Dreamliner ATCL yatumwa Sudan

Dreamliner ATCL yatumwa Sudan

Itarudi na Abria? Ikirudi tupu hasara iwapo tu wanalipa. Kama hawalipi haina maana

That is a charter flight....Atcl itakuwa imekula hela ndefu kama hamna ufahamu na baadhi ya field bora upite kama upepo bila kutoa comment
 
Vilevile Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Hiyo para nmeelewa, maana ila kwa gharama Ni upumbavu kutumia ndege yetu maaana inaenda kurudi tupu,(wakati UN watakuwa wamelipia kwenda TU)........

Haaah We jamaa Nan kakuambia kuwa ikienda itarudi tupu bila abiria?

Tujifunze utamaduni wa kufuatilia habari kwa ukamilifu wake pamoja kuandika ukweli na sio personal opinion yako kulazimisha iwe ndio habari

Dreamliner itarudi na Wanajeshi waliomaliza muda wao kuhudumu Darfur
 
Ilikwenda Harare trip moja kilichotokea mzee alisikia akaanguka..lengo halijafikiwa
Sasa issue ni abiria au ni marketing strategy hakuna.Anyway ukiuliza sana utaambiwa wewe mpinzani hata kama unataka kuweka mawazo yako inakuwa ngumu.Nipambane na hali yangu
 
bado linatapatapa mwisho wa siku litamilikishwa jeshi ili muache kuhoji kama ilivyofanywa kwa kivuko. Na hii ndo Tanzania. Tunaanza kujenga nyumba kabla hata kuchimba msingi, jiulize hiyo nyumba itasimamaje.

Aise kwa suala la kuwa na ndege Mkulu alikurupuka sana ,

Naona kwa sasa haliingizi kitu kabisa. Lipo tu .
Yaan mtu unaweka pesa mahali tena pesa nying afu haizai
 
Vilevile Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Hiyo para nmeelewa, maana ila kwa gharama Ni upumbavu kutumia ndege yetu maaana inaenda kurudi tupu,(wakati UN watakuwa wamelipia kwenda TU)........
Kwa kawaida hawa wanaokwenda, wanakwenda kubadilishana na kundi lililotangulia ... ni kitu kama "shift". Hata kama wanakwenda mara moja UN hulipia kwenda na kurudi kwa ndege waliyoikodi.
 
THE DREAMLINER

MAOFISA na Askari wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi inayoongozwa na Uzalendo,uadilifu, uhodari hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshi na wapiganaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuboresha Uchumi ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuonesha uzalendo kwa vitendo kwa kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana ya Taifa.

“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.

Aidha,Meja Jenerali kapinga alisema mbali na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.

Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la la Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi Alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi kwa Mchango mkubwa kufanikisha kupata tenda hiyo.

“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa maslahi ya Nchi “ Alisema Mhandisi Matindi.

Vilevile Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.

Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13, Luteni Kanali Khalfan Kayage anayekwenda na Kikosi hicho alisema kuwa inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya Tanzania Kimataifa.
Ikirudi itakwenda wapi?
 
Aise kwa suala la kuwa na ndege Mkulu alikurupuka sana ,

Naona kwa sasa haliingizi kitu kabisa. Lipo tu .
Yaan mtu unaweka pesa mahali tena pesa nying afu haizai
stay tuned hili dreamliner itaanza safari India julai, na baadaye china ,ila limekula madola yetu tungeweka madola katika viwanda tungepata faida nyingi sana .....
 
stay tuned hili dreamliner itaanza safari India julai, na baadaye china ,ila limekula madola yetu tungeweka madola katika viwanda tungepata faida nyingi sana .....
Mda ni jawabu zuri sana Maishan

Let me wait.
 
Shida sio kiruka ,shida ni je faida inapatikana?
 
LItatua kyela?
Kuna watu wanalihitaji huko
 
Uongozi wa etc inabidi uniongezee. Ndegr mnanunuliwa na kukabidhiwa bure, na wateja(tenda) nazo mpaka mtafutiwe?
 
Back
Top Bottom