Dudubaya amjibu Mwakyembe, azidi kumshukia Ruge Mutahaba

Wanaolalamika wengi hawana hoja, huo ndio msingi wangu.

Wote wanaolalama ni walioishiwa, na wanataka tuamini kuwa wao ndio waliolengwa na Ruge.

Huwezi kuwasisikia kina AY, Mwana FA n.k wakilalama, sasa akili haikwambii ni tofauti tu ya kiakili inawagharimu, Dudu hana vision za AY na hilo ndio tatizo wala sio kudhulumiwa.

Kuna Wasanii wengi kama ungewauliza wachague kfanya kazi na Ruge waibiwe au waende kwingine, nina imani wangemchagua Ruge, na ni wale wenye vision tu na si sampuli ya kina Dudu baya.

Ruge kama Binanadamu mwingine hawezi kukosa mapungufu, lakini natamani kusikia kutoka kwa Watu makini na sio hawa Waropokaji wasio na vision.
Jay d sio mtu makini ? Vipi sugu
 
Nimekuleza kuwa yawezekana wakawa hawajui mbinu mzuri ya kukueleza hoja zao.Naamini hoja wanazo isipokuwa wanafikishaje ujumbe.Kila mtu ana uwezo na namna ya kueleza jambo.Na bado kushindwa kujieleza kwa ushawishi kunaweza kusiondoe ukweli.Weye umekazania ushawishi wa kujieleza ki-hoja badala ya kuuelewa ukweli na bado unakiri kuwa Ruge kama binadamu lazima alikuw na udhaifu wake.
Nazungumzia mapungufu ya jumla, kwamba ukiwa na vision yako utanufaika zaidi ya kupoteza....ndio maana nimetoa mfano wa kina AY.
 
dudubaya ana ushamba mwingi hakuwa na usanii wowote wa maana kipindi icho.

ile kusifiwa upuuzi wa kuwadharirisha wengine kisa vita ya mawingu na wasafi basi kaona anakubalika sana.

kama ruge alikuwa anawanyonya kwa nini hawakwenda pengine ama kuanzisha studio yao.

aache utoto, kesho yakimfika atakosa msaada.
Na mbona wakati marehemu yuko hai hakutamka hayo?????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dudubaya ana ushamba mwingi hakuwa na usanii wowote wa maana kipindi icho.

ile kusifiwa upuuzi wa kuwadharirisha wengine kisa vita ya mawingu na wasafi basi kaona anakubalika sana.

kama ruge alikuwa anawanyonya kwa nini hawakwenda pengine ama kuanzisha studio yao.

aache utoto, kesho yakimfika atakosa msaada.
Usilolijua ni usiku wa giza Mkuu huyo msanii kafanya kazi na clouds kafanya kazi na bongo records anakijua anachokiongea usimbishie tu km wewe hujaona pande zote za shillingi..
 
Watanzania kwa unafiki tu sijawahi ona

Acha Dudubaya aseme anayo yasema hata akienda jela au akiuwawa ni yeye mwenyewe atabeba mizigo yake

Sasa mtu mnasema ni almasi akitokea mwingine kusema hapana sio almasi ni copper mnamchukia ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hoja dhaifu, nchi yetu inafuata utawala wa sheria, kama Ruge angekuwa mhalifu kiasi hicho basi waliokereka wangebisha hodi mahakamani kudai haki yao kwa "mnyonyaji" . huku ni kutokuitendea haki maiti, tukumbuke kuwa kila mtu laaazima atakufa siku moja, na kitu kizuri zaidi na cha kutia moyo ni kuwa "aliyekufa hafi tena ila ambaye bado". Maadam kila mtu atakufa basi sababu ya kufa kwetu isitushughulishe sana kuliko tutakumbukwa vipi tutakapoondoka duniani, na kama ukikosa kabisa zuri la kuwaachia basi panda hata mti wa kivuli upenuni kwako ili wajikinge na jua kali.
 
Kufa tutakufa sote kaka, wachana na dudu kama dudu hebu jaribu kufikiri Kwa mapana fikra zake, hivi ulishawahi kusikia msanii yeyote wakati Wa fiesta akisema labda amesaini mkataba Kwa ajili ya show zaidi ya kuwashortilisted tu..........
Hata kama Ruge angekuwa hakosei hilo bado kuna mengine mengi ambayo angekuwa anakosea tu yeye kama mwanadamu. Unamaanisha wote aliowakosea walitakiwa watafute vyombo vya habari kutangaza waliyokosewa na Ruge baada ya kufa??

Ishu hapa sio usahihi au kutokuwa sahihi kwa alichokisema Dudubaya, ila ni kitendo cha kutumia media kutangaza mambo yaliyomuumiza yeye binafsi kwa jamii nzima baada ya mhusika kufariki. Huu sio ubinadamu. Na nawashangaa ambao bado wanasapoti huu upuuzi.

Lakini pia kuna jambo lingine hatujaliangalia:

Kuna kitu kinaitwa Law of natural justice. Mtu hachukuliwi kama mwenye kosa bila kupewa nafasi ya kujitetea au kujibu tuhuma. Kipindi chote cha uhai wa Ruge hakuwahi kufungua mdomo kuwajibu waliokuwa wanamtuhumu mabaya. Huenda ni kwa jinsi alivyoumbwa maana ma genius huwa hawanaga kawaida ya kuongea ongea. Ila huenda kama Ruge angeamua kufungua mdomo kujibu huwezi jua nini kingetoka kinywani mwake; huenda angetuonesha upande wa pili wa watoa tuhuma wana makosa gani pia na kukufanya uwaone wao ndo hawafai! Ila kwa kuwa hakuwahi kusema na bahati mbaya hawezi tena kusema kwa kuwa amefariki basi si busara kuendelea kumtuhumu maana hana tena nafasi ya kupata haki yake ya 'natural justice'

Mwisho mkumbuke Ruge hakudeal na muziki tu. Vipi kuhusu maisha ya watoto 150 aliosaidia kupatikana hela ya upasuaji wa mioyo yao?? Vipi kuhusu wahanga wa mafuriko huko Kilosa aliookoa maisha yao?? Vipi kuhusu bodaboda aliowafungulia SACCOSS na kuwawekea milioni 60?? Vipi kuhusu mamalkia wa nguvu?? Vipi kuhusu vijana aliowasaidia kupitia FURSA, Vipi kuhusu...................the list is so long!

Yaani umsikilize na kuungana na Dudubaya na wenzake ambao hujajua hata wao walikosea wapi kumsema mabaya Ruge usahau haya mazuri kibao aliyoyafanya Ruge?? Ukijichunguza vizuri utagundua kuna mahali unakosea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
BASATA wameshamaliza! Kuanzia sasa ukimzungumzia Dudu baya utatanguliza "aliyekuwa msanii wa bongo fleva" na sio "msani wa bongofleva"
IMG-20190301-WA0011.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"wanao nipenda hawasemi na wanao nichukia hawanijui' by ruge

"kinacholalamikiwa ni cheo changu sio ruge ndo maana raisi kila analofanya analaumiwa kutokana na cheo ila sio kwamba ni m-baya" by ruge
jamaa alikuwa genius kweli
 
Hata kama Ruge angekuwa hakosei hilo bado kuna mengine mengi ambayo angekuwa anakosea tu yeye kama mwanadamu. Unamaanisha wote aliowakosea walitakiwa watafute vyombo vya habari kutangaza waliyokosewa na Ruge baada ya kufa??

Ishu hapa sio usahihi au kutokuwa sahihi kwa alichokisema Dudubaya, ila ni kitendo cha kutumia media kutangaza mambo yaliyomuumiza yeye binafsi kwa jamii nzima baada ya mhusika kufariki. Huu sio ubinadamu. Na nawashangaa ambao bado wanasapoti huu upuuzi.

Lakini pia kuna jambo lingine hatujaliangalia:

Kuna kitu kinaitwa Law of natural justice. Mtu hachukuliwi kama mwenye kosa bila kupewa nafasi ya kujitetea au kujibu tuhuma. Kipindi chote cha uhai wa Ruge hakuwahi kufungua mdomo kuwajibu waliokuwa wanamtuhumu mabaya. Huenda ni kwa jinsi alivyoumbwa maana ma genius huwa hawanaga kawaida ya kuongea ongea. Ila huenda kama Ruge angeamua kufungua mdomo kujibu huwezi jua nini kingetoka kinywani mwake; huenda angetuonesha upande wa pili wa watoa tuhuma wana makosa gani pia na kukufanya uwaone wao ndo hawafai! Ila kwa kuwa hakuwahi kusema na bahati mbaya hawezi tena kusema kwa kuwa amefariki basi si busara kuendelea kumtuhumu maana hana tena nafasi ya kupata haki yake ya 'natural justice'

Mwisho mkumbuke Ruge hakudeal na muziki tu. Vipi kuhusu maisha ya watoto 150 aliosaidia kupatikana hela ya upasuaji wa mioyo yao?? Vipi kuhusu wahanga wa mafuriko huko Kilosa aliookoa maisha yao?? Vipi kuhusu bodaboda aliowafungulia SACCOSS na kuwawekea milioni 60?? Vipi kuhusu mamalkia wa nguvu?? Vipi kuhusu vijana aliowasaidia kupitia FURSA, Vipi kuhusu...................the list is so long!

