Allency
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 13,731
- 13,100
Watanzania tuna shida sana, mara nyingi tunajitahidi kuukwepa ukweli. Mtu akitekeleza sheria mnaaza kusema eti uonevu au matumizi ya dola. Sheria zipo wazi lakini mnajitahidi kuzikwepa na hamtaki kuzifuata. Hata Mungu katuagiza kutii mamlaka zilizo juu yetu. Sasa utasemaje unatii mamlaka huku hufuati sheria za mamlaka husika? Halafu hizi sheria si zimetungwa na bunge, kama zinatukandamiza kwa nini tumpelekee lawama mkuu wa nchi wakati yeye anatekeleza sheria zilizowekwa na bunge? Je mlitaka asisimamie sheria? Binafsi naamini hakuna laana yoyote itakayompata kwa sababu anasimamia sheria, bali laana itatupata sisi tunaolitumia vibaya jina la Mungu kuweza kumlaani yule anayesimamia sheria ambazo Mungu mwenyewe katuagiza tuzitii.
Biblia takatifu katika kitabu cha Warumi 13:1-5
"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."
Wewe unayesema anasimamia sheria ipi?
Ipi sheria inayompa Raisi wa jamuhuri mamlaka ya kuzuia mikutano ya siasa?