nyumbamungu
JF-Expert Member
- Mar 3, 2017
- 997
- 828
Sasa ipo rasmi Septemba Mosi, 2019 mtashusha bei baadhi ya vifurushi, inatakiwa mfahamu sio wote wanaomiliki ving'amuzi vya Dstv ni wapenda kandanda, yupo mteja analipia kifurushi cha Bomba 19,000. lakini chaneli anayoipenda ni Nat Geo Wild #182 au Nickelodeon #305, Disney #309.
Punguzeni wingi wa chaneli kutoka 70+ hadi chaneli 50+ na bei muweke 10,000. Bila chaneli za michezo, endapo mteja atazitaka chaneli za michezo (Supersport ) itambidi aongeze 9,000. Watazameni washindani wenu kama Azam Tv (45+ch kwa 10,000.) StarTimes (33+ch kwa 11,000) wote hawaungi chaneli za michezo.
Kwa sasa hivi chaneli inayoongoza Tanzania kupendwa na watu wenye rika mbalimbali watoto hadi wakubwa tena inayotuhusu sisi Watanzania sio nyingine Maisha Magic Bongo #160, hapo ndio penye shida hata kama mtatoa ofa ya kulipia miezi sita, je baada ya hapo gharama za kifurushi ni rafiki?
Nina imani kama mtalijadili hili la wingi wa chaneli na ukubwa wa bei ya kifurushi 19,000. Mtaweza kuwashawishi hata wale ambao walinunua Dstv kwaajili ya Ofa, ilivyoisha ofa amekitelekeza, mkumbuke Azam Tv amepata leseni ya Chaneli za ndani na tayari amezirudisha Clouds TV, Chanel 10 na ITV, fanyeni maamuzi magumu kuweza kupata wateja wapya.
Nipo tayari kurekebishwa.