Drywall na ujenzi wa kisasa

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
500
Drywall ndio habari ya dunia kwa sasa hasa katika kuta za ndani. Drywall sio mbao ni madini ya gypsum yaliyofungwa ndani ya karatasi nzito.

Drywall ina faida zifuatazo:

- Ina unafuu wa bei.

- Inadhibiti hali ya hewa ndani ya nyumba.

- Ujenzi wake ni rahisi na wa haraka.

- Ni ngumu kuwaka moto. Karatasi la nje litaungua lakini madini ya gypsum yanaungua kwa moto wa joto kali sana.

-Muonekano wake ni mzuri na wa kupendeza.

-Inarahisisa kupitisha mabomba na waya za umeme

- Kuna zisizopitisha maji (waterproof)

-Haina uzito mkubwa sana hivyo haihitaji msingi na zege la nyumba nzito.

-Ni rahisi kuirepea, au hata kuitoa na kuweka nyingine.

Inaweza kufanywa iwe na uwezo wa kutopitisha sauti(soundproof)


 

Princemwalejr

JF-Expert Member
Nov 9, 2017
496
500
Mkuu, hasa huko kitaani kwetu wizi umezidi. Sasa kwa hii material, si itakuwa kama wanatafuta Mbege uchagani..

Mwizi itabidi akate mbao zote hizo akiwa tayari keshaingia ndani ya nyumba. Sasa nyumba za uswahilini zinakaa watu wangapi mpaka mwizi aachiwe avunje ukuta?
 

RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,620
2,000
Wabongo tuache kuingiza iphones kutoka nje tuanze kuleta vitu vya aina hii. Tena hii inaweza hata kutengenezwa Tanzania.
Mbona hii kitu ipo. Wengi wanafanya partitions kwenye ofisi, wanatumia mbao na gypsum boards tu. Ukipiga rangi hamna mtu anaejua kuwa huo si ukuta wa tofali.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom