Ole Lenku paid a total of Ksh1 million and secured their release, four days after they were sentenced.
 
Hapo tanzania kweli hatukuwafanyia ubinadam
Hao wakina mama ....

Ova
 
Serikali yetu ya Tanzania inatafuta choko choko za kipumbavu sana na mataifa ya jirani na nje. Kuna baadhi ya makosa yanahitaji onyo tu, sio lazima kila kitu kufanya komoa komoa.
 
Kwa hiyo Mmasai hawezi kuwa mhamiaji haramu!!!?

Tatizo la kuishi Buza siku zote hautoki kuna mambo haitokuja hata siku moja uyaelewe, tafuta Mtanzania anayetokea kwa jamii za mipakani kama vile Wanyasa, Wahaya, Wanyambo, Wamaasai, Wadigo n.k. akuambie namna wao huhusiana hayo maeneo. Ingekua mumekamata Mkenya aliyetokea huku kati, huyo fanyeni yenu, lakini hao akina mama mara nyingi utakuta wanakutana na kushirikiana kwenye mambo kama vicoba na mchana kila mmoja anarudi upande wake wa mpakani, sasa mkianza kuwavizia kihivyo kisa mihemko.
 
bora wameokolewa maana Tanzania yenyewe ni jela tosha, halafu kisha eti mtu akuweke kizimbani ni kama umetupwa kwenye moto wa jehanam,,, unateketea lakini hufi

asante sana Mheshimiwa Ole Lenku for coming through. niko sure hata hao mapolisi hawakua wamewai kuona chopper.... umewashangaza sana
 
Unazingua eroo, wa-Arusha wamejaa Nairobi mitaa ya Kamukunji, kwa wingi. Tena wanaishi kitamaduni kabisa mjini na zile shuka zao za purple na hata vitambulisho vya nchi yao hawana. Acheni kukuza chuki za kipumbavu, hampo special kama mnavidhania. Toning'o roi?
Juzi kati bodaboda kutoka Tanzania walipokamatwa hapo kenya sikuona ukitokwa mapovu namna hii.
Ooh kumbe mkuki mtamu kwa nguruwe ila kwa binadamu mchungu!

Sheria ifuate mkondo wake.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom