Drogba

Wazungu ni wabaguzi sana Roy Keane alikuwa anafanya makosa makubwa kuliko hata hayo ya Drogba but siku zote Fergie alikuwa anamtetea,Cantona alienda kupigana na mashabiki still kocha alimtetea ndio maana hata Hidink anamtetea Drogba saanajua umuhimu wake
Mbona Ballack alitaka kumpiga refa? Yule refa nae anastahili kuadhibiwa yeye ndio kasababisha yote hayo
 
This is being blown out of proportions na media za wazungu tu, Drogba's aggression was only verbal wakati aggro la Ballack lilikuwa ni physical kabisa, he chased and touched the ref. repeatedly! but no one is saying anything about it!
Labda mimi ninachoweza kumlaumu Drog ni jinsi ambavyo reputation yake ya ku dive ilivyowa cost Chelsea, marefa wote wanajua jamaa ni drama queen so hata foul ikiwa genuine wanakuwa hawana uhakika kama jamaa amechezewa rafu au kajirusha tu, ndo mana incidents zake nyingi ndani ya box marefa hawatoi penati.
 
Drogba ni binadamu kama binadamu wengine hasira alizokuwa nazo ni haki yake maana yule refer alibowa sana maana amewakosedha Chelsea penati napi tena za wazi kabisa, me nahisi alihongwa na barcelona si bure. Inekuwa mie ningemuweka na vibao kabisa kama noma naiwe noma kawanganya chelsea tonge mdomoni.

wewe na Drogba, baba mmoja na mama mmoja.Possession-Barca 68% - Chelski 32%.Inakuwaje mnadefend in ur home ground????with Barca wakiwa na wachezaji 10 for nearly 35mins.Na nyie mmevuna mlichopanda.The best teams will be in Rome and those r -Man U Vs Barca.........innit.
 
Naona kuna watu wanachanganywa na magazeti ya uingereza hapa au ya wazungu kwa ujumla.... Kitendo alichokifanya Drogba kwa mtu yeyote anayejua suala la emotions ni kitu cha kawaida kabisa..hamna jambo la ajabu pale..na ni wachezaji wengi sana duniani ufanya vile coz football is a game of passion and emotions, nani anakumbuka game kati ya Barca na chelsea kipindi cha frank rijkaad, jinsi Frank rijkaad aliyokwenda kumvaa refa na kuanza kumfokea just like what drogba did,wakati mpira umekwisha? na reaction za media ilikuaje??? was it the same???the answer is no!!!! ulisikia porojo zozote kua UEFA watamfungia Rijkaad kama sasa kila chombo cha habari kinavyojaribu ku speculate- nakutaka kuifundisha UEFA kazi ya kufanya??? jibu ni hapana...so guys lazima muelewe hata mkikataa vipi hivi vitu mtavifumbia macho lakini hizi propaganda za rangi is there in EUROPE hata mkatae, the way waafrika tunavyo think kuhusu wazungu nitofauti kabisa na wao wanavyotuchukulia.........kuna mtu hapa ndio kalogwa kabisa eti anamtetea Ballack eti kua alimfokea refa wakati mpira ukiwa unaendelea.....eti yeye ni afadhali kuliko drogba..which for me ndio mbaya kabisa..na chakushangaza hata red card hakupewa!!! so sio mnavichukulia ki ushabiki hii vitu lakini sasa mpaka media zimeshaanza ku speculate na kua wasemaji wa chelsea..the sun wameshasema Drogba atafukuzwa Chelsea...wakati hamna hata officer yeyote kutoka chelsea aliyezungumzia suala hilo....Hawa watu they are not good for us hata kidogo...ukifanya vizuri watakupamba sana coz umewafanya kazi yao but kuna wengine wanasubiri ukosee tu waanze kukupiga jungu vibaya..upotee... I m sorry for Didier to be the Victim of this.....
 
Mbu uko biased kama magazeti ya UK. Nnachokiona hapa ni ubaguzi wa rangi, hamna cha ziada. ..
Wengine si wapenzi/mashabiki wa mpira wa miguu.
Alichofanya kaka DROGBA wanafanya wengi ila kwakuwa ni black from AFRICA imekuwa taabu kwelikweli....
Drobga alichofanya ni kumzongazonga mwamuzi na sidhani kama alimgusa. Kumzonga mwamuzi kwenye ile mechi karibu wachezaji wote wa Chelsea na Barca (kabla hawajapata bao) walifanya.

Mimi huwa siimbi kiitikio chanyimbo zinazoanzishwa na haya magazeti ya UK, huwa yanatengeneza mabifu na hii si mara ya kwanza. Na mara hii watampata huyu kwa sababu ya rangi yake.

...bandugu, Bob 'Mallya' aliimba;

"Emancipate yourselves from mental slavery;
None but ourselves can free our minds.
Have no fear for atomic energy,
'Cause none of them can stop the time..."

...Mnapoanza kusingizia matatizo ya mtu na Rascism, huo utakuwa ni mjadala mwingine. I've no more comment!

MBU unamchukia huyo jamaa sababu kila akicheza na Gunners anawapiga bao pamoja nayote aliyofanya jamaa anawabeba sana Chelsea

...:D kauli yako ina 'kaukweli' ndani yake, halafu huenda kesho J'2 asicheze kutokana na 'msongo' wa mawazo, ...tatizo Essien yupo, duh!
 
Waafrika bwana! kila kitu ubaguzi wa rangi!

Hivi kwenye mambo ya mpira wachezaji wakianza kuleta mambo ya "emotions" ni mechi ngapi zitaisha salama? tumeona mara nyingi tu timu mbalimbali zikinyimwa penalti au zingine zikipewa penalti hewa lakini wachezaji wanacontrol "emotions" zao. Chinga Drogba alitakiwa awe na uwezo wa kucontrol hizo "emotion" zake kama walivyofanya Cole, Check, Baleti na wenzao.

Sitaona ajabu wanaomtetea Grogba kwa kisingingizio cha "emotions" walimtetea pia Tyson alipoondoka na kipande cha sikio cha Evanda kwwa madai eti Tyson alikuwa na emitions baada ya refa kutomchukulia hatua yoyote Evanda kwa kumpiga "vichwa" Tyson.

Acheni kutetea ujinga wa mtu kwa kisingizio cha emotions na ubaguzi wa rangi.
 
This is being blown out of proportions na media za wazungu tu, Drogba's aggression was only verbal wakati aggro la Ballack lilikuwa ni physical kabisa, he chased and touched the ref. repeatedly! but no one is saying anything about it!
Labda mimi ninachoweza kumlaumu Drog ni jinsi ambavyo reputation yake ya ku dive ilivyowa cost Chelsea, marefa wote wanajua jamaa ni drama queen so hata foul ikiwa genuine wanakuwa hawana uhakika kama jamaa amechezewa rafu au kajirusha tu, ndo mana incidents zake nyingi ndani ya box marefa hawatoi penati.

...Drama Queen wakutosha!

kwa hakika pamoja na kwamba siishabikii Chelsea, lakini nilidhani naye (angebadilika) angekuwa among the Legends from this continent mfano; Abedi 'Ayew' Pele, Roger Milla, George Weah, etc!
 
he wazee
pole pole tuliza boli kiwanja kidogo

ukiangalia Didi amefanya makosa, tatizo unapokwenda mbio uwanjani pressure huwa inapanda ndio matatizo ya Didi hakuweza kujikatrol pia sisi tukifika kusifiwa tunaona tuko sawa sisi na wao lakini bado ukweli utabakia kuwa ni wageni
 
....hivi kulikuwa kuna haja kweli Drogba baada ya 'saka-saka' lile kugeukia Tv-Camera (knowing millions of people around the globe are watching) kuanza kusema hovyo? ...kama sio u-drama Queen ni nini?

Kilichomkamatisha Drogba ni ile 4-letter rant, aka f-word!;

" It is a Disgrace, it is a f****** Disgrace!" ...huh, Didier kwa mbwembwe naye,...si angetukana kikwao tu, nani angejua 'baule'? :D
 
Waafrika bwana! kila kitu ubaguzi wa rangi!

Hivi kwenye mambo ya mpira wachezaji wakianza kuleta mambo ya "emotions" ni mechi ngapi zitaisha salama? tumeona mara nyingi tu timu mbalimbali zikinyimwa penalti au zingine zikipewa penalti hewa lakini wachezaji wanacontrol "emotions" zao. Chinga Drogba alitakiwa awe na uwezo wa kucontrol hizo "emotion" zake kama walivyofanya Cole, Check, Baleti na wenzao.

Sitaona ajabu wanaomtetea Grogba kwa kisingingizio cha "emotions" walimtetea pia Tyson alipoondoka na kipande cha sikio cha Evanda kwwa madai eti Tyson alikuwa na emitions baada ya refa kutomchukulia hatua yoyote Evanda kwa kumpiga "vichwa" Tyson.

Acheni kutetea ujinga wa mtu kwa kisingizio cha emotions na ubaguzi wa rangi.

Ndugu yangu naona unakosea na unapotosha dhana yote kwa ujumla....hatusema kua drogba hajafanya makosa na sisi waafrika kama unavyosema hatulalamikii kua drogba anasingiziwa kwa kua hakufanya kosa..tunajaribu kusema ni kua hili jambo linakuzwa mnooo utafikirikiri ni dhambi ambayo binadamu yeyote hatakiwi afanye asilani ni kama kuua...suala la cole na wachezaji wengine wa chelsea kutofanya kama drogba alivyofanya ni suala lao wenyewe na jinsi walivyoyapokea matokeo..huwezi ukalinganisha feelings za watu kupokea jambo flani..wote tunaweza tukafiwa lakini mwengine akagalagala na kuzimia na wewe ukaishia kutoa machozi tu...imetuuma sote lakini suala la emotions hutofautiana katika kuguswa kwa mtu...na vibaya sana ukazihold izo emotions zako bila kuzitoa...provided kua hazitaleta madhara yeyote...alichofanya yeye ni kutoa uchungu alionao moyoni but akaweza kujicontol bila kurusha ngumi wala kufanya kitu kinachoweza kuleta madhara yeyote katika mwili wa yule refa.........ulitaka ajicontrol vipi zaidi ya pale???? yani asifanya lolote augulie tu moyoni sababu cole na lampad nao wamefanya hivyo??? no way!!!! angepata shida!!
 
...ulitaka ajicontrol vipi zaidi ya pale???? yani asifanya lolote augulie tu moyoni sababu cole na lampad nao wamefanya hivyo??? no way!!!! angepata shida!!

...mkuu wakunyuti, unakubali Cole na Lampard hawaku react kama Drogba, lakini wakati huo huo unakubaliana naye ('kujifanya') ku overreact, huoni hilo ni tatizo?
 
....hivi kulikuwa kuna haja kweli Drogba baada ya 'saka-saka' lile kugeukia Tv-Camera (knowing millions of people around the globe are watching) kuanza kusema hovyo? ...kama sio u-drama Queen ni nini?

Kilichomkamatisha Drogba ni ile 4-letter rant, aka f-word!;

" It is a Disgrace, it is a f****** Disgrace!" ...huh, Didier kwa mbwembwe naye,...si angetukana kikwao tu, nani angejua 'baule'? :D

F-word hata marefa wa UK premiership wanalitumia mkuu..mara nyingi mfano, (msinitoe macho washabiki wa) Man U wakipewa dubious penalties vs Spurs, akina Howard Webb wakiulizwa kulikoni majibu yao ndio huwaga :..F***-OFF !! lol
 
...ha ha haa... hasa Rooney! unakumbuka majuzi juzi alipokuwa substituted na SAF, acha akitwange ngumi kibendera cha kona,

...jamaa naye ana vihasira vya kijinga yule! Game imkatae yeye, hasira zake azimalizie kwenye chupa za maji na vibendera vya uwanja!
 
