Dstv wamelewa sifa, kwa sasa wanaboa...

Dstv wamelewa sifa, kwa sasa wanaboa...

Hivi tume ya ushindani na Tcra hawawezi kuingilia kati, ikiwezakana waambiwe kupunguza bei na kuirudida ss8 kwa kifurushi cha bomba, la sivyo wafungiwe ndani na nje ya nchi.
K/koo bei ya kingamuzi ni 130,000/ kwa mwezi ni 40,000 unaangalia Ligue 1, EPL, Europa, Uefa ila changamoto ni matangazo ya mpira ni Kifaransa.
Mzee mpira si unaonekana lakin, au unamanisha kila chanel zina rugha ya kifaransa.
Mm naona bora hao.
 
Sihitaji kumshawishi mtu, lakini Startimes ni bora sana kulinganisha na DStv. Najua kuna hoja ya Premier league inayooneshwa DStv, lakini Bundesliga na serial A zioneshwazo Startimes huingiza timu mfululizo fainali ya UEFA kuliko hiyo ligi pendwa.
Startimes wana UEFA???
 
Mzee mpira si unaonekana lakin, au unamanisha kila chanel zina rugha ya kifaransa.
Mm naona bora hao.
kuna bar huku tabata wanatumia hiyo canal sport,tunaangalia mpira bila shida..alftime kila mtu na mambo yake gozi likirudi uwanjani fresh magori yakifungwa tunashangilia kama kawa...advantage nyingine tunajifunza kifaransa pia mdogomdogo..merci buku!!
 
Mwenyewe nimetumiwa hiyo sms kuwa S8 channel namba 208 haitaonekana kwenye kifurushi cha tsh19000/= kuanzia 15 January 19

Hili tatizo la gharama za vifurushi ni Africa nzima au hapa TANZANIA? Maana kuna rafiki yangu anaishi Zambia anasema gharama za dstv ni affordable sana tofauti na hapa
Hapa kwetu tumezoea kupigwa tena watu wanaona sifa kununua bidhaa kwa bei ya juu ili tu waonekane wapo wachache wenye hiyo kitu (siku akili za ubinafsi zitakapotutoka vichwani uwe una hela ama la ndipo DSTV itakuja kuonekana affordable hata kwa Tanzania)
 
Mimi kwenye category ya movie, naona Startimes ana composition nzuri ya Nigeria na Ghana movies eg Ebonylife, Iroko 1,2&3,AM na za East Africa, pia reality movies na animal movies. Ila haya ni maoni yangu yanayotegemea taste yangu. Nakushauri Google channel list from their websites for self comparison.
 
F A wamenyanganwa rights Azam kabeba
Europe pia walinyanganwa na Startimes

Ni maswala ya ushindani tu
 
K/koo bei ya kingamuzi ni 130,000/ kwa mwezi ni 40,000 unaangalia Ligue 1, EPL, Europa, Uefa ila changamoto ni matangazo ya mpira ni Kifaransa.
hiyo 4o,000/= ni package moja tu au kuna nyingine ya chini zaidi ya hapo?
 
Pale Azam pana Tido Mhando ambaye amefanya kazi huko London tena kwenye chombo kikubwa tu, BBC na Hilary Charles kwenye kitengo cha michezo pale BBC, sijui wanashindwaje kuwaadabisha hawa dstv, yaani kama Azam anaanza kuonesha ligi ya England mi hata leo nahama dstv, wameshanichosha.
 
Back
Top Bottom