CCM na Ruge Mutahaba wanavyowanyonya Bongo Flavor

TAJIRI MKUU WA MATAJIRI

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
5,721
10,220
*RUGE MUTAHABA (Clouds Media Group ) AWATUMIA WASANII KWA MASILAHI YA CCM kwa UNYONYAJI.


Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mkurugenzi wa Makampuni ya Clouds media group Bwana Ruge Mutahaba ameonyesha wazi unyonyaji wake kwa Wasanii wa Muziki wa Kizazi kipya kwa kuwapa onyo kali kwa kuwataka kuipigia
kampeni CCM kwa kuwalipa shs 300, 000 na kuwaambia kuwa wasipokuwa tayari nyimbo zao hazitapigwa katika vituo hivyo vya Clouds fm na Clouds Tv.

Mtakumbuka kuwa hata ile hafla iliyofanyika Mlimani City iliyosemekana kuandiwa na Wasanii kwa kile walichodai ni Wasanii kumuaga Rais Jakaya Kikwete ni kiini macho, mchongo uko hivi,

Mwenyekiti wa CCM Taifa akijinasibu kuwa wana maarifa ya kushinda na kwa kutambua upepo wa siasa kugeuka aliamua kumtumia Ruge kuwaalika wasanii lengo likiwa ni kuwataka tena kinguvu kushiriki kuwapigia kampeni CCM kwa ujira huo na Ruge kutoa vitisho kuwa wasishiriki kufanya Kampeni za UKAWA na kwenda mbali zaidi kwa kuwaambia kuwa wakikiuka masharti hayo nyimbo na Video zao hazitapigwa kamwe na hawatashirikishwa kwenye matamasha kama vile FIESTA na mengine.

Hayo ni maagizo pia kutoka ngazi za juu ya chama kuwa wasanii washiriki kampeni za UKAWA na zoezi hilo pia limeratibiwa kwa ukaribu zaidi na January Makamba na Ridhiwani Kikwete ili kuhakikusha wasanii wanaiunga mkono CCM.

Wasanii wamekuwa wakilalamikia Hati Miliki (IP (Intellectual Property )) ambayo inasababisha kunyonywa haki zao na Rais JK aliwaahidi wasanii kuwafungulia Studio kubwa ya Kuredia Mziki lakini Studio hiyo ni kiini macho na imekuwa ikinilikiwa na Clouds media chini ya Ruge Mutahaba.

Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi (Sugu) aliwahi kuitilafiana na Uongozi wa Clouds Media kwa kile kilichodaiwa kuwa ni unyonyaji wa hali ya juu kwa wasanii inayofanywa na Bwana Ruge na ndio maana wasanii hawaendelei.

Ruge Mutahaba, tunajua wazi kua CCM imekuwa ikitumia chombo chenu kwa manufaa yake na wewe umekuwa mnyonyaji mkubwa, haki ya kumpigia kampeni mgombea ni haki ya Mtu mwenyewe, kwanini utumie vyombo vyako kushurutisha wasanii kwa maslahi yako na CCM na kuwataka wasiipigie kampeni UKAWA, Tunakutaka uache mara moja na Demokrasia na uhuru utumike, tunajua unafanya hayo kwa mamlaka ya nani,

Nihitimishe kwa Wasanii, ni bora na haki yenu kufanya maamuzi yenu bila kushinikizwa, sasa basi mkiwa na haki hiyo ni bora kujitathimini, hivi wewe ni wa kutumika kwa kulipwa Chakula na kupiga picha na Rais na kulipwa Laki Tatu na kukushurutishwa kwa kuamliqa maamuzi na mtu eti kisa hatapiga nyimbo ama video yako, kwani kituo ni Clouds tu?, tuamke na kuyatafuta mabadiliko na uhuru wa maamuzi ba kuondoa nfumo Kandamizi wa akiba Ruge, Riziwani na January Makamba.

#Amua Hatima ya taifa na maisha yako kwa kushiriki katika mchakato wa kumpata kiongozi bora kwa kufanya maamuzi kulingana na matakwa yako,

#Ruge acha kutumika.


CC:- Nyani Ngabu,mshana jr,Ritz
 
kwan clouds ndo radio pekee ya kukufanya ufanikiwe? hv wakina mbaraka mwishehe,remmy ongara na wengne mbona tanzania ilikuwa inawajua kpnd hcho clouds ilikuwapo? wa kina mr ii sugu wametoka miaka ya tisini clouds ilikuwapo? tanzania kuna radio 15 kubwa acha zle ndogo ndogo haya kuna TV 10 kubwa leo ni bora nyimbo yako wakionyesha EATV unaonekana nchi 3 itakuwa clouds tv ambayo wako nyuma sana kwa graphic ukilinganisha na EATV leo wasanii wanaompgia magoti ruge ni wapuuzi wasio jitambua mbona cku hz kuna njia nying sana za kutoka kmuzk nje ya clouds ? leo kama wanamuona nick wa pili ni genus wakat ufahamu na upeo wake ni wakawaida sana wasanii wabadilike clouds imekuwa kama ccm empire ya sanaa kwa kpnd hiki wafanye nao mpango je wakisusa wote clouds watawapeleka wakina nan fiesta ?
 
Tunaomba uweke hapa ushahidi usio tia shaka juu ya madai yako!

Huu ni uzushi ulio tukuka hakuna msanii ambaye anawezwa kulazimishwa kumpigia mtu campaign mtu fulani ni uamuzi binafsi wa wasanii wenyewe na hakuna mtu anaweza kulazimishwa kufanya jambo!

Halafu madai ya kusema mtu asipo piga campaign hatopigiwa mziki wake ni ya kijinga kabisa....kwa hiyo unataka kutuambia kuwa wanaopigiwa nyimbo zao wote hupiga campaign?Pia Clouds fm sio radio pekee nchini!

Mimi nakuomba kama una ushahidi na unayo yaongea yapeleke TCRA au Basata au weka hapa ushahidi!

Tunajua kabisa kipindi hiki mnamihemko sana kwa hiyo mnataka kumuingiza kila mtu kwenye siasa zenu zisizo na msingi kabisa!
 
Oiiiii oiii izooooo business maliza eti Nikki na uwezooooo mdogo sana siunajua washamba kaja mjini lazima akipewa air na jisahau izooooo kaza ivoo mziki wako utaishii mileleeeee
 
Wacha waende kama mashibiki na wapenzi wa miziki yao ni sisimu tu wacha wapige kampeni ila kiusanii watakuwa wamejiua kwa kupoteza wote wa wapenzi na nashabiki wao wa vyama vingine..
 
Hivi Jb amejenga kweli au Amekodishiwa nyumba na ccm kwa kujipendekeza kwa muheshimiwa ni hatari !!
 
Huo uzi niwaukweli kabisa km ww unabisha hufuatilii muziki wetu wasanii wengi sana wakiilalamikia clouds media group kwa unyonyaji wao na km ukileta ujuaji utapotea mf mzuri 20%, Dudubaya hata Mr Nice kwa kiac kikubwa clouds imechangia kumpoteza.
 
Na ndio maana wasanii wengi wakubwa huwezi kuwaona kwenye majukwaa ya upinzani kidogo mwaka huu angalau Roma, Ney, Kala nawaona.
 
Na ndio maana wasanii wengi wakubwa huwezi kuwaona kwenye majukwaa ya upinzani kidogo mwaka huu angalau Roma, Ney, Kala nawaona.

Hao ndio waliojitambua,hata hivyo ukawa hawana haja ya kukusanya watu kwa mbiu,sifa za viongozi wao ni kivutio tosha
 
Back
Top Bottom