Dr Walid Amani Kabourou yuko wapi?

Dr Walid Amani Kabourou yuko wapi?

I know what you mean mkuu.
Lakini ni muhimu kukumbushana mambo kama haya ambayo yanatukumbusha tumetoka wapi, tulitakiwa kuwa wapi na wapi tulipo sasa; wapi tunataka kuelekea na tufanye nini ili kufika huko tunapopataka.

Naunga mkono mkuu ni muhimu kutafakari katika safari yetu kama sote ni mamba au kuna kenge kati yetu mfano Shibuda tushamuona, historia ni matukio ya juzi na jana ili yatupe muelekeo ya ku-anticipate ya kesho
 
Naunga mkono mkuu ni muhimu kutafakari katika safari yetu kama sote ni mamba au kuna kenge kati yetu mfano Shibuda tushamuona, historia ni matukio ya juzi na jana ili yatupe muelekeo ya ku-anticipate ya kesho
Bila hivyo tutakua tuna-manufacture vyibuda na hatimaye kupiga hatua moja mbele, mbili nyuma.
 
Dr. Warid Kabouru! au ndi anataka anzisha chadema asili?
 
Homie, huyu jamaa alivuruga sana harakati za demokrasi kwa kuwasaliti vijana wa Mwanga, Bangwe, Buzebazeba, Gungu, Majengo, Kibirizi na Ujiji. Sasa anavuna matunda ya usaliti wake, magamba walimtumia sasa wamemtelekeza.
Vijana wa KG walikesha kule ukumbi wa kuhesabu kura Bangwe kuhakikisha hakuna kura haziingizwi ukumbini wakati wa kuhesabu. Walipigwa na FFU kwa ajili yake, matokeo yake usaliti.
Historia ya Dk Kaburu hunifanya nisimuamini sana Zitto.

Vijana wa Kigoma wanamwita pimbi ukiwakumbusha habari za Kaburou wapata kichefuchefu
 
Nikienda mbinguni na kumkuta, nitamuomba mungu niende kwa shetani! Serious

Ni kweli alitukwaza nikikumbuka nilivyolala na njaa kwa ajili yake ili aende mjengoni, Hata hivyo kama Mungu atamsamehe atakuwa ametubu na sisi itabidi tumsamehe lakini kuomba kwenda kwa shetani utakuwa umepata hasara ya milele jitahidi kwa kadri uwezavyo usiende huko hebu pacheki au kupasikia HAPA Diggs Journey Gateway
 

Karudi USA... Maisha Bongo ya CCM yamshinda na Ph.D yake
 
Dr. Amani warid k. Alidhani siasa ina maslahi siasa ni wokovu wa kufa msalabani ili watu wanaokuamini waokoke mwanzoni ndivyo alivyofanya. Aliwaamsha wanakigoma walioitwa wakimbizi wakati huo na hata viongozi wa serikali (baadhi). Ila kutema kwake big g kwa karanga za kuonjeshwa ni pimbi, mkenge, na msaliti. Sisi walimu tunaotoa taaluma anastahili kuvuliwa hana hadhi ya kuitwa Dr. Hoja ni je yuko wapi! Mi mwl. Sina haja ya kujua shetani aliko ila natakiwa kumuepuka!
 
Anakula urojo kwa kuthamini mbinu za kuangamiza upinzani. Nasikia kahamia Kigamboni, akila pensheni kwa dhuluma hii.

Acha kua unangea maneno yasio na msingi ilimradi tu uchangie mada bwana,ngoja nikufundishe kitu kaka,yani ni kwamba kuhama chama sio dhuluma kwa yeyote na sisi Wenye ujuzi huwa hatuangalii vyama kaka sisi huwa tunaangalia maendeleo kwa hiyo mtu sio lazima awe chadema au CUF ndo afanye maendeleo,kwahiyo kuhama chama kwa huyu bwana isiwe nongwa.
 
Lamwai, Hiza, Cabourou, bado yule Mmama wa Wanawake Mbeya (CHadema), aliishia wapi? Shitambala je? CCM inaua kikatili mno jamani.
 
huyu jamaa kwa sasa ndio mwenyekiti wa ccm mkoa wa kigoma
 
Kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Kigoma na Mjumbe wa NEC ya CCM.Huenda akaingia pia kwenye Kamati Kuu pindi itakapochaguliwa hapo Mwakani
 
Sikilizeni! Dr Aman Walid Kabourou aliihama CDM kwa pesa ya EPA. Mwenye jukumu la kuhakikisha anahamia CCM alikuwa Maranda ambaye magamba wammefunga jela. Maranda na Dr Kabourou wana uhusiano wa kidugu, na ndiyo sababu kila siku kesi ya Maranda ilipokuwa inatajwa ama kusikilizwa pale Kisutu Dr Kabourou alikuwepo. Baada ya kukwapua pesa ya EPA, Mangulla akampa Maranda kazi ya kuhakikisha analirejesha jimbo la Kigoma Mjini CCM. Kumbuka waratibu wakuu wa EPA ndani ya CCM walikuwa Mangulla, Rostam, Mama Meghji na Salome Mbatia. Dr Kabourou akapewa sh 147 millioni kutoka zile za EPA, aliandikiwa hundi na Maranda. Ushahidi upo kwenye ripoti ya uchunguzi ya Hosea, Mwanyika na Mwema. Dr Kabourou akaahidiwa ubunge wa Afrika Mashariki, akapata. Siku hizi sijui alipo! Atakuwa anatafutiwa nafasi, subirini.
Kama ni mcheza Darts, basi hapo umepiga kwenye BULL. Huyu bwana kwa sasa anaishi KIGAMBONI naona huo mgao alioupata aliamua kwenda kujenga kibanda chake huko ili ajifiche vizuri.
 
Kama ni mcheza Darts, basi hapo umepiga kwenye BULL. Huyu bwana kwa sasa anaishi KIGAMBONI naona huo mgao alioupata aliamua kwenda kujenga kibanda chake huko ili ajifiche vizuri.

Kigsmboni ya Dar au ya Dodoma ?
 
Hata mimi nilikua najiuliza kuhusu huyu jamaa. Ila alikosea sana kurudi gambani huyu ni sawa na akina Masumbuko Lamwai wamepotea kabisa hata ndugu yangu Tambwe Hiza wote hawa kushinei baada kurudia gamba
dah! Umenikumbusha tambwe hiza, mwanzoni wakati anajiunga ccm alipewa kakitengo pale kwa kina nape, walipoona sasa amekwisha nasikia wamechukua cheo wamemuacha anashangaa tu!
 
hebu fuatilieni mwenyekit wa CCM mkoa wa kigoma ni nani?nadhani huyu bwana amechaguliwa uchaguzi uliopita kuwa mwenyekiti
 
Acha kua unangea maneno yasio na msingi ilimradi tu uchangie mada bwana,ngoja nikufundishe kitu kaka,yani ni kwamba kuhama chama sio dhuluma kwa yeyote na sisi Wenye ujuzi huwa hatuangalii vyama kaka sisi huwa tunaangalia maendeleo kwa hiyo mtu sio lazima awe chadema au CUF ndo afanye maendeleo,kwahiyo kuhama chama kwa huyu bwana isiwe nongwa.

Hata kama.........na je kwa nini amekuwa bubu........mwanasiasa muhimu kusikika
 
Back
Top Bottom