Yaani umsikilize na kuungana na Dudubaya na wenzake ambao hujajua hata wao walikosea wapi kumsema mabaya Ruge usahau haya mazuri kibao aliyoyafanya Ruge?? Ukijichunguza vizuri utagundua kuna mahali unakosea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
upo sahihi mkuu kwa wanao mjua wana sema jamaa hua anapenda nidhamu katika kazi mfano: makonda na diaomond aliwapa sana air time ila walivyokeuka maadili akawawajibishwa ndo bifu likaanzia hapo
 
Hata kama Ruge angekuwa hakosei hilo bado kuna mengine mengi ambayo angekuwa anakosea tu yeye kama mwanadamu. Unamaanisha wote aliowakosea walitakiwa watafute vyombo vya habari kutangaza waliyokosewa na Ruge baada ya kufa??

Ishu hapa sio usahihi au kutokuwa sahihi kwa alichokisema Dudubaya, ila ni kitendo cha kutumia media kutangaza mambo yaliyomuumiza yeye binafsi kwa jamii nzima baada ya mhusika kufariki. Huu sio ubinadamu. Na nawashangaa ambao bado wanasapoti huu upuuzi.

Lakini pia kuna jambo lingine hatujaliangalia:

Kuna kitu kinaitwa Law of natural justice. Mtu hachukuliwi kama mwenye kosa bila kupewa nafasi ya kujitetea au kujibu tuhuma. Kipindi chote cha uhai wa Ruge hakuwahi kufungua mdomo kuwajibu waliokuwa wanamtuhumu mabaya. Huenda ni kwa jinsi alivyoumbwa maana ma genius huwa hawanaga kawaida ya kuongea ongea. Ila huenda kama Ruge angeamua kufungua mdomo kujibu huwezi jua nini kingetoka kinywani mwake; huenda angetuonesha upande wa pili wa watoa tuhuma wana makosa gani pia na kukufanya uwaone wao ndo hawafai! Ila kwa kuwa hakuwahi kusema na bahati mbaya hawezi tena kusema kwa kuwa amefariki basi si busara kuendelea kumtuhumu maana hana tena nafasi ya kupata haki yake ya 'natural justice'

Mwisho mkumbuke Ruge hakudeal na muziki tu. Vipi kuhusu maisha ya watoto 150 aliosaidia kupatikana hela ya upasuaji wa mioyo yao?? Vipi kuhusu wahanga wa mafuriko huko Kilosa aliookoa maisha yao?? Vipi kuhusu bodaboda aliowafungulia SACCOSS na kuwawekea milioni 60?? Vipi kuhusu mamalkia wa nguvu?? Vipi kuhusu vijana aliowasaidia kupitia FURSA, Vipi kuhusu...................the list is so long!

Yaani umsikilize na kuungana na Dudubaya na wenzake ambao hujajua hata wao walikosea wapi kumsema mabaya Ruge usahau haya mazuri kibao aliyoyafanya Ruge?? Ukijichunguza vizuri utagundua kuna mahali unakosea sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza nikuombe radhi Kwa kujikuta umenielewa contrary na nilivomaanisha. Siko hapa kumjadili Marehemu Ruge au bwana dudubaya ila Niko hapa kujadili hoja, kama ilivokawaida mpaka mwanadamu anaondoka duniani anakuwa kafanya mengi yaliyo mazuri na mengi yaliyo mabaya pia hivo hivo na Kwa marehemu Ruge pia. Imekua ni kawaida na watu tumezoea watu kusifia mema aloyafanya MTU pindi akifariki na huwa tunajitahidi sana kuyafunika mabaya yake, na si kwamba watu wanakua hawaukumbuki ubaya walotendewa na marehemu, la hasha !!! Huyu dudubaya Leo kaamua kuja kitofauti kabisa na kunena mabaya ya marehemu kinyume na ilibozoeleka.

Hii principle of natural justice kwamba kujieleza, umesema Ruge alikua hafumbia mdomo kujibu shutuma hilo haliharalishi wala kumfutia hizo shutuma zaidi ya kuwaacha watu na uwalakini.

Ruge kafariki kama ilivo Kwa watu wengine, na si Ruge tu alivosemwa Kwa ubaya baada ya kifo chake kuna wengine wanasemwa ila wasemaji wanakosa platform za kusemea ili mambo yaenee mitandaoni kama alivopata platform dudubaya na mambo kusambaa sana Kwa sababu marehemu na huyu msemaji wrote ni maarufu.

Kusemwa Kwa ubaya pindi ukifariki si jambo la kushangaza maana hata hayo mabaya unayosemwa nayo ni kweli Kwa namna moja uliyatenda Kwa sababu matendo yetu duniani ni mchanganyiko Wa mema na maovu, hivo ukiona wanakusifia Kwa mazuri ujue wamekustahi kukufichia uovu wako na si kwamba hawajui na pengine sababu yaweza kuwa watu wanaogopa kuanika maovu yako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom