Duh, ingekua vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duh, ingekua vipi?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by TheChoji, Feb 2, 2012.

 1. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Unasikiliza dondoo za magazeti asubuhi unakutana na habari kama hizi..

  - Serikali ya Tanzania imetangaza msaada wa paundi milioni hamsini kusaidia wahanga wa mafuriko huko Brazil.
  - Kampuni ya kutengeneza magari ya kiTanzania aina ya Nyumbu, imetangaza kuyarudisha magari ya kifahari Nyumbu NY44 na NY54 zaidi ya 400,000 yaliyouzwa nchi za Asia na Australia kwani yamegundulika kuwa na hitilafu kwenye mfumo wa gia boksi ili yakafanyiwe matengenezo kwenye plant ya Mvomero. Magari mengine NY45 na NY60 zaidi ya 200,000 yaliyorudishwa kutoka USA na Japan yameshafanyiwa marekebisho.
  - Shirika la ndege la Air Tanzania limeanzisha safari za kwenda Uingereza, Canada, Japan, USA na nchi nyingine 20 kwa kutumia ndege zake mpya 40 aina ya Airbus A380. Hali hii imesemekana kutishia uhai wa shirika la Emirates
  - Timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars imefanikiwa kuingia robo fainali ya kombe la dunia baada ya kuifunga Argentina mabao 3-1, mechi hiyo ilifanyika kwenye uwanja wa kimataifa wa Ruvuma. Fainali za kombe la dunia zitafanyika jumapili ijayo kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Mechi za nusu fainali zitafanyikia viwanja vya Bagamoyo na Ifakara. Mashabiki wameombwa kuwahi kukata tiketi za treni ziendazo kasi mapema ili kuepuka usumbufu.
  - Waziri mkuu wa Israel yupo nchini kwa matibabu tangu ijumaa ya wiki iliyopita ambapo amelazwa kwenye hospitali ya kimataifa ya magonjwa ya moyo mjini Kilosa. Waziri wa mambo ya ndani alimtembelea jana kumjulia hali.
  - Dola ya marekani imezidi kuimarika dhidi ya shilingi ya kitanzania huku Paundi imeendelea kulegalega.
  - Waigizaji 25 kutoka Hollywood Marekani, wako nchini kwa ziara ya miezi miwili ili kujifunza utengenezaji filamu kutoka kwa wenzao wa Tanzania. Waigizaji hao jana walipata bahati ya kutembelea maeneo ya kimataifa ya utengenezaji filamu huko Sahare - Tanga.
  - Jeshi la Tanzania limesema litaendelea kutoa mafunzo kwa marubani wa Urusi ili kuisaidia nchi hiyo kujizatiti zaidi kivita. Waziri wa ulinzi alizungumza hayo wakati akizindua ndege mpya za kivita zilizotengenezwa na kiwanda chetu cha Biharamulo.
  - Vyuo vikuu vya Chunya na Nachingwea vimeahidi kuendelea kushirikiana katika kufanya utafiti utakaosaidia kupunguza athari zitokanazo na mionzi ya jua. Tayari vyombo vitatu vimeondoka duniani kuelekea nje ya obiti ili kukusanya taarifa muhimu. Taarifa hizo zitatumwa kwenye obsevatori ya kimataifa - Njombe.
  Mwisho wa udondozi kutoka hapa TBC. Kwa habari za lugha ya kijerumani, jiunge nasi saa nne na lugha ya kichina ni hapo saa sita. asanteni.
   
 2. Rosweeter

  Rosweeter JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 1,136
  Likes Received: 3,890
  Trophy Points: 280
  Halafu unazinduka, "Alaa, kumbe nilikuwa naota"...!
   
 3. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  dAH! LABDA MWAKA 3000..MASKINI SINTAKUWEPO!!!! ILA NINGETAMANI NIWEPO...NAKUPENDA TANZANIA!
   
 4. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Ina maana mambo hayo kwetu watz itabaki kuwa ndoto? Mi natamani sana kusikia walau mojawapo kati ya hizo..
   
 5. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  We acha tu. Kwa jinsi mambo yalivyo, naona hata mwaka 3000 ni jirani. Hivi sisi tuna nini?
   
 6. The Bleiz

  The Bleiz JF-Expert Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2012
  Messages: 3,643
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Hii kitu labda baadae sana chief..
   
 7. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Katika shughuli za mheshimiwa Rais za kuombaomba, mshauri aiombe Marekani au Urusi tubadilishane majina ya nchi mikoa na vitongoji, then utasikia hayo maneno mazuri yakitamkwa kwa majina hayo uliyoorodhesha
   
 8. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  majungu na kulalamika.
   
 9. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  ha haa. Hii kare.
   
 10. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Duh! Ingekuwa poa sana.
   
Loading...