Dr. W. Slaa anaondoka CHADEMA

Dr. W. Slaa anaondoka CHADEMA

Naomba tu niseme atoke atakayetoka na aingie atakayeingia

Nitakacho mimi ni mabadiliko tu, maCCM yaondoke tu bac
 
Naendelea kusisitiza, amini niliyoyaleta hapa. Hili si jukwaaa la porojo na wala siwezi kushusha hadhi yangu kwa kuleta uongo. Dk. Slaa anaondoka usiku huu. Take my word.
 
Nimeangalia post zako za nyuma hujawai kuwa mfuasi wa Dr wala Ukawa.
Ufuasi haupo tu kwenye comment mkuu..... upo katika nyanja nyingi ikiwa ni fikra, mawazo, msimamo nk. Pia, katika siasa masaa 24 ni mengi sana kutokea mabadiliko hivyo hata hii inaweza kuwa ni comment yangu ya kwanza kuonesha mabadiliko.
 
Sasa usiku huu anakwenda kumkabidhi nani hivyo vitu? Kwanini asiende mchana? Au anakwenda kuvