mcfm40
JF-Expert Member
- Nov 2, 2010
- 4,452
- 3,150
Hivi vandugu, kama kingereza hakipandi kwa nini tusizungumze Kiswahili halafu kikatasfiriwa kama wafanyavo wenzetu wachina? Tanzania ni nchi ambayo Kiswahili na Kiingereza ni lugha zao rasmi za kimawasiliano. Sasa inakuwaje viongozi wakuu wa serikali kama raisi na Katibu Mkuu kiongozi kushindwa kuzungumza kiingereza sawasawa (fluently)? Kuna tatizo la namna tunavyowa pata viongozi wetu wakuu! Busara ya kawaida inataka Kiongozi mkuu kabisa wa nchi kama rais, makamu wa raisi, waziri mkuu, jaji mkuu, spika wabunge walau wawe vizuri kimombo kwa sababu hawa sio national figures tu bali ni international figures. Simaanishi kwamba kujua kiingereza ndio kuendelea bali ni jambo la ajabu kwamba viongozi wakuu wetu wengi wao wanamumunya mumunya tu lugha. Nadhani pamoja na sifa nyingine ni vizuru kiongozi mkuu wa serikali akawa na uwezo wa kuzungumza walao lugha mbili za kimataifa hata hiyo lugha moja basi vizuri. Wakati wa Press conference jana na juzi mwili ulikuwa unapatwa na baridi kikwete alipokuwa anaotoa hotuba yake kwa kiingereza! Akiacha kusoma tu basi alikuwa anapata shida sana kupata misamiati sahihi ya kuongea anapojaribu kukazia pointi yake. Funga kazi ilikuwa wakati wa press konferensi na Obama WAKATI WA MASWALI NA MAJIBU aliposema " THAT QUESTION SHOULD HAVE BEEN ASKED ME!! AKITAKA KUSEMA "THAT QUESTION SHOULD HAVE BEEN DIRECTED TO ME." Hili ni lile swali alilouliza mwandishi mmoja wa Tanzania kwa Obama kitu kama hiki: Are you satisfied with the progress of MCC? Sas kama ungenge ni shida mpka kwa viongozi wetu wakuu, je itakuwaje kwa wale wa ST kanumba wanaotakiwa kusoma na kujibu mitihani kwa kiingereza? huu ni ushahidi kwamba ni wakati sasa wa kukikumbatia Kiswahili chetu na kuachana utumwa. Madhara ya kung'ang'ania kuzungumza lugha usiyoielewa vizuri ni kwamba huwezi kuongea kwa hisia na vionjo vyako vya asili na pia ujumbe hauwafikii walengwa kwa impact inayotakiwa, licha ya kwamba unaweza usieleweke pia. mwisho inakuwa ni kujidhalilisha.