Area 56
JF-Expert Member
- Dec 8, 2015
- 1,555
- 4,085
Mwanzoni walianza kutokuonesha Ngao ya hisani, baadae wakaja wakasema hawataonesha Europa League, Na sasa wamenitumia sms kuwa Chaneli pendwa SS8 namba 208 inayoonesha Serie A itahamia kwenye kifurushi cha 39,000 kutoka kwenye kifurushi cha 19,000 kuanzia Januari 15.
Hii yote inakuja mara baada ya kutangaza kuwa hawataonyesha michuano mikongwe ulimwenguni ya Kombe la F.A kwa msimu huu. Nafikiri kuna tatizo sehemu, pengine Dstv wameshalewa sifa, maana Europa League kwa upande wa South Africa hao Dstv wanaonyesha michuano hiyo au sisi Watanzania wametuchoka?
Laiti kisimbuzi cha Canal + kingekuwa kinatangaza kwa lugha ya kiingereza nafikiri sisi walevi wa mpira tungekimbilia huko, maana gharama zake ni nafuu sana.
Mlio karibu na Dstv wafikishieni habari, sisi kama wateja pia tumeanza kuwachoka kama wao walivyotuchoka.
Sikukuu njema wakuu!