DRC: Wanajeshi wa Kenya wamewasili DRC huku waasi wakikaribia Goma

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
Wanajeshi wa Kenya wamewasili Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa ajili ya kupambana na makundi ya waasi ambayo yamesababisha ukosefu wa usalama katika eneo hilo kwa miongo kadhaa.
5421C065-4BB5-49D1-BD62-6317DD00102A.jpeg

Wanajeshi 903 wa Kenya wameingia DRC chini ya makubaliano ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wanajeshi hao watashika doria katika mji wa Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambako mapigano makali yameripotiwa Ijumaa, kati ya wanajeshi wa serikali ya DRC na kundi la waasi la M23.
2E266399-5B0C-4702-85EA-A8B4FE2FE5CC.png

Kamanda wa kikosi cha Kenya Luteni Kanali Dennis Obiero, ameambia waandishi wa habari mjini Goma kwamba lengo lao kubwa ni “kumshambulia adui kwa ushirikiano na jeshi la DRC na kusaidia katika kuyapokonya silaha makundi ya waasi.”

Obiero amesema kwamba “ukosefu wa usalama ni jambo ambalo linaharibu maisha ya kila mtu katika jamii.”
5EC5BFF4-A872-47BC-AAB7-3947FD2B426A.jpeg

Ameeleza kwamba jeshi la Kenya litashirikiana na mashirika ya kutoa misaada katika kurejesha utulivu na amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Kuna zaidi ya makundi ya waasi 120 mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, ambayo yamekuwa yakishambulia raia, kusababisha vifo na uharibifu wa mali.

Waasi wa M23 wameongeza mashambulizi
Mapigano makali yamekuwa yakiendelea kati ya kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika sehemu ya Rugari, Kivu Kaskazini tangu Ijumaa.

Kulingana na mwandishi wa VOA mjini Goma, mapigano kati ya waasi hao na wanajeshi wa DRC yanaendelea katika mji wa Kibumba, kilomita 25 kutoka Goma.
Mji wa Goma ni mji mkubwa wa kibiashara, wenye zaidi ya watu milioni moja.
Usambazaji wa nguvu za umeme umetatizika mjini Goma ambapo waasi hao wanalenga kudhibiti.

Kundi la M23 liliwahi kudhibiti mji wa Goma mnamo mwaka 2012 kabla ya kufurushwa na jeshi la serikali.
Kundi hilo limedhibiti mji wa Bunagana, mpakani na Uganda.
 
Acha kupotosha bhana. Licha ya Kenya kuahidi kutumia $ 37m kutuma kikosi Cha wanajeshi zaidi ya 900 nchini DRC,lakini mpaka Sasa ndege mbili zilizowasili mjini Goma zimebeba wanajeshi 118 tu wa Kenya. Wewe hao 900 waliowasili DRC mpaka Sasa umewatoa wapi?
MTZ 255Dar bado umenisahihisha kimakosa ni wanajeshi 900 waliowasili DRC

Al Jazeera’s Webb said the first arrivals were expected to be part of a larger force sent by Nairobi.
98719EDD-9332-4F5F-AA39-1AD2F01E0A5B.jpeg

“Kenya says it’s going to send a battalion of around 900 soldiers. This is a tiny number when you consider the vast territories controlled by armed groups in the eastern DR Congo, or compared to the UN peacekeeping force which has at times had as many as 20,000 soldiers and has failed to stabilise the region,” he said.

“People are waiting to find out what these Kenyan troops will actually do, and whether they will join in the DR Congo army’s fight against M23.”
 
MTZ 255Dar bado umenisahihisha kimakosa ni wanajeshi 900 waliowasili DRC

Al Jazeera’s Webb said the first arrivals were expected to be part of a larger force sent by Nairobi.
View attachment 2415480
“Kenya says it’s going to send a battalion of around 900 soldiers. This is a tiny number when you consider the vast territories controlled by armed groups in the eastern DR Congo, or compared to the UN peacekeeping force which has at times had as many as 20,000 soldiers and has failed to stabilise the region,” he said.

“People are waiting to find out what these Kenyan troops will actually do, and whether they will join in the DR Congo army’s fight against M23.”
Kichwa chako mbona Ni Kigumu kuelewa?

Kenya imeahidi kutuma wanajeshi zaidi ya 900 kwenda DRC. Lakini mpaka Sasa Ni ndege 2 za kijeshi zimewasili mji wa Goma zikiwa na wanajeshi 118 tu. Kwahiyo wanajeshi 900 walioahudiwa na Kenya Bado hawajafika DRC.
 
Tz sisi tunapeleka wangapi

..Tanzania imepeleka Congo wanajeshi 800+ walioko ktk kikosi cha UN/SADC kinachojumuisha wanajeshi wa Tanzania, Malawi, na Afrika Kusini.

..Askari wa Tanzania wamekuwepo DRC tangu wakati wa Uraisi wa Jakaya Kikwete.

..Pia kipindi Kikwete akiwa Raisi askari toka DRC waliletwa Tanzania kupata mafunzo ya Maafisa wa jeshi.

..Kabla ya hapo wakati wa Mkapa Tanzania ilipeleka wakufunzi wa kijeshi kufundisha askari wa DRC.

..Wakufunzi hao waliondolewa wakati Rwanda wamevamia DRC kumpindua Mzee Kabila.

..Hapa chini mtaona askari walinda amani wanawake toka Tanzania wanavyoshirikiana na wananchi wa DRC.

..Tanzania imepeleka Congo wanajeshi 800+ walioko ktk kikosi cha UN/SADC kinachojumuisha wanajeshi wa Tanzania, Malawi, na Afrika Kusini.

Wanajeshi wa JWTZ wameenda Congo kwa mwavuli wa MONUSCO tunataka sasa waende kwa mwavuli wa makubaliano ya EAC km Kenya.
 
Wanajeshi wa JWTZ wameenda Congo kwa mwavuli wa MONUSCO tunataka sasa waende kwa mwavuli wa makubaliano ya EAC km Kenya.

..nadhani suala hilo ni gumu.

..vikosi vyetu vilivyoko MONUSCO viko pale kupitia jumuiya ya SADC.

..naamini Tanzania tutakuwa tunajichanganya kuwa na vikosi ktk SADC na EAC ndani ya DRC.
 
..vikosi vya Tanzania vikiwasili DRC.

..ukisikiliza hiyo video wanaripoti kuwa Tanzbatt-7 wamebadilishana na Tanzbatt-8.

..maana yake ni kwamba tangu 2013 hicho ni kikosi[battalion] cha 8 cha Jwtz huko DRC.

..pia kamanda mkuu wa Force Intervention Brigade inayohusisha Tanzania, Malawi, na Afrika Kusini, kwa sasa hivi anatokea Jwtz.

..Kamanda Mkuu wa Force Intervention Brigade ni nafasi ya kupokezana kati ya Jwtz, Mdf, na Sandf.

Wakenya wameyasahau ya Al-Shabab yaliyotokea Westgate? Nahofia M23 wasije wakaamua kupanga kujilipua nda ya Kenya.
 
Back
Top Bottom