Dua mbaya na laana zinazoelekezwa kwa Mh Rais, zitamuacha salama?

mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,385
2,000
Kuna vilio kila mahali na dua mbaya kuelekea kwa rais Magufuli na serikali yake hali ambayo sasa inaogopesha! Kila ukifungua mtandao wa kijamii utakutana na malalamiko, dua na laana zikuelekezwa kwa Magufuli na serikali yake.

Hata wale waliokua wanamuunga mkono sasa wamemgeuka na kushangaa anayofanya.

Wengi wanamlaumu kwa uonevu na kutumia dola vibaya kukandamiza haki za raia.

Kumkosoa rais na serikali yake sssa kunaonekana ni kumtusi na uchochezi.

Kwa sasa watu wapo katika hofu kubwa. Hujui ni wakati gani ukikosoa au kutoa maoni yako juu ya utawala huu utaitwa
mchochezi au umemtusi rais.

Kwa mfano nikisema namchukia rais Magufuli nitaambiwa nimetoa lugha ya uchochezi. Yaani sio maoni yangu binafsi bali etu ni uchochezi.

Serikali hii ina hofu kubwa. Sijui ni kwa nini? Labda wamegundua kwamba waliyoahidi wananchi ni vigumu kutekelezeka hivyo wanazuia wakosoaji wasiseme? Hofu kuu iliyonayo serikali hii dhidi ya wakosoaji wake inafanya wajikute wanajihami hata kwa mambo madogomadogo yasiyokuwa na msingi! Mambo ambayo yanafanya kila mwenye akili timamu ashangae! Kuna nini?

Hii model ya utawala anayoijaribu Magufuli hapa nchini haitafanikiwa. Tanzania sio Rwanda wala North Korea. Tanzania kwa miaka mingi tumezoea uhuru wa kukosoana na kupingana bila kupigana.

Sasa naona huu utamaduni mzuri unaminywa. Nimekuwa najiuliza hivi kile kikosi kazi alichounda Mh Magufuli wakati wa kampeni kumshauri namna ya kufanya mabadiliko makubwa katika nchi ndiyo haya wsliyomshauri?

Hivi ni kweli tutasonga mbele kimaendeleo huku kukiwa nacauti nyingi namna hii zikiulaumu utawala wa nchi hii. Natumia neno 'utawala' kwa makusudi kwa sababu hii awamu ya tano inatawala badala ya kuongoza! Yaani nchi inaendeshwa kikoloni zaidi.

Nimalizie kwa kuulizs tena swali, je, ni kweli rais ataweza kufanikiwa kutekeleza mipango yake ya maendeleo huku akipingwa na kulaaniwa vikali hivi na wananchi wake? Rais aliyejipambanua kama mcha Mungu, akionekana kwenye nyumba za ibada kila siku, leo analaaniwa na kuombewa dua mbaya hivi?

Ni wakati muafaka kwa rais na serikali yake kujitafakari upya namna ya kuileta nchi pamoja na kuattract zaidi support kutoka kwa wananchi badala ya kufanya mambo yanayochochea chuki dhidi ya serikali na kuwagawa watanzania!

Hii mambo ya kuminya uhuru wa maoni na taarifa hayajawahi kusaidia nchi yoyote kusonga mbele. Demokrasia na maendeleo ni vitu pacha. Vinakwenda pamoja. Demokrasia huleta maendeleo na maendeleo huleta demokrasia! Maendeleo ya kweli ni maendeleo ya watu sio maendeleo ya vitu. Na bila uhuru na demokrasia hakuna maendeleo ya watu!

Mwenye masikio na asikie!
 
mcfm40

JF-Expert Member
Nov 2, 2010
4,385
2,000
Dua hizo ndizo zinazompa ujasiri Rais katika maamuzi yake. Wanaomuombea mema ni wengi kuliko wanaomuombea manaya. Busara ya Mungu ndiyo inayoongoza utendaji wa Rais wetu.
Sidhani! Busara ya Mungu haiwezi kumfanya mtu aogope kukosolewa! Hekima ya Mungu haimuelekezi mtu kuweka ndani wanaotofautiana naye kimawazo! Nadhani anaongozwa na hekima ya kishetani!
 
NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203

Narudia tena sentence hii mnao muombea mabaya Rais wetu hamzidi elfu 50 kwenye million 50,
Na 2020 kwa kishindo cha ajabu na anayepinga tuweke dau mbele ya mashaidi.

Mimi naweka kibanda changu Mbweni na ajitokeze nyumbu hapa.
 
Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,011
2,000
Watanzania tuna shida sana, mara nyingi tunajitahidi kuukwepa ukweli. Mtu akitekeleza sheria mnaaza kusema eti uonevu au matumizi ya dola. Sheria zipo wazi lakini mnajitahidi kuzikwepa na hamtaki kuzifuata. Hata Mungu katuagiza kutii mamlaka zilizo juu yetu. Sasa utasemaje unatii mamlaka huku hufuati sheria za mamlaka husika? Halafu hizi sheria si zimetungwa na bunge, kama zinatukandamiza kwa nini tumpelekee lawama mkuu wa nchi wakati yeye anatekeleza sheria zilizowekwa na bunge? Je mlitaka asisimamie sheria? Binafsi naamini hakuna laana yoyote itakayompata kwa sababu anasimamia sheria, bali laana itatupata sisi tunaolitumia vibaya jina la Mungu kuweza kumlaani yule anayesimamia sheria ambazo Mungu mwenyewe katuagiza tuzitii.

Biblia takatifu katika kitabu cha Warumi 13:1-5
"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,318
2,000
Kila mamlaka MUNGU anaijua na ndio alieiteua,kumchagua kwetu ni kama mashahidi na MUNGU ndo kamuweka,tuliwahi kuhubiriana ni yupi aje atakaefaa,na sifa tulizoziwaza na tulizopewa na viongozi wa vyama mbali mbali ni sifa za tulienae sasa,naamini yupo kwa mpango MUNGU na binafsi ninamuombea
 
Odhiambo cairo

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
13,058
2,000
Mimi nadhani hofu ya Maghufuli, CCM na serikali yake ni kwa jinsi gani wananchi na wapiga kura walivyowahasi mwaka jana na kufikia kugawa kura almost nusu kwa nusu . Wanafikiri kwa kunyamazisha watu !!, basi watarudi kundini wapende wasipende.

Mimi pia nasema kokote duniani hakuna taifa lililofanikiwa kupitia mkono wa chuma na ukandamizaji. Niwashauri ndani ya chama na serikali yake kumshauri vizuri mkuu
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
76,343
2,000
Watanzania tuna shida sana, mara nyingi tunajitahidi kuukwepa ukweli. Mtu akitekeleza sheria mnaaza kusema eti uonevu au matumizi ya dola. Sheria zipo wazi lakini mnajitahidi kuzikwepa na hamtaki kuzifuata. Hata Mungu katuagiza kutii mamlaka zilizo juu yetu. Sasa utasemaje unatii mamlaka huku hufuati sheria za mamlaka husika? Halafu hizi sheria si zimetungwa na bunge, kama zinatukandamiza kwa nini tumpelekee lawama mkuu wa nchi wakati yeye anatekeleza sheria zilizowekwa na bunge? Je mlitaka asisimamie sheria? Binafsi naamini hakuna laana yoyote itakayompata kwa sababu anasimamia sheria, bali laana itatupata sisi tunaolitumia vibaya jina la Mungu kuweza kumlaani yule anayesimamia sheria ambazo Mungu mwenyewe katuagiza tuzitii.

Biblia takatifu katika kitabu cha Warumi 13:1-5
"Kila mtu hana budi kutii serikali inayotawala. Kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu; na serikali zote zilizopo zimewekwa na Mungu. 2 Kwa hiyo anayepinga mamlaka inayotawala ana pinga chombo kilichowekwa na Mungu; na watu wanaoasi watajiletea hukumu. 3 Kwa maana watawala hawatishi watu wanaotenda mema bali wale wanaotenda maovu. Kama hupendi kuishi kwa kumwogopa mwenye mamlaka, basi tenda mema naye atakusifu. 4 Maana mwenye mamlaka ni mtumishi wa Mungu kwa manufaa yako. Lakini kama ukitenda maovu, basi ogopa kwa maana hatembei na silaha bure. Yeye ni mtumishi wa Mungu anayetekeleza adhabu ya Mungu juu ya watenda maovu. 5 Kwa hiyo ni lazima kutii wenye mamlaka, si kwa sababu ya kuogopa adhabu tu bali pia kwa ajili ya dhamiri."
Kwa mfano , ni kifungu gani katika sheria ya wapi kinachokataza mikutano ya kisiasa ya hadhara Tanzania ? Naomba kifungu hata cha biblia .
 
ISIS

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
91,509
2,000
Dua hizo ndizo zinazompa ujasiri Rais katika maamuzi yake. Wanaomuombea mema ni wengi kuliko wanaomuombea manaya. Busara ya Mungu ndiyo inayoongoza utendaji wa Rais wetu.
Well said. ...wamesahau DUA LA KUKU HALIMPATI MWEWE. ...EHH RHABUKA NAKUOMBA UMLINDE RAIS WETU JPJM
 
shamajengo

JF-Expert Member
Jan 17, 2015
1,150
2,000
Nasikitika viongozi wa dini hawalioni hili wamekaa kimya as if yanayofanyika ni sawa
 
legend Babushka

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
491
1,000
Mimi sioni sababu ya kumtakia mabaya. Naamini anafahamu anayofanya kwenye kuongoza kwake, na kama anasikia vilio vya watu ni vema amuombe Mungu ili ampe hekima anaowaongoza wasilalamike. Ila akumbuke pia machozi ya watu sio mazuri. Ukimletea mtu maendeleo ambayo ndani yake hakufurahii, haina maana. Namuomba Mungu ayafute machozi yetu na kumfanya Raisi wetu kuwa ni furaha kwa watanzania wote.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom