Dstv wamelewa sifa, kwa sasa wanaboa...

Dstv wamelewa sifa, kwa sasa wanaboa...

haki ya kuonyesha EPL mzigo wake sio mchezo,DSTV wana haki yakurusha EPL south,namibia zambia,zimbabwe botswana,tanzania,uganda,kenya,rwanda,ghana,nigeria etc.

kwa maana hiyo ukinunua haki ya kuonyesha EPL lazima uonyeshe kwenye nchi zote hizo.

kama unakumbukumbu miaka kama 10 iliyopita ilijitokeza kampuni moja ilikuwa inaitwa GTV ikanunua haki za kurusha EPL kwa 60% na DSTV 40% at last GTV wakachemsha wakawa wanapata hasara wakauza haki yao ya kurusha EPL kwa DSTV

kwa hiyo mkuu kununua haki za kuonyesha
lazima uwe bepari mkubwa.sidhani hapa tanzania kuna bepari wa ku compet na DSTV(south africa)
Mkuu nilifanya kazi Gtv aisee hii kampuni ilinifanya nikahama mji
Hadi leo Nina decoder zao
 
Sihitaji kumshawishi mtu, lakini Startimes ni bora sana kulinganisha na DStv. Najua kuna hoja ya Premier league inayooneshwa DStv, lakini Bundesliga na serial A zioneshwazo Startimes huingiza timu mfululizo fainali ya UEFA kuliko hiyo ligi pendwa.
Mkuu,hta zikichukua uefa kila mwaka,ladha ya epl bhana iache tu,epl ina utamu wake
 
Hajakwambia kuwa hamna local channel hata moja
Essentially Canal+ ni kwa ajili ya Mauritius(ndo maana wanarusha kwa kifaransa) isipokuwa beams zinafika hadi maeneo fulani ya Tz. Sasa local channels zitahusikaje hapo?
 
Mwanzoni walianza kutokuonesha Ngao ya hisani, baadae wakaja wakasema hawataonesha Europa League, Na sasa wamenitumia sms kuwa Chaneli pendwa SS8 namba 208 inayoonesha Serie A itahamia kwenye kifurushi cha 39,000 kutoka kwenye kifurushi cha 19,000 kuanzia Januari 15.

Hii yote inakuja mara baada ya kutangaza kuwa hawataonyesha michuano mikongwe ulimwenguni ya Kombe la F.A kwa msimu huu. Nafikiri kuna tatizo sehemu, pengine Dstv wameshalewa sifa, maana Europa League kwa upande wa South Africa hao Dstv wanaonyesha michuano hiyo au sisi Watanzania wametuchoka?

Laiti kisimbuzi cha Canal + kingekuwa kinatangaza kwa lugha ya kiingereza nafikiri sisi walevi wa mpira tungekimbilia huko, maana gharama zake ni nafuu sana.

Mlio karibu na Dstv wafikishieni habari, sisi kama wateja pia tumeanza kuwachoka kama wao walivyotuchoka.

Sikukuu njema wakuu!
Hiyo SMS ya kuhamisha SS8 kwenda kifurushi cha family naisubiri kwa hamu.
BTW, hawa jamaa wamelewa sana sifa, na ukosefu wa upinzani ni chanzo cha haya yote.
 
Mwenyewe nimetumiwa hiyo sms kuwa S8 channel namba 208 haitaonekana kwenye kifurushi cha tsh19000/= kuanzia 15 January 19

Hili tatizo la gharama za vifurushi ni Africa nzima au hapa TANZANIA? Maana kuna rafiki yangu anaishi Zambia anasema gharama za dstv ni affordable sana tofauti na hapa
Nahisi ni Tanzania na nchi nyingine ambazo hawa jamaa hawana ubia nazo (namaanisha hawaonyeshi ligi ya nchi hizo)

Zambia DSTV wanaonyesha ligi yao kama ilivyo kwa Nigeria. Nahisi kutakuwa na unafuu
 
Nimeona mahali kwamba mkataba wa kuonesha ligi ya England kwa dstv, ambao ulikuwa unaisha mwaka 2019, so far wamesign mkaba mwingine tena ambao unawapa haki ya kuendelea kuonesha ligi hiyo mpaka mwaka 2022, wao wamepata haki hiyo wakati, kwese wao wamepewa haki ya kuonesha mechi moja kila jumamosi, na tena mechi ambayo siyo kubwa.
Kwa hiyo pamoja na machungu ambayo tunayapata kutoka kwa dstv, bado tuna safari ndefu saana ya kuachana nao maana wao ndo wamekuwa na haki ya kuonesha ligi hiyo toka 1992.
Mkuu avatar yako ni matata... Teh tehe teheee
 
