Where is uniformity? Nchi yetu imechoka kiasi cha kushindwa kuwapa wote ma-backpack ya kijeshi ya aina moja? Naona wengine wanaingia na asante mmachinga kwenye ndege!
Unaongea hivyo sababu haujui vita ya kule, hujui chanzo, huwajui wanaopigana na hujui namna wanavyo shambuliana.
Namaanisha hujui tabia zao na mode of operrand yao hao Janjaweed.
Huko jeshini kuna watu wa ku-plan man o yote ikiwemo na risk zote za usafiri huo n.k.
Hahaha idadi ilikua kubwa na op ni nyingi acha woga.. ma dollar matamu hapo Congo joto lilikua kubwa sana ..Sikh 366 ni chache sana Ila ukiwa pale ukamaliza siku moyoni unajua mwenyew hahah
Hahaha idadi ilikua kubwa na op ni nyingi acha woga.. ma dollar matamu hapo Congo joto lilikua kubwa sana ..Sikh 366 ni chache sana Ila ukiwa pale ukamaliza siku moyoni unajua mwenyew hahah
Usinikumbushe mkuu.Nashukuru zilijenga nyumba za wazee.Darfur!What the hec was all that for,anyways!For the sake of our neighbours,brothers and sisters,outta there!Burying our damn bodies into sand dunes of that hotter land like fxck3n ostriches😂😂😂😂😂🔫👏👏👏👏👏
Maelezo yana uongo. Kama itakuwa ikisafirisha wanajeshi itakuwa ni wanajeshi wa Tanzania tu. Nchi zinapokuwa zinafanya deployment ya wanajeshi wake hupewa options mbili kuchagua 1) Ilipwe pesa ili isafirishe wanajeshi yenyewe au 2) UN itoe ndege ya kusafirisha wanajeshi. Nchi nyingi zenye mashirika ya ndege ya serikali huchukua option namba moja!
Kusema kulikuwa na tenda na wameshinda wanafanya ionekane kama ATCL sasa itakuwa inasafirisha wanajeshi wa UN wakati ni kwamba itsafirisha wanajeshi wa Tanzania tu.
Anayeshinda tenda ndiye hufanya option 2) hapo juu na hii hulazimisha ndege kupakaliwa rangi nyeupe na maandishi meusi “UN - United Nations” na inakuwa hadimu kuiona anga ya nchi mama kwa kipindi kirefu.
ATCL ikionekana iko vile tunavoifahamu - itakuwa haina mkataba na UN. Ninapongeza kuchagua option 1) na hii itaongeza mapato ya ATCL.
Ndege yetu ikatokea inatunguliwa,lawama kwa nani?! Kwa nini wasipelekwe na ndege za UN ambazo zinatambulika na kisheria haziruhusiwi kushambuliwa?!
Tumekosa safari za kimataifa zenye tija hadi tuvizie mara kupeleka mbuzi Dubai na sasa wanajeshi Sudan?! Je safari hizo ni endelevu kwa wiki ama mwezi mara ngapi?!
Hongera, kafanya nini? alinunua ndege kwa pesa zake mfukoni? Mkataba wa manunuzi ya ndege Kama sheria zinavyosema unaujua?
By the way, wanajeshi hawatakiwi kusafiri kwenye civil planes.
Ndege ya ATCL aina ya Boeing 787 Dreamliner yaenda Sudan kupeleka wanajeshi ktk jimbo la Darfur kulinda amani. Boeing 787 Dreamliner ya ATCL ni ndege mahsusi ya abiria yenye uwezo wa kwenda masafa marefu lakini hii ni mara ya kwanza kushiriki ktk operesheni za kijeshi kwa ajili ya ulinzi wa amani.
Akizungumzia ushiriki wa Tanzania ktk kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa, mkuu wa operesheni na mafunzo ktk JWTZ, Major General Alfred Fabian Kapinga amesema huu ni mwaka wa 12 mfululizo toka Tanzania ihusike ktk kampeni za ulinzi wa amani chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa.