...mkuu wakunyuti, unakubali Cole na Lampard hawaku react kama Drogba, lakini wakati huo huo unakubaliana naye ('kujifanya') ku overreact, huoni hilo ni tatizo?[/QUOTE

Sikubaliani na unavyosema KUJIFANYA KU OVERREACT , na hapo ndipomnapokosea na ndio chanzo cha mambo yote..mnavyomuona uyu bwana ni mtu wa kufake fake tu na hayuko real.....mimi naamini alikua real na hakujifanya kuoverreact ..bwana Mbu...
 
Drogba ni hot cake na Waafrika inatupasa tujivunie kipaji cha mshkaji. Nimeskia Real Madrid wameshatenga kitita kumnyakua jamaa kabla hata ya ile gemu iliyojaa vimbwanga.

hey... STOP.. kweli lakini sio kujivunia kwa matusi mkuu hapa hatupo pamoja kabisa. Report inasema jamaa mpk kwenye Tunnel alikuwa bado anamtukana refa nini sasa cha kujivunia hapa. Yaani alichofanya kweli ni binadamu lakini ulimwengu mzima ulikuwa unaangalia. Sikuona logic ya yeye kuigeukia camera na kuanza kuongea ina maana kabisa kichwani mwake alikuwa anajua anachofanya na alijua kwamba watu wanamwangalia. He is Stupid...yes i mean it... Stupid

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=UHnDM4rFr1M"]YouTube - Didier Drogba loses his head![/ame]
 
hey... STOP.. kweli lakini sio kujivunia kwa matusi mkuu hapa hatupo pamoja kabisa. Report inasema jamaa mpk kwenye Tunnel alikuwa bado anamtukana refa nini sasa cha kujivunia hapa. Yaani alichofanya kweli ni binadamu lakini ulimwengu mzima ulikuwa unaangalia. Sikuona logic ya yeye kuigeukia camera na kuanza kuongea ina maana kabisa kichwani mwake alikuwa anajua anachofanya na alijua kwamba watu wanamwangalia. He is Stupid...yes i mean it... Stupid of them all

YouTube - Didier Drogba loses his head!

Labda urudie kusoma tena unachokinukuu maana kipo clear..labda kama una mengine.
 
Sikubaliani na unavyosema KUJIFANYA KU OVERREACT , na hapo ndipomnapokosea na ndio chanzo cha mambo yote..mnavyomuona uyu bwana ni mtu wa kufake fake tu na hayuko real.....mimi naamini alikua real na hakujifanya kuoverreact ..bwana Mbu...

...na hiyo ndio pointi yangu,...huyu bwana kila analofanya namuona fake! kuanzia nywele zake za kuchoma, kujiangusha, mpaka kujifanya eti ana hasira :)

Hivi ni dhambi mtu kupata hasira wakati ukihisi haukutendewa haki?

...hakuna dhambi kupatwa na hasira, ila dhambi ni matendo mabaya utayoyafanya baada ya kushindwa kuidhibiti hasira. Lakini Drogba yeye 'alijifanya' ana hasira, ...hakuwa na hasira.
 
Labda urudie kusoma tena unachokinukuu maana kipo clear..labda kama una mengine.

....hahahahah... sina mengine mkuu nimekuelewa sana kwamba real wanamtaka ........ lakini point yangu inabaki kwamba jamaa alichemsha na hakuna cha kujivunia. Karibu tena
 
....hahahahah... sina mengine mkuu nimekuelewa sana kwamba real wanamtaka ........ lakini point yangu inabaki kwamba jamaa alichemsha na hakuna cha kujivunia. Karibu tena

teh teh..kweli naona kweli hukuelewa..nilichosema ni kuwa tujivunie kipaji chake..(nadhani umeona hio bold)..lol

Kama hangekuwa na kipaji the mzunguz wangeshamfuta kazi siku nyiingii..oh..no hata VISA asingepata.. hata hivyo jamaa nadhani amezaliwa na kukulia Paris hivyo hamna 'kitimoto' wa kumzingua..got money in the bank na kipaji anacho..na mjeuri vilevile!

aurevoir..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom