Dr. Wilbrod Slaa kesho kuanza rasmi vikao vya chama

Dr. Wilbrod Slaa kesho kuanza rasmi vikao vya chama

Status
Not open for further replies.
Hatimaye katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa kesho ataanza rasmi kuhudhuria vikao vya chama ambapo atahudhuria kikao cha kamati kuu ya Chadema.

Kuonekana kwa Dr. Slaa kesho kutamaliza rasmi mjadala wa muda mrefu na propaganda zilizotawala eti Dr. Slaa kajitoa Chadema.

Katika hatua nyingine, upigwaji wa kura za maoni katika jimbo la Kibamba kwa watia nia wa Chadema utafanyika kesho baada ya mtia nia John Mnyika kupata nafua kutokana na kusumbuliwa na homa kwa muda.

Habari na G Sam
Mkuu wamaanisha kuumwa kwa Mnyika kumesababishwa kura zisipigwe Kibamba?
 
Mimi siyo mdini kwa kawaida ila kwa yanayomkuta Dr Slaa kuna harufu ya udini,Mbowe ni Mlutheri na Lowassa ni Mlutheri pia,kuna uwezekano Dr Slaa yanamkuta haya yanayomkuta kwasababu ni Mkatoliki,Mbowe kuwa makini na namna mnavyomfanyia Dr Slaa, mtapoteza kura za Wakotiliki wengi,Dr Magufuli ni Mkatoliki lazima mkumbuke,tupo wengi.
Siasa bwana, leo nimesikiliza kwa makini ile hotuba ya Lowassa aliyoitoa wakati anajiunga Chadema.

Kuna mstari anasema alikatwa sababu ya dini yake.?

Ngoja kwanza...
 
Teknolojia, I respect you Comrade..!!

Linapokuja suala la siasa jaribu kidogo suala la Dini likae pembeni, Nafurahi kusikia kwamba kwa Kawaida wewe si mdini, Lakini funga Novena kwaajili ya pepo huyu mchafu anayekunyemelea! Binafsi nani ni Mkatoliki, lakini linapokuja suala la kuchagua kiongozi, Dhehebu langu na Dini yangu huweka pembeni. Uwezo, Uchapakazi, Maono ya kazi ndivyo huchukua nafasi. Kamwe Dini, Dhehebu halijawahi kuwa kigezo ktk kumchagua kiongozi yeyote maishani mwangu, Natamani sana iwe hivyo hata kwako.

Kwa yanayotokea kwa Dr Slaa.

Mkuu Tek, Dr Slaa mpaka tunapoandika haya hakuwa amechukua fomu kugombea nafasi ya Urais ndani ya Cdm. Kinachotokea kudelay kwa Dr Slaa ni kusimmia misingi tu hakuna kingine chochote. Na kinachotokea kwa Mbowe na Lowassa ni hamu ya kuongoza na Matamanio ya kuiondoa ccm Madarakani. Hakuna suala lolote linalohusiana na Misingi ya Dini ili kufikia Maamuzi hayo. Ondoa mawazo hayo Kamanda wangu.

BACK TANGANYIKA

pokea likes 100 i salute you kamanda wa ukweli, hakuna kitu kibaya kama siasa za udini halafu ukiona hata watu makini nao wanaanzakujiingiza kwenye udini inakatisha tamaa
 
Mkuu, Dr. Slaa ni kiongozi mahiri wa Chadema. Hatutathubutu kamwe kufanya mzaha eti tukampoteza! Tumehakikisha kuwa anarejea katika hali yake kama awali na niwahakikishieni kuwa Dr. Slaa ameongeza ari na nguvu kuhakikisha CCM inang'oka

Kamanda nimekuelewa vzr sanaaa
 
Sala za wanamaombi zimefanya kazi, come on comred. We know that the fiancé needs you, but the nation needs you the most.
Amina! Kindly dr sikiliza sauti za watanzania wanaolitakia taifa hili mema. Puuza wanaoongea upuuzi ili uondoke cdm then wafanye sherehe. Kubaliana tu na hali halisi . wewe ni chumvi katika chakula kinachoandaliwa na ukawa.
 
Nyie endeleeni kutapakanya uongo tu humu,Yericko yalimkuta kwa mambo kama hayo.
 
Hatimaye katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa kesho ataanza rasmi kuhudhuria vikao vya chama ambapo atahudhuria kikao cha kamati kuu ya Chadema.

Kuonekana kwa Dr. Slaa kesho kutamaliza rasmi mjadala wa muda mrefu na propaganda zilizotawala eti Dr. Slaa kajitoa Chadema.

Katika hatua nyingine, upigwaji wa kura za maoni katika jimbo la Kibamba kwa watia nia wa Chadema utafanyika kesho baada ya mtia nia John Mnyika kupata nafua kutokana na kusumbuliwa na homa kwa muda.

Habari na G Sam

Wewe mpuuzi sana unayefikiri kwa kutumia masaburi. Dr SLaa hawezi kujidhalilisha kwa propaganda za kijinga
 
Mimi siyo mdini kwa kawaida ila kwa yanayomkuta Dr Slaa kuna harufu ya udini,Mbowe ni Mlutheri na Lowassa ni Mlutheri pia,kuna uwezekano Dr Slaa yanamkuta haya yanayomkuta kwasababu ni Mkatoliki,Mbowe kuwa makini na namna mnavyomfanyia Dr Slaa, mtapoteza kura za Wakotiliki wengi,Dr Magufuli ni Mkatoliki lazima mkumbuke,tupo wengi.

Nikigundua hilo nitakuwa wa kwanza kupinga
By the way ww unafanya kazi waliyokutuma Lumumba
 
Hatimaye katibu mkuu wa Chadema Dr. Willbrod Slaa kesho ataanza rasmi kuhudhuria vikao vya chama ambapo atahudhuria kikao cha kamati kuu ya Chadema.

Kuonekana kwa Dr. Slaa kesho kutamaliza rasmi mjadala wa muda mrefu na propaganda zilizotawala eti Dr. Slaa kajitoa Chadema.

Katika hatua nyingine, upigwaji wa kura za maoni katika jimbo la Kibamba kwa watia nia wa Chadema utafanyika kesho baada ya mtia nia John Mnyika kupata nafua kutokana na kusumbuliwa na homa kwa muda.

Habari na G Sam

Mkuu kwani we ni nani ndani ya CHADEMA? na hiyo taarifa umeipata wapi? Source pls... Kama ni wewe mwenyewe umeambiwa na Dr. au?!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom