DSTV Pwaaa: Kuongeza bei za Bundle mara kwa mara mtapoteza wateja

DSTV Pwaaa: Kuongeza bei za Bundle mara kwa mara mtapoteza wateja

mambo yote azam tv na leo nimeona mechi ya simba km kawaida
 
Tamu ni QSat bandle la 2000 kwenye line ya Tigo au mtandao wowote, tosha mwezi mzima. Channel zotee za DSTV zinapatikana[/QUOTE}Kiongozi wanapatikana wapi hawa niwapelekee pesa jumatatu ? Thanks in advance for your tireless efforts to make my life a little bit easier.

Utatapeliwa wewe hivyo vilifanya kazi zamani kwa sasa havipigi mzigo .
 
Watanzania wengi wanaongea sana. Kama huwezi lipa Premium hamia Azam nako kuna mpira. Acha wanaoweza waendelee lipa
 
yaani DSTV soon mtatokomea.mambo ya kuongeza bei za bundle kwa mwaka sijui mara ngapi..mtapoteza wateja..
kile kifurushi cha bei ndogo sasa ni 18,500/
hivyo vingine sivipatii picha.
ngonja nikajitafutie kingamuzi changu cha startimes nilichoweka uvunguni

18,500 34,000 56,000 135,000 148,000 chagua kilicho bora.
 
The same.... Bei kuubwa halaf sasa umeme ukikatika ukiwaka lazima decoder ifanye scanning km dk 5..inakera sana


Kwa technology ya DStv sijui kwa nini receivers zao zina boot mda mrefu hivi. 5 mins just booting/loading, its sick kwa kweli.
DStv hana mshindani kwa sasa, hasa katika sports, ndio maana yupo huru kuweka bei ya vifurushi, huku akijua watz tunapenda mpira...kwa hiyo tutanunua tu.
Tunachotakiwa ni kuwa na ushindani, I bet in five yrs azam atakuwa mahali ambapo anaweza kuleta ushindani kwa hawa jamaa.
Kingine kama mtu ana uwezo mdogo, aendelee kutumia vingamuzi vya bei rahisi. Basi.
 
Ttz sio dola walipandisha gharama. Subirini bei elekezi baada ya dola kupanda kama c 200,000
 
Unaota? Hao wachina wako walishapigwa ngwara kitambo,....nao wanmechangia Dstv kupandisha gharama hasa kwani makaburu walitumia pesa nyingi kununua makufuri na kujenga mageti.

It depends na utaalam wako unaishia wapi! Kama your account ni CC CAM for the time being hamna kitu. Lakini AVATAR CAM ni mwendo mdundo. It's a long story, let's the intelligent have DSTV FOR FREE he he he
 
bora premier league imalizike tuweke pembeni kidogo labda ligi ikianza tena augst dola itashuka maana ni majanga kifurushi toka 92000 hadi 113000
 
Mkuu inakuaje hiyo, tupe maujuzi ya jinsi ya kuipata kwenye masmartphone

Asikudanganye mtu. Huko nako msiba. Account hazifanyi kazi. Utaibiwa mjini hapa. Nimenunua moja ya hivyo ving'amuzi nimetumia wiki mbili tu hakuna huduma wakati ilikuwa na account ya mwaka mzima.
 
Cyo Tu Dstv Muda Si Mrefu Bei Za Bidhaa Zote Tanzania Zitapanda Unga,vocha[vifurushi] Tayari Vimepanda Bei
 
Mimi nashauri wana jamvi tuzikubali hali zetu za maisha. Katika soko huru kila mtu anapanga bei kulingana na maslahi yake.

Pale ambapo hatuwezi kujikuna tuwaachie wenye kucha ndefu. Turidhike tu kama mtoa mada anavyorejea startimes ambayo ndo stahili yake.
Dstv ni premium ni kwa wenye uwezo tu, shukuru na ridhika na majaliwa uliyopewa na Mungu.
 
Back
Top Bottom