Dudu baya aka konky master

Jamaa anajua mpaka kilichomo ndani ya area 51 kule nevada na wakati ni eneo lenye usiri mkubwa kiasi kwamba raia wa marekani wenyewe hawajui kilichomo.
Juzi kati nikasikia anachambua kuhusu ile ndege ya Malaysia iliyopotea,eti akasema yeye anajua ilipo.
 
Haahaaaa hapa sasa nilichoka kabisa
 
Mimi naona Anatumia akili kwakuwa badala ya kuwa anapiga kelele mitandaoni Ila amegeuza Kama fursa ile kuongea ongea atakuwa anapata riziki ya halali.

Jambo ambalo anabidi kuboresha aboreshe katika kuacha kuongelea mambo negativity Kama kuwaponda wasanii Ila ajikite kuelezea mambo ya msingi yenye tija.

Awe Kama Mwalimu ambaye analenga kuwapa watu ufahamu.
 
Pamoja na yote
Naangalia sana YouTube na mambo ya nyumbani sana.

Nikaona akihojiwa masuala kadhaa
Yaani jamaa anatokwa jasho usoni hana hata tissues

Anafuta uso kwa mkono halafu anazuga kama anashika kochi kumbe anafutia jasho lake.

Yaani kuna watu ustaarabu uliwapita kushoto
Mtoto wangu wa miaka minne hawezi kufanya hivyo.

Ila mengine sawa anaongea

Ila tujifunze ustaarabu wala sio kazi kubwa
 
Nadhani mleta mada aidha kasema fact kukuhusu wewe au mtu wako wa karibu.
Ungesema kasema moja, mbili tatu ambazo sio kweli na fact ni Aa, be che.
Sasa hapa kati ya wewe na yeye nani ana shida zaidi?
 
Mwamba ni ex seminarian nampata sana. Sishangai kama anayo madini juu mada mbalimbali.
 
Uzuri wa Dudu anaeleza vitu kwa undani sana, anaongea facts bila kupepesa, nashuhudia hayo kwa mambo ninayoyajua.
 
Dudubaya anatumia haki zake za kikatiba na kibinadamu kujieleza.

Tatizo si Dudubaya anajifanya much know.

Tatizo Watanzania wengi hawasemi, wako timid.

Tatizo hatuna wataalamu au wataalamu hawasemi.

Nature abhorrs a vacuum. So when experts do not speak, Dudubaya will.

Dudubaya goes "Where Eagles Dare", even without expertise.

Mara nyingine njia nzuri kabisa ya kuwatoa wataalam pangoni ni kusemea taaluma yao bila utaalamu, halafu wao watoke waje kukukosoa.

Ukisema Dudubaya ni much know kaharibu maongezi ya vita vya Ukraine, tupe na wewe uchambuzi wako unaomkosoa Dudubaya na kuweka alichokosea sawa.
 
Dudubaya anatumia haki zake za kikatiba na kibinadamu kujieleza.
Broo nimecheka sana hii Line yako ya kwanza
You are absolutelly right mkuu. Kabisa yani💯
 
Ninajua kwanini biashara zina kufa Tanzania na nini kifanyike pia kwanini mitaji siyo tatizo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…