Tanzania ina vikosi chini ya Umoja wa Mataifa kulinda amani ktk nchi za Lebanon, Central African Republic, Sudan na DR Congo. Na katika kupeleka vikosi imekuwa ikitumia ndege za JWTZ na zingine zilizokodishwa na Umoja wa Mataifa. Hii ni mara ya kwanza ATCL kutumika na kutakuwepo mwendelezo wa ATCL kutumika ktk misheni za ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa ATCL amesema wamefarijika shirika kupata tenda ya Umoja wa Mataifa kusafirisha walinzi wa amani. Amelishukuru jeshi JWTZ na wadau wengine waliofanikisha kupata kazi hii inayoshindaniwa na mashirika mengi ya ndege duniani ktk kufanya kazi za Umoja wa Mataifa.
THE DREAMLINER
MAOFISA na Askari wa Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania (JWTZ), wanaoshiriki Ulinzi wa Amani katika Jimbo la Darfur nchini Sudan kwa Mara ya kwanza kwa kipindi cha Miaka 10 ya Ulinzi wa Amani Jimboni humo wametumia Ndege ya Shirika la Ndege ya Serikali ya ATCL ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu katika kulifanya Shirika hilo linapiga hatua zaidi kwa maslahi ya Shirika na Taifa kwa ujumla.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita wa JWTZ Meja Jenerali Alfred Kapinga amesema Jeshi ni Taasisi inayoongozwa na Uzalendo,uadilifu, uhodari hivyo ni faraja kubwa kwa Jeshi na wapiganaji kuunga mkono jitihada za Serikali katika Kuboresha Uchumi ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika kuonesha uzalendo kwa vitendo kwa kutumia vitu vya nyumbani kwa maslahi mapana ya Taifa.
“ Tumekuwa tukitumia Ndege zetu za Jeshi lakini tumekuwa tukitumia Ndege za mataifa mengine kwa Mikataba kutoka Umoja wa Mataifa lakini sasa ni faraja kwani tumefanikiwa kuwashawishi Umoja wa Mataifa kutumia Ndege zetu” Alisema Meja Jenerali Kapinga.
Aidha,Meja Jenerali kapinga alisema mbali na kutumia Ndege hiyo lakini aliwaasa Maafisa na Askari hao kuhakikisha wanapeperusha vema Bendera ya Nchi na kuendelea kuitangaza kwa sifa nzuri za Utendaji Kimataifa.
Kwa Upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Ndege la la Tanzania (ATCL), Mhandisi Ladislaus Matindi Alisema ni Fursa Nzuri kwa ATCL na wanalishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania kupitia kwa mkuu wa majeshi ya Ulinzi kwa Mchango mkubwa kufanikisha kupata tenda hiyo.
“ Namshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo na watendaji wake kwa Uzalendo wake na kuhakikisha anafanikisha ATCL kupata fursa kwa mara ya kwanza na hii itakuwa mwanzo mzuri na tutahakikisha tunaitumia vizuri fursa hii kujitangaza zaidi Kimataifa kwa maslahi ya Nchi “ Alisema Mhandisi Matindi.
Vilevile Mhandisi Matindi aliongeza kuwa Ndege ya Dream Liner ina uwezo wa kusafiri kwa saa 12 bila kusimama, hivyo kwa kutumia saa tatu kusafiri kutoka hapa mpaka nchini Sudan ni sehemu ndogo ya Uwezo wake na ni nafasi ya kuwajaribisha watendaji wa Ndege wa ATCL katika kuhudumia safari Ndefu.
Naye Kamanda wa Kikosi cha TANZBATT- 13, Luteni Kanali Khalfan Kayage anayekwenda na Kikosi hicho alisema kuwa inawapa nguvu kupeperusha Bendera yetu kupitia Ndege na ameahidi kufanya kazi kwa Bidii kuendeleza jina na sifa nzuri ya Tanzania Kimataifa.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.