DSTV Pwaaa: Kuongeza bei za Bundle mara kwa mara mtapoteza wateja

DSTV Pwaaa: Kuongeza bei za Bundle mara kwa mara mtapoteza wateja

Yaani DSTV soon mtatokomea, mambo ya kuongeza bei za bundle kwa mwaka sijui mara ngapi. Mtapoteza wateja..
Kile kifurushi cha bei ndogo sasa ni 18,500/, hivyo vingine sivipatii picha.

Ngonja nikajitafutie kingamuzi changu cha startimes nilichoweka uvunguni
Kweli mkuu mimi mwanzo nilikuwa nalipa cha 85,000/= wakapamdisha hadi 92,000/= na sasa ni 113,000/= lakini mimi kwa ufahamu wangu ni kuwa Dstv hawajaongeza bei isipokuwa shilingi yetu ndio nimeshuka thamani sana sasa hivi inakaribia kuwa sh 2,000.= kwa dola moja. Ilivyo ni kuwa wao bei zao ziko katika mfumo wa dola lakini huwa wanazibadili kuwa za kiTZ sasa ya TZ inaposhuka thamani lazima utaona kama bei imeongezeka kumbe sivyo. Kama pesa yetu ingekuwa kuna wakati huwa inaongezeka thamani ungeweza kuona bei ikipungua. Vivyo hivyo hata kwenye mafuta. Unaweza kuona kimataifa bei imeshuka lakini ukashangaa huku kwetu bei haipungui sana au inapanda kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi. Na hii nisikutishe, itaendelea kupanda kwakuwa shilingi ninaendelea kushuka thamani
 
tusisahau wanakimbizana na dola, waweza kulaumu dobi kumbe kaniki ndio rangi yake
 
Hakuna haja ya kubet mkuu..na haiwezi kuwa rahisi kiasi hicho..Look here,those people know what they are doing.
Biashara yao ni kwenye Sports,particularly,football..na hasa of the so called famous leagues..Kupata haki ya kuonesha ligi kama epl ni gharama kubwa..lkn pia kuna makampuni mengine makubwa duniani yanacontend kufanya biashara hiyo..

Kwa mfano,dstv wana haki ya kufanya biashara hiyo eneo la kusini mwa jangwa la sahara..ni wao pekee ndio wenye umiliki..kwa maana nyingine,hakuna kampuni yoyote yenye ruhusa ya kufanya biashara hiyo katika kipindi hiki ambacho bado mkataba wao haujaisha muda wake.

Kwa kawaida,baada ya muda wa kibali kuisha,makampuni mengi tu huomba kuonesha ligi hizo..kama ambavyo zabuni za kawaida zinvyogombewa na makampuni mbalimbali..ila ni moja tu ndiyo hushinda na kupewa haki ya kufanya biashara..sasa kwa sasa ni dstv pekee ndio ina haki hiyo..

Kwa mfano kampuni ya beIN Sport(iliyokuwa aljazeera sports) inafanya biashara kama hii eneo la MENA(middle east & northern africa),haina ruhusa ya kufanya biashara yake eneo la kusini kwa jangwa la sahara..ingawa matangazo yao yanapatikana hadi nchi kadhaa zilizo kusini mwa sahara,lkn wao officially hawatoi services kama vile kuuza decoder zao au accounts..kwa kuwa kufanya hivyo ni kinyume cha mikataba yao.

Kama nilivyosema hapo juu,ni jambo ambalo haliwezekani kudhania kwamba siku moja Azam itatoa ushindani mkubwa kwa dstv..na hapa namaanisha ushindani kwamba,watu wakimbilie kujiunga na azam ili kupata kile kitu kilichowasukuma kujiunga na dstv!! Like,kupata sports channels zenye kuonesha epl,la liga,bundes league,uefa,etc kwa mechi zote..it really,looks unlikely kwa kweli.

Kitu wanachoweza kufanya ni kununua baadhi ya mechi kama walivyokuwa wanafanya TING na of course, hata TBC1 ya Tido!! Lakini hii kwa azam haiwezi kuwa na maslahi kwao,hasa kibiashara..na kama wakiamua kuonesha mechi nyingi,nao watapandisha bei zao ili kukidhi gharama za uendeshaji..halafu kesho na kesho kutwa tutakuta hapa hapa kuwatupia lawama na kuwaita majina mengi mabaya!!

Azam inaweza kuleta ushindani mkubwa kwa makampuni ya huku kwetu na labda nchi za jirani ila si kwa dstv..So,ni vema tukakumbushana pia kwamba,dstv will contend na makampuni kama vile beIN Sports,Sky,Fox,BBC,etc na Azam will contend na akina Zuku,Startimes na blaa..blaa..blaa..

Ndugu yangu mrimi sikubaliani na wewe kwa kiasi furani kwamba azam hataweza kuomba haki ya kuonyesha ligi kubwa za ulaya hiyo si kweli....hata huko uingereza ambako sky ana dominate kuna haki amezipoteza kwa BT.kuna kipindi huko nigeria alipoteza kwa HITV..Hilo linawezekana na anachoweza kufanya azam ni ku tender kuonyesha tanzania au afrika mashariki....na muda si mrefu dstvatapoteza haki za kuonyesha ligi kubwa kwa nchi zinazoongea kireno maana ZAP yupo kasi kule.its a matter of time.
 
