engmtolera
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 5,150
- 1,437
MSANII wa Bongo Fleva, Godfrey Tumaini Dudubaya (pichani) hivi karibuni alitupwa selo baada ya kukamatwa na polisi wilayani Geita kwa kudaiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, Ijumaa lina kisanga kamili.
Kwa mujibu wa mlalamikaji, Warwa Nkurunzinza, Desemba 31, 2010 alimtumia Dudubaya fedha shilingi 250,000 kupitia akaunti yake ya Benki ya NBC Tawi la Geita kwa lengo la kufanya shoo kwenye mkesha wa kuamkia Januari Mosi, mwaka huu.
Hata hivyo, Nkurunzinza alidai kuwa, pamoja na kufanya hivyo, Dudubaya hakutokea hali iliyofanya amfungulie kesi msanii huyo katika kituo cha polisi na kupewa RB yenye namba GE/RB/1829/04 ili akamatwe.
Msanii huyo alipokamatwa alifikishwa mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo ya Nyankumbu, wilayani Geita, Mbauro Mbauro na kusomewa mashtaka yake.
Mbele ya Hakimu Mbauro, Nkurunzinza alidai kuwa, alikuwa ameandaa shoo katika Kijiji cha Rwamgasa nje kidogo ya Mji wa Geita iliyokuwa itumbuizwe na Dudubaya lakini akaingia mitini hadi alipokamatwa Mei 28, mwaka huu.
Hata hivyo, mshtakiwa huyo yuko nje kwa dhamana baada ya kutimiza masharti kwa kupeleka wadhamini watatu ambao ni wakazi wa wilaya hiyo na fedha taslimu shilingi 100,000.
Katika hatua nyingine, mwandishi wa habari hii chupuchupu apewe mkongoto na wapambe wa msanii huyo baada ya kumfotoa Dudubaya akiwa mahakamani hapo.
Kesi hiyo ilihairishwa hadi Juni 8, mwaka huu itakapotolewa hukumu.