Kinacho Fanya dstv ionekane ipo ni kwa sababu Tanzania us Dora ipo juu sana na wao vifurushi vyao wana vithaminisha kwa Dora
Siku Dora ikishuka dstv itakuwa bwelele
 
Hivi tume ya ushindani na Tcra hawawezi kuingilia kati, ikiwezakana waambiwe kupunguza bei na kuirudida ss8 kwa kifurushi cha bomba, la sivyo wafungiwe ndani na nje ya nchi.
Mkuu SS8 kurudishwa kwenye kifurushi cha bomba haiwezi kuwa kigezo pekee cha kuwabana hawa jamaa na udhalimu wao, maana wanaweza wakaiacha hiyo channel lakini wakaondoa vipindi vya maana hasa mpira, mieleka na riadha wakabakiza mambo ya ovyo tu.

Nadhani wanatakiwa kuwabana kuhusu gharama na content za channel zao, kwanza hata kabla ya kuzuiwa local channels wao walikuwa na chache sana unlike visimbuzi vingine.
 
Mkuu najua ni gharama saana, lakini unakuta kama hao sky wao wananunua na kuuza kwa wengine kama ambavo dstv wamenunua kwa sky, kwa ajili ya kutukamua watu wa africa, kwa hiyo Azam ananunua kwa sky ili atuuzie hapa bongo, sema Azam mtandao wao sio mpana kama dstv, na nadhani itakuwa hailipi kwa coverage yao so far.
Nadhani Dstv amepewa tenda hiyo kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara.Kwa hiyo hakuna kampuni nje na Dstv/supersport inaweza kurusha bila kukubaliana na dstv.
Pia usisahau huenda maadiliko ya sera za nchi ndio yanapekea wao kubadili vifurushi.mfano wakiondoa ss8 kuna channel ya movie au ya muziki wataishusha huku kwenye 19 elfu kufidia.
kwa hiyo wao wanangalia upepo ulivyo.Mwanzo walikuwa hawaoneshi serie A baadae wakaanza.so naona ni upepo tu.
 
Vipi kuhuau receiver za Bein sports. Kuna mwenye uelewa juu ya hili jaman? Naskia ziko poa sana.
 
Ipo siku TV zitakuwa kama App mfano YouTube yani unanunua Data unaangalia unachotaka (Live streaming)
 
Mwanzoni walianza kutokuonesha Ngao ya hisani, baadae wakaja wakasema hawataonesha Europa League, Na sasa wamenitumia sms kuwa Chaneli pendwa SS8 namba 208 inayoonesha Serie A itahamia kwenye kifurushi cha 39,000 kutoka kwenye kifurushi cha 19,000 kuanzia Januari 15.

Hii yote inakuja mara baada ya kutangaza kuwa hawataonyesha michuano mikongwe ulimwenguni ya Kombe la F.A kwa msimu huu. Nafikiri kuna tatizo sehemu, pengine Dstv wameshalewa sifa, maana Europa League kwa upande wa South Africa hao Dstv wanaonyesha michuano hiyo au sisi Watanzania wametuchoka?

Laiti kisimbuzi cha Canal + kingekuwa kinatangaza kwa lugha ya kiingereza nafikiri sisi walevi wa mpira tungekimbilia huko, maana gharama zake ni nafuu sana.

Mlio karibu na Dstv wafikishieni habari, sisi kama wateja pia tumeanza kuwachoka kama wao walivyotuchoka.

Sikukuu njema wakuu!

dalili ya fastjet kwa DSTV
 
Mkuu najua ni gharama saana, lakini unakuta kama hao sky wao wananunua na kuuza kwa wengine kama ambavo dstv wamenunua kwa sky, kwa ajili ya kutukamua watu wa africa, kwa hiyo Azam ananunua kwa sky ili atuuzie hapa bongo, sema Azam mtandao wao sio mpana kama dstv, na nadhani itakuwa hailipi kwa coverage yao so far.
Azam kwa sasa wapo mpaka Zimbabwe,nchi kama 12 hivi
 
Kama nilivyowachoka azam,nimeshusha ungo la azam nimetupa stoo mpaka watakapokubaliana kuonyesha ITV na cheneli zingine

Back
Top Bottom