DSTV Sharing

DSTV Sharing

Paul S.S

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2009
Posts
6,408
Reaction score
3,269
Wadau wa teknolojia naomba ushauri wenu kwa hili kama lina wezekana
Jirani yetu ana tumia DSTV na anadai gharama kwa mwezi zimemzidi uzito, so ametuita majirani zake wawili akatuomba kama tupo interested atatuunganishia cable kutoka kwenye king'amuzi chake tupate mambo kwa minajili ya kusaidiana wakati wa malipo ya mwezi.

Changamoto inayo tukabili ni je inawezekana labda kufanya namna yoyote pengine hata kununua kifaa fulani kitakacho weza kufanya kila mmoja aka control chaneli atakayo kwa wakati wake na si yeye akiweka kipindi fulani basi wote mnalazimika kuangalia hicho
Huwa naona hii maneno kwenye mahotel, kila tv chumbani unabadili chaneli kama kawaida
Nawasilisha
 
Wakuu hakuna mwenye idea na hii maneno?
 
mi navyojua ipo ile ya tv mbili lkn yakuvuta naona mmoja ata controll na wote mutakuwa munaangalia anocho angalia.

lkn ya tv mbili sioni kama inazidi gharama naona 150k.inakuwa risiva mmoja lkn ways kwa tv mbili na remote mbili.
 
NGOJA DSTV WENYEWE WATAKUELEKEZA BRO,si ahame tu mbona footbal lipo hata Star Times kwa buku 9 tu
 
Wadau wa teknolojia naomba ushauri wenu kwa hili kama lina wezekana
Jirani yetu ana tumia DSTV na anadai gharama kwa mwezi zimemzidi uzito, so ametuita majirani zake wawili akatuomba kama tupo interested atatuunganishia cable kutoka kwenye king'amuzi chake tupate mambo kwa minajili ya kusaidiana wakati wa malipo ya mwezi.

Changamoto inayo tukabili ni je inawezekana labda kufanya namna yoyote pengine hata kununua kifaa fulani kitakacho weza kufanya kila mmoja aka control chaneli atakayo kwa wakati wake na si yeye akiweka kipindi fulani basi wote mnalazimika kuangalia hicho
Huwa naona hii maneno kwenye mahotel, kila tv chumbani unabadili chaneli kama kawaida
Nawasilisha

Mkuu kwa sasa haiwezekani kwa sababu wamezibiti kadi haiwezi kufanya kazi tofauti na dekoda yake
 
Inawezekana pale tu kila mtu atakaponunua decoder yake..kuna kitu kinaitwa extraview yaan tv mbili znatumia malipo ya card moja na dish moja ila decorder lazima ziwe tofauti ili kila mtu aweze kuona mambo yake kwa wakat wake..ukiwapata hawa mawakala wa dstv wenyewe wapo wanaofaham kuunga hivyo au fungua page yao search hiyo extraview kwa maelezo zaidi..yupo mtu namfaham anatumia hivyo tv ya sitting room na bedroom kwa malipo ya card moja..
 
Au kama vipi mtafute fundi aunge direct ila ndo itakuwa mnaona kile anachoona mwenye decoder tu..
 
Thanx kwa maoni yenu.
Inaonekana itakuwa ngumu, ngoja kwanza tukomae na startimes zetu kwa sasa wakati michakato ya kuwaona hao wataalamu ikiendelea
 
kuna decorder inaitwa dual view(PVR) itawapa contrlol users wawili
 
Itabidi wote mnunue decoder zinazoweza kufanya ExtraView, itabidi waya 3 zitoke dish hadi kwenye kila decoder, kisha decoder "master" iunganishwe na decoder zengine "slave" kwa kutumia waya mwingine, official limit ya waya huu ni meter 50, waya huu ukipoteza mawasiliano decoder "slave" zinaacha kuonyesha picha.

Na kuna fee inaongezeka kwa mwezi kama unataka ExtraView.
 
Dah.......... zoezi gumu sana hili mkuu, maana inabidi tununue tena decoder zingine,
Tulidhani kwa hii aliyonayo inawezekana, ngoja tukome na startimes tu, na mshkaji itabidi augulie maumivu tu

Inawezekana. Kuna kifaa ( jina limenitoka) kinatumiwa na wale wanafanya biashara ya cable TV au kwenye mahoteli
 
Hii kitu inawezekana ila inabidi muwe na dikoda 2. Ila dishi ni moja tu..pia mtashare watu wawili na sio watatu..primary dicoder pia inatakiwa iwe on ili dikoda ya pili iweze kupata data.
 
Inawezekana. Kuna kifaa ( jina limenitoka) kinatumiwa na wale wanafanya biashara ya cable TV au kwenye mahoteli
Mkuu swali ni je kinapatikana mitaani au lazima ukipate kwa wao wenyewe DSTV?
Hata mimi nimeona mikoani jamaa wa cable tv na kwenye mahoteli, tena unabadili channel kupitia TV na si decorder.
Hata hivyo dhumuni letu ilikuwa ni kujaribu wote tupate chaneli na kuzicontrol wenyewe bila kuwashirikisha DSTV kujaribu kupunguza gharama
Kwa maelezo ya wadau hapo juu, inaonekana inawezekana lakini lazima urudi DSTV wakuuzie vingamuzi vingine na bei inakuwa kubwa zaidi kwa huduma hiyo ambapo tutakuwa hatuja save kitu

Mikoani kama Dodoma Dstv bill ni shs 10,000 kwa mwezi.
 
Back
Top Bottom