Nimeamua kuvunja kisimbuzi cha Azam kwa maana walivyotufanyia ni zaidi ya utapeli

mliverpool

JF-Expert Member
Jan 6, 2015
788
1,000
Brand ya Azam kubwa Sana kwa bidhaa nyingine kabla ya kuingia ktk biashara ya media,na brand Yao ilijenga taswira ya uaminifu i'la kwa Mara ya kwanza naona biashara hii mpya ya media /tv inaelekea kuvunja uaminifu wote ambao azam Kama Azam imejingea kwa wateja.

Azam tv ilivyotufanyia ktk maboresho Yao ya vifurushi Ni zaidi ya utapeli,Bora wangetumbia kuanzia mwanzo kuwa wanapndisha Bei za vifurushi kuliko kuleta ujanja ujanja wa kutoa chanel hi kupeleka huku hii kupeleka huku na kuwavuruga watwja.

Mimi kuanzia zamani nilikuwa natumia kifurushi Cha Azam plus Cha elf 23,humo nolikiwa naweza kuangalia chanel zote za michezo maana naangaliaga sana ESPN, Ukitoa Azam sports 1 na 2, pia chanel zote za watoto Kama baby tv n.k,chanel za wanyama,chanel za movies zote nilikuwa nazipata n.k

Juzi wamekuja na ujanja ujanja wao wkatudanganya wameshusha Bei za vifurushi Tena wakawa wanajinadi kabisa cha 23,000 Sasa hivi kitakuwa elf 20,nikajiroga kulipia elf 20,nilichokipata Ni zaidi ya Kero,chanel zote ninazoangaliaga hakuna,watoto chanel zao hakuna zolizopo sizo wanazozitaka wao,Sasa wameshusha Bei ipi?

Mbaya zaidi nikataka nifanye topup niende kifurushi Cha juu kumbe haiwezekani labda ulipie Tena upya,yaani elf 28 nyingine, ikabidi nivumilie mwez uishe,kifurushi kimeisha jana,watoto wanataka kuangalia tamthilia zao na mimi sina hela yote ya kulipia kwa mwezi nikasema nilipe walau kwa wiki nakuja kuangalia Bei ya wiki sijui wameset kwa margin ipi kubwa pasipo mfano kuliko ya mwezi, imagine kifurushi Cha elf 20 kwa mwezi,ambapo ukigawanya kwa wiki 4 unapata elf 5,Basi kwa sabahu za kibiashara wangeweza kiweka hata elf 6 ili au 7,kwa margin ya elf 2 siyo mbaya wao wamekuja kuweka elf 9 kwa wiki yaani ukizidisha Mara 4 unapata almost elf 36,mbona havina mahusiano?

Kwa kweli mm Kama niliyekuwa mteja nimekwazika Sana,na kwa kuwa Sina namna ya kufanya nyingine nimeamua kuvunjilia mbali kisimbuzi hiki,Hawa jamaa hapa nyumbani nawaambia kimeharibika,nifanye mpango niwanunulie walau DSTV wanaonekana hawana Mambo ya kiswahili,watazoea tamthilia na michezo ya kule Kama walivozoea Azam!
 

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
20,218
2,000
Wanangu walizoea cartoon za azam. Sasa wamehamia dstv baada ya kunambia baba azam wamefuta channel za cartoon. Sijajua kimewasibu kitu gani azam
 

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
20,218
2,000
Aiseee huu mwaka nao unataka kuelekea vibaya, kuna mtu hapa kachoma vyeti vyake vyote kuanzia msingi hadi chuo kikuu, wewe nawe umevunja kisimbuzi.

Huu mwaka utakuwa wa kuvunja na kuchoma tuu.
ila kuvunjwa king'amuzi siyo utatuzi angekiuza walau arejeshe nusu hasara.
 

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,194
2,000
Aiseee huu mwaka nao unataka kuelekea vibaya, kuna mtu hapa kachoma vyeti vyake vyote kuanzia msingi hadi chuo kikuu, wewe nawe umevunja kisimbuzi.

Huu mwaka utakuwa wa kuvunja na kuchoma tuu.
huyo wa kuchoma vyeti imekuaje Mkuu?
 

mkakeni

Member
Jan 20, 2013
60
125
Uko sahihi mkuu...nadhani wamesgatosheka pesa...acha tupungue. Mm pia nahama nirudie kingamuzi cha zamani..AZAM
 

Tony Laurent

JF-Expert Member
Jan 5, 2011
2,219
2,000
Kweli kabisa, hawa jamaa wamefanya mambo ya hovyo sana. Bora wangeacha bei zile zile za zamani. Walichotufanyia ni uhuni. Mwanangu anapenda chaneli ya katuni ya Baby TV, iliyokuwa inapatikana kwenye kifurushi cha elfu 23.

Sasa hivi wameihamishia kwenye kifurushi cha elfu 28. Sasa dogo anabaki analia tu akiwekewa katuni za cheneli za kifurushi cha elfu 20 hataki.
Ngoja nijaribu kuzitafuta katuni zile zinazoonyeshwa Baby TV kwa wauza CD za elfu 2 nimnunulie dogo, maana sina namna kwa sasa.
 

sajo

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
890
1,000
Miye Nina Mpango Wa Kuagiza Canal+,ila For The Time Being Acha Niende Startimes,familia Nzima Kwa Sasa Inaangalia Gangaa
Hicho canal+ kinauzwaje na kinaonesha channel za michezo kama ligi ya EPL?? Malipo yake kwa mwezi ni shilingi ngapi?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom