Bilionea Asigwa
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 16,515
- 28,487
Msanii Dudubaya ambaye siku za karibuni ameachia wimbo wake mpya unaofahamika kwa jina la 'Kokoriko' amefunguka na kusema kuwa msanii Ray C ambaye alisaidiwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kuachana na matumizi ya dawa za kulevya amerudia tena.
Kwa mujibu wa Dudubaya anasema msanii huyo hakuwa na dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake kuachana na matumizi ya dawa hizo za kulevya bali alipata tu msukumo na ndiyo maana ameweza kurudia tena matumizi ya dawa hizo.
Dudubaya alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha eNEWS alisema kuwa mtu kuacha matumizi ya dawa hizo ni lazima awe na dhamira ya dhati kutoka moyoni mwake ndiyo anaweza kufanikiwa la sivyo ni sawa na kucheza kwani baada ya muda atarudia tu.
"Kuacha hata ufusika au kitu chochote kile ni dhamira ya moyo wako, hakuna kitu chochote kinaweza kumsaidia mtu kama hana dhamira ya dhati kutoka moyoni kutaka kuacha kitu fulani, ndiyo maana hata Ray C amerudia matumizi ya dawa za kulevya yuko Bunju.
Ray C alisaidiwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete lakini watu wote na wadau wamemshindwa saizi yuko Bunju anakula ngada kama kawaida, hivyo unatakiwa useme kutoka moyoni nachukia kitu hiki hapo ndiyo utatoboa kwenye hilo."
Alisema Dudubaya.