Duh! Hawa Wakango wa Shinyanga sio poa

Duh! Hawa Wakango wa Shinyanga sio poa

Ngareroo

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2019
Posts
2,167
Reaction score
2,612
Habari zenu wadau wa jukwaa hili,poleni sana na Covid19(Corona),,Bhana Leo nitatumia Lugha ya Taifa na sio Ngareroo Slangs ili watu wote waelewe coz niliyoyakuta huku ni Nouma.

Tangia tarehe 19 mwezi huu wa3 nipo Shinyanga aka Shytown Sehemu moja panaitwa Kitangili,Kikubwa kilichonileta huku nimekuja kumsalimia Mama angu baada ya vyuo kufungwa kwa siku30,,Pia to be honest Arusha nimekimbia Corona washikaji zangu sio poa,nikaona bora nikae huku kwa Wasukuma coz sijaskia kisa chochote cha mgonjwa wa Corona.

Sasa kama Heading inavosema,juzi kuna Chaliangu tunasoma nae chuo kimoja ila yeye huku anaishi Ndala,around saa6 hivi alikuja home na Gari la binua mchanga(Tipa)kule nyuma kajaza machalii wahuni wanapiga kelele kinyama,,nikamuuliza hiki ni nini?akanambia wanaenda kula nyama msibani sehemu moja hivi panaitwa Ndala Msufini,so ni'join na wajuba tuzuke eneoni duuh!!nyama izo vipi tena msibani na makelele ya kuzidi yote haya??Nikasema anyways nikamuaga mama nikapanda...

Kwanza njiani ni full mahoni na makelele,ile tumefika dereva hata hajasimamisha tipa lake tushuke akabinua bodi la nyuma yaani atumwage kama mchanga sijui kokoto vile!!,,Lakini hakuna aliemwagwa coz wote tuliruka so akamwaga kandambili2 ila wahuni wote tupo chini muda2,nikasema Kweli hii Shytown...

Nilipoulizia nani kaamua kufariki nkaambiwa ni mtu aliezaliwa baada ya mapacha wao(Wasukuma)humuita Shija sijui Kashinje??...

Baada ya muda nikiwa nacheki warembo wa kisukuma mala nikaona watu wamevaa nguo kama waganga wa jadi hivi wanavipara alafu wanawake walikua matiti wazi daah!!niliuliza hawa ndo kina nani?nikaambiwa ni'Wakango',,walikua wakiimba nyimbo kwa Kisukuma nilikua naelewa kidogo sana nikaamua kumuomba dem flani alikua kwenye mti anitafsilie ila aliishia kucheka2 alaf akaondoka kwa aibu,nikawa na shauku ya kutaka kujua zaidi maana ya wakiimbacho, Ndipo nilipompata jamaa ndo akanifafanulia daah!!

Maneno yale ya Kisukuma waliyokua wakiimba siyakumbuki exactly ila kiswahili chake alinitafsilia kuwa kwa Kiswahili wanamaanisha"Tunaigombania Papuchi na hakuna kulala",,daah mala tena"Kina mama mfurahi maana chakula chenu ni Mikuyenge,imemulika Papuchi"Hahahaha daah ndo nikawa nawaza hawa watu(Wakango)sijui ni dini,Dhehebu au sijui ni Kabila hili! Kwanini wanafanya ivi tena msibani??Daah nilichoka,Wasukuma najua mpo humu naombeni mnisaidie katika hili, Mama angu sio msukuma Ni Muarusha ila alihamia tu huku, So sikijui Kisukuma japo najitahidi kukijua,saiv najua salamu zooote...



Aisee erooo huku siondoki niendelee ku'enjoy,Chuga ntakuja ila bado sana...


@ NgarenaroBoy.
 
Story nzuri kaka..., ila kama kweli ulikimbia Corona A - Town alafu unaenda misibani na kwenye mikusanyiko hapo wataalamu wa physics wanaweza kusema umefanya workdone zero..

Ila kwa kupata knowledge asante sababu usingekwenda huko huenda tusingejua vichaa wapo kila mahali (mfano mtu kumwaga binadamu kama mchanga) ingawa thinking about it nadhani hii habari imeongezewa vikorombezwo
 
Hiyo jamii uliyojichanganya nao ni waabudu mizimu na mashetani hasa. Usikute asilimia kubwa ni raia wa gamboshi. Kimbia jitenge nao kama wewe una imani ya Mungu muumba wa mbingu na nchi. Hao si binadamu bali wamejaa mizimu na mashetani. Ni kitengo cha kishetani hicho.
 
Jihadhari na nyama za misibani, utalishwa nyama za misukule. Usukumani misukule inafugwa kwa ajili ya kufanya kazi ngumu, na pia inafugwa ili iliwe nyama
Aiseee Bujibuji umenifanya niwaze sana,,Nyama za misukule tena?
 
Hiyo jamii uliyojichanganya nao ni waabudu mizimu na mashetani hasa. Usikute asilimia kubwa ni raia wa gamboshi. Kimbia jitenge nao kama wewe una imani ya Mungu muumba wa mbingu na nchi. Hao si binadamu bali wamejaa mizimu na mashetani. Ni kitengo cha kishetani hicho.
Daah nimekuelewa Kakaa.Shukrani sana
 
Back
Top Bottom