DSTV yazindua kifurushi cha 17000, nafuu mno

MstahikiMeya

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
1,633
559
31.jpg

MultiChoice Africa ina furaha kuwatangazia kuwa imezindua kifurushi kipya maalumu kwa watanzania. Kifurushi hiki kimetengenezwa mahususi kwa watanzania kikiwa na chaneli zaidi 65 za kitaifa na kimataifa zitakazotoa burudani pekee kwa familia za kitanzania.

Kifurushi hiki kipya cha Bomba kina chaneli nyingi nzuri ikiwemo chaneli iliyozinduliwa hivi karibuni ya Maisha Magic Swahili inayoonyesha filamu za kitanzania; chaneli ya Telemundo inayojulikana kwa michezo ya kuigiza ya kimapenzi ya Amerika ya Kusini pamoja na Nickelodeon na Disney Junior zinazoonyesha vipindi vya watoto.

Meneja Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel, alisema kuwa kifurushi kipya cha Bomba kitagharimu kiasi cha TSh 17,000 tu kwa mwezi: " Uzinduzi wa kifurushi hiki cha Bomba ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu, kuona kuwa sasa watanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.

Kila wakati, MultiChoice inafanya jitahada za kubuni namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani. Sasa, watanzania wameongezewa uwanja wa uchaguzi kwa bei iliyo chini na kiwango cha juu cha burudani ikiwemo filamu, makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo."

Usikose ofa yetu ya uzinduzi huu - watakaojiunga watapata DStv ikiwemo gharama ya ufundi kwa TSh 99,000 tu kwa kipindi maalum. DStv Bomba pia itakuwa na chaneli za Africa Magic Epic Movies, Discovery World, CBS Action, CBS Reality na CBS Drama pamoja na Select Sport 1 na 2 kwa vipindi vizuri vya michezo. SuperSport Select na SuperSport Select 2 zitaonyesha ligi kuu ya Uingereza, Kombe la klabu bingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Hispania, Ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi. SuperSport Blitz itawaletea habari zote za michezo. Kwa habari zaidi kuhusu burudani kwa ajili ya familia,
 
hao dstv bei zao kubwa sana kwa pageg za prium kwa africa mashariki lakini africa ya kusini ni sawa na bure
 
Aiseee mie ombi langu ni waache kututoza hiyo subscription fee kwa terms za dollar.. Inatuumiza sana.. Imagine DSTV Premium imeruka toka TShs. 135,000/= per month to TShs. 142,000/= just kwa sababu dola imepanda..!
 
Tatizo Shilingi yetu haina Thamani tena. Tusipopata viongozi wasomi wazalendo wenye mapenzi mema na hii nchi, basi tutegemee mporomoko huu wa Tsh zaidi na zaidi na mfumuko wa bei zaidi.
 
Ngoja nitafute mteja niuze azam tv.
Yaani mkuu AMU hii taarifa ni njema sana, kwa style hii azamtv kazi wanayo labda waboreshe huduma zao kwa kuongeza chanel ambazo zitakuwa zinanyesha ligi mbalimbali za barani ulaya.
 
Hiyo package ya kuonyesha channel 2 za supersport ni sh. ngapi?

17500...ndio hvyo mkuu

Mkuu tofautisha supersport from the rest.. Wanaposema supersport wanamaanisha channel zao za michezo only.. Iko chini ya mwamvuli mmoja wa DSTV.. Ina maana kwa kifurushi hicho cha TShs. 17,500/= huwezi kuona channel yeyote ya supersport..

Sijaelewa swali la DISOLN vizuri ila kama anamaanisha channel za supersport nitakuwa nimemjibu hapo juu..
 
Last edited by a moderator:

Nimekupata vyema mkuu asante umejibu swali langu
 
Last edited by a moderator:
mimi huwa nalipia hicho kifurushi cha 17,000 inamaana hii ofa itanihusu au kuna namna tofauti ya kununua hiki kifurushi ?
 
Wangefanya vizuri zaidi kama wangejumuisha chanel za Super sports kwa bei hiyo.
 
mimi huwa nalipia hicho kifurushi cha 17,000 inamaana hii ofa itanihusu au kuna namna tofauti ya kununua hiki kifurushi ?

swali kwako mkuu hua unaona channel ngapi za mpira i mean ligi ya Epl...na je kuna channel gan itaonesha big brother kwenye kifurushi hiko....nipe jibu nisije kufnya maamuzi yenye majuto Pumb
 
Last edited by a moderator:
31.jpg

MultiChoice Africa ina furaha kuwatangazia kuwa imezindua kifurushi kipya maalumu kwa watanzania. Kifurushi hiki kimetengenezwa mahususi kwa watanzania kikiwa na chaneli zaidi 65 za kitaifa na kimataifa zitakazotoa burudani pekee kwa familia za kitanzania.

Kifurushi hiki kipya cha Bomba kina chaneli nyingi nzuri ikiwemo chaneli iliyozinduliwa hivi karibuni ya Maisha Magic Swahili inayoonyesha filamu za kitanzania; chaneli ya Telemundo inayojulikana kwa michezo ya kuigiza ya kimapenzi ya Amerika ya Kusini pamoja na Nickelodeon na Disney Junior zinazoonyesha vipindi vya watoto.

Meneja Mkuu wa MultiChoice Tanzania, Peter Fauel, alisema kuwa kifurushi kipya cha Bomba kitagharimu kiasi cha TSh 17,000 tu kwa mwezi: " Uzinduzi wa kifurushi hiki cha Bomba ni jambo la furaha na msisimko sana kwetu, kuona kuwa sasa watanzania wanaweza kupata kifurushi kinachokidhi mahitaji yao.

Kila wakati, MultiChoice inafanya jitahada za kubuni namna ya kuwapa wateja wetu uwanja mpana wa burudani. Sasa, watanzania wameongezewa uwanja wa uchaguzi kwa bei iliyo chini na kiwango cha juu cha burudani ikiwemo filamu, makala, habari, vipindi vya watoto, muziki, vipindi vya dini na michezo."

Usikose ofa yetu ya uzinduzi huu - watakaojiunga watapata DStv ikiwemo gharama ya ufundi kwa TSh 99,000 tu kwa kipindi maalum. DStv Bomba pia itakuwa na chaneli za Africa Magic Epic Movies, Discovery World, CBS Action, CBS Reality na CBS Drama pamoja na Select Sport 1 na 2 kwa vipindi vizuri vya michezo. SuperSport Select na SuperSport Select 2 zitaonyesha ligi kuu ya Uingereza, Kombe la klabu bingwa Ulaya, Ligi Kuu ya Hispania, Ligi kuu ya Ujerumani pamoja na riadha na ngumi. SuperSport Blitz itawaletea habari zote za michezo. Kwa habari zaidi kuhusu burudani kwa ajili ya familia,

Kama hamna SS1-SS7, yaani EPL, hakifai. Tupa kule.
 
Ngoja nitafute mteja niuze azam tv.

Azam wape muda ndugu, bado wageni sana ila wanaonyesha mwelekeo mzuri. Mwanzoni nilinunua Azam kisha nikaanza kuwachukia, ila nilipokuja tulia nikakuta wana channel zinazonifit kabisa. Yaani kama wakiongeza CNN na EPL, bhaaaaaaaaas!! Napenda sana chanel 170, 171, 172 ,200,201, 202 movies, na 500-502 Documentaries, BBC , Aljezira, muziki. Nk, wanajitahidi, wape muda! Documentary channels wananikuna saaaana. Sijajua mieleka inaonyeshwaga juma ngapi na saa ngapi, ila nayo ipo! Ni burudani kwa bei nafuu.
 
Kuna za chini ya kapeti kuwa mkataba wa super sport na Dstv unakaribia kuisha na Azam. Tv ameshafanya mazungumzo na super sport ili kuingia mkataba

Nadhani dstv wameshaliona hilo ndo maana wanakuja na package ndogo ila is too late.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Mkuu tofautisha supersport from the rest.. Wanaposema supersport wanamaanisha channel zao za michezo only.. Iko chini ya mwamvuli mmoja wa DSTV.. Ina maana kwa kifurushi hicho cha TShs. 17,500/= huwezi kuona channel yeyote ya supersport..

Sijaelewa swali la DISOLN vizuri ila kama anamaanisha channel za supersport nitakuwa nimemjibu hapo juu..

Basi hawajasolve issue bado, nilidhani angalau boli litakuwapo, yaani EPL. Wangekuwa wamenipa raha hapo. Ningejipinda nami.
 
Last edited by a moderator:
Kuna za chini ya kapeti kuwa mkataba wa super sport na Dstv unakaribia kuisha na Azam. Tv ameshafanya mazungumzo na super sport ili kuingia mkataba

Nadhani dstv wameshaliona hilo ndo maana wanakuja na package ndogo ila is too late.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

Naomba hii habari iwe ya kweli ndugu! Please! Ata wakitugonga kwa 30000-40000 kwa mwezi ila kuna EPL, mambo yatakuwa si mabaya!! Nitakula nyasi kwa miezi kadhaa!
 
Back
Top Bottom