Gharama za Dstv, inflation or no inflation ziko juu sana. Mahali ambako haki za walaji (Consumers 'Rights) zinalindwa hali ni tofauti. Huku kwetu kwa maskini ndipo jamaa wanapopigia mkwanja. TCRA ndio chombo ambacho cha kudhibiti huduma zote za mawasiliano. Pia, kwa niaba yetu kuna kitu kinaitwa (Consumers' Consultative Council) ambayo inapaswa kuhakikisha maslahi yetu yanalindwa. Tatizo: Mamlaka za Udhibiti na viongozi wetu wanapata "complimentary" au "Concessionary rates". Mengine hayawahusu. Watoa huduma wameteka mamlaka za udhibiti "regulatory capture". Period. Bila kuwepo ushindani uwepo wa soko huria linaloenda kiholela tusitegemee ahueni yoyote!!!
 
watu wanaaka asubuhi wanajipandishia wanavyotaka...ngonja bwana Azam a
 
Ndugu yangu mrimi sikubaliani na wewe kwa kiasi furani kwamba azam hataweza kuomba haki ya kuonyesha ligi kubwa za ulaya hiyo si kweli....hata huko uingereza ambako sky ana dominate kuna haki amezipoteza kwa BT.kuna kipindi huko nigeria alipoteza kwa HITV..Hilo linawezekana na anachoweza kufanya azam ni ku tender kuonyesha tanzania au afrika mashariki....na muda si mrefu dstvatapoteza haki za kuonyesha ligi kubwa kwa nchi zinazoongea kireno maana ZAP yupo kasi kule.its a matter of time.

ndio tuombe hilo Azam akipata hili deal dstv ataandika maumivu...maana wanachofanya ni ukandamizaji
 
Kweli mkuu mimi mwanzo nilikuwa nalipa cha 85,000/= wakapamdisha hadi 92,000/= na sasa ni 113,000/= lakini mimi kwa ufahamu wangu ni kuwa Dstv hawajaongeza bei isipokuwa shilingi yetu ndio nimeshuka thamani sana sasa hivi inakaribia kuwa sh 2,000.= kwa dola moja. Ilivyo ni kuwa wao bei zao ziko katika mfumo wa dola lakini huwa wanazibadili kuwa za kiTZ sasa ya TZ inaposhuka thamani lazima utaona kama bei imeongezeka kumbe sivyo. Kama pesa yetu ingekuwa kuna wakati huwa inaongezeka thamani ungeweza kuona bei ikipungua. Vivyo hivyo hata kwenye mafuta. Unaweza kuona kimataifa bei imeshuka lakini ukashangaa huku kwetu bei haipungui sana au inapanda kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi. Na hii nisikutishe, itaendelea kupanda kwakuwa shilingi ninaendelea kushuka thamani

basi tunakazii kubwa sana na itafikia kipind tutakuwa hauangalii tena TV....maana salary iko palepale
 
Kifurushi cha compact plus kilichokuwa 95,000 sasa hivi kinakuwa 110,000. Ila siwalaumu si mmeona shilingi inavyozidi kuanguka lazima wapandishe maana bei zao zinatokana na exchange rate.
 
Nyie wengine mnalalamika tu kwnza hamjawajua vizuri dstv ukilipa kabla ya tarehe yako yakulipia mwezi unaofwatia unalipia hela ndogo kuliko ada ya mwezi. Mfano mimi mwezi wa tatu nililipa Sh 66000 kwa compact tarehe 22 na salio langu lilokua linaisha tarehe 24 tarehe 22 ya mwezi wa 4 nililetewa msg kwmba nilipe Sh49000 kabla ya tarehe 24 na bahati nzuri nilikua ndio nimetoka tu kulipa Sh66000 kwhiyo kwa mwezi wa 7 nitaletewa msg yakulipa elfu ishirini na kitu. Hawa watu sio wabaya kama unalipia mapema ukilipa mapema ada inapungua. Hua wanasema ukilipa ada yako hata week moja kabla ya tarehe ya makato salio lote kwnye account yako inaamishiwa kwnye mwezi unaofwata na ni kwli.
 
basi tunakazii kubwa sana na itafikia kipind tutakuwa hauangalii tena TV....maana salary iko palepale
Hilo ndillo tatizo kubwa unapanta mshahara ambao thamani ya shilingi inaposhuka wenyewe una baki palepale labda ungekuwa unathaminishwa kwa dola ingekuwa afadhali
 
Unaota? Hao wachina wako walishapigwa ngwara kitambo,....nao wanmechangia Dstv kupandisha gharama hasa kwani makaburu walitumia pesa nyingi kununua makufuri na kujenga mageti.

Mbona kuna akaunti zime survive bado zinachakachua server za mkaburu kupitia qsat
 
Mbona kuna akaunti zime survive bado zinachakachua server za mkaburu kupitia qsat
Hata kwenye PM nitajie account iliyosurvive hii kumbakumba ya dstv nitakulipia miezi 3 bure hakika....:yo:
Kuna ndugu yangu yupo Algeria nataka aninunulie decoder ya Bein nione kama nitaookoa hela za kulipa kodi ya nyumba maana hawa makaburu wankula mshahara mzima,
 
Leo gemu (Arsenal vs Chelsea ) naliangalizia online...! tena nashanga leo hamna kustak kama zamani...sina hakika kama DSTV watanipata tena. Maana mpira ndiyo ilikuwa hitaji langu huko.
 
Jamani sio kila mtu awe na dstv ukitaka uzuri kubali kulipia zaidi.
 
Tatizo siyo DSTV. Tatizo ni shilingj yetu kuzidi kuporomoka mbele ya dola ya Kimarekani. Hali ya mporomoko ikiendelea hivi, kifurushi cha bei ya chini kitafika laki.
 
Kenya kifurushi hicho hicho ni KSH 8500.

Sh 8500/= ya Kenya ni sawa na shilingi 168000/= ya Tanzania. Mnawalaumu DSTV bure. Tatizo siyo wao. Tatizo ni shilingi ya Tanzania kuporomoka kila siku.
 
Back
Top Bottom