Duh! Hii Kali !

Duh! Hii Kali !

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,685
Mwanamke Avuliwa Nguo zote Baada ya Kuingia Stand ya Mabasi Akiwa na Nguo Fupi
VIBAKA.jpg

Biashara zote zilisimama kwa muda katika stendi kuu ya mabasi ya Bomet nchini kenya wikiendi hii baada ya kundi kubwa la wanaume kumvamia mwanamke mmoja aliyekuwa amevaa kingua kifupi na kisha kumvua huku wengine wakimchezea nyeti zake.....
Mwanamke huyo ambaye inadaiwa alienda katika stendi hiyo kufanya booking ya basi,alikutwa nakisanga hicho baada ya kuvamiwa na kundi kubwa la wapiga debe na vibaka ambao walianza kwa kumzomea na kumrushia makopo ya maji......
Kwa mujibu wa shuhuda wa tukio hilo,sakata hilo lilichukua takribani dakika 15 za kumzomea na kumtukana wakiwa wamemzunguka kabla ya kumvua nguo zake.....
"Walimzomea na kumtukana vibaya huku wakiwa wamemzingira.Juhudi za wanawake wasamaria wema kumuokoa zilikwamakwa kuwa kundi lilikuwa kubwa na wao walikuwa wanaogopa kufanyiwa hivyo"...Alisema shuhuda huyo
Mbali na shuhuda huyo,Bwana Sang naye analielezea tukio hilo kwa kudai kuwa ile sketi ilikuwa ni zaidi ya fupi na pia ilikuwa nyepesi na ndani ndani hakuwa na kitu, hali iliyosababisha wapiga debe hao wamvae na kumvua.....
Bwana Sang anadai kuwa kesi nyingi za ubakaji zimekuwa zikisababishwa na wanawake wenyewe kutokana na mavazi yao wanayoyavaa....
Baada ya tukio hilo kupamba moto, polisi walifika japo walichelewa na hatimaye kufanikiwa kumwokea mrembo huo mikononi mwa vibaka hao....
Kutokana na tukio hilo,shirika la maendeleo yawanawake limelaani vibaya tukio hilo na kuahidikuchukua hatua kali zaidi endapo udhalilishaji huo utaendelea na kufumbiwa macho....

...TOA MAONI YAKO
 
Ni udhalilishaji tu. hakukua na njia nyingine ya kumkanya huyo dada asirudie kuvaa uchi zaidi ya kumvua nguo?
 
Ni udhalilishaji tu.
hakukua na njia nyingine ya kumkanya huyo dada asirudie kuvaa uchi zaidi
ya kumvua nguo?

Ujinga mtupu, watu wengine wanahalalisha tabia zao za kipuuzi kwa kisingizio cha makosa ya wengine. Huyo mwanamke kuvaa nusu uchi hakuhalalishi kudhalilishwa hivyo.
 
Wakati mwingine unaweza kupata baridi kwenye joto kali
'
Hivyo ndivyo ilivyo!
 
Bangi zao ziliwatuma wafanye hivyo huu si ubinadamu hata kidogo adhabu ya kumtupia maneno ilitosha kabisa kumfanya abadilike sema tu walikuwa na hamu ya kumchungulia mama wa watu wapuuzi hao na polisi wakiwaachia wajue ipo siku watawafanyia hivyo mama zao.
 
Hakuna mtu mwenye mamlaka ya kumfundisha mtu nzima namna ya kuvaa. kama hakuna sheria ya nchi kuhusu mavazi basi hakuna mtu yeyote mwenye mamlaka ya kufanya walivyofavya.

Hata kama kungekuwepo sheria kuhusu hilo lakini bado ni mahakama tu ndio ina wajibu wa kumadhibu mtu kwa mujibu wa sheria na si kila mtu kujiamulia anavyofikiri au alivyofundishwa kwao au kwenye dini yake.

Katika nchi inayoongozwa kisheria na yenye mchanganyiko wa makabila, imani za kidini na kijamii tofauti sii vizuri ukataka kila mtu aamini kama unavyoamini wewe. kama unaona anakukera sii lazima kumwangalia waweza kumpotezea kwani wakati wewe unachukia wapo wengine kwa kumwona tuu wanafurahi na kuongeza siku zao za kuishi.

Kati ya hao waliofanya hivyo wengine ni watenda dhambi wakubwa. Hiyo ni trespass to person na kitendo hicho ni gross indecent assault wahusika wachukuliwe hatua za kisheria ili kuzuia udhalilishaji wa namnas hiyo usijitokeze tena
 
Bangi zao ziliwatuma wafanye hivyo huu si ubinadamu hata kidogo adhabu ya kumtupia maneno ilitosha kabisa kumfanya abadilike sema tu walikuwa na hamu ya kumchungulia mama wa watu wapuuzi hao na polisi wakiwaachia wajue ipo siku watawafanyia hivyo mama zao.

Sasa bangi hapo ni zipi, Alievaa kihovyo na kushindwa kuuheshimu mwili wake na mumewe/mpenzie mwenye haki ya kuziona sehemu nyeti za mwili wake au hao waliotumia njia isiyofaa kumsahihisha?
 
By the way? Nadhani na wale wa mitepesho waanziwe,tuone jinsi boxer zao zilivyo safi "pull up your pants, no body want to see your underwear"
 
Hao majamaa bangi kweli!!! Kama alivyovaa kimin walihisi wanashawishika, ikawaje baada ya kumvua hizo nguo!!!!!??
 
Jamani jamani huwezi kucheka wala kununa pengine labda umpe poleeeeeeeeeee
 
Hahahaa Mm Nge Kuwa Karibu Ningemfunga Na Kamba Kabsaaa Maana Alikuwa Anatanga Biashara ya Mwili huyo si buree..
 
mi kua mkosaji haihalalishi wewe kufanya kosa ili kunifundisha, ujinga mtupu
 
Ni udhalilishaji tu. hakukua na njia nyingine ya kumkanya huyo dada asirudie kuvaa uchi zaidi ya kumvua nguo?

Pamoja ni kuwa ni udhalilishwaji lakini inawezekana ikawa dawa. Unadhani atarudia tena??? hawezi na wengine watajifunza kutoka kwake! Kazi kwao watembea uchiiiiii
 
Back
Top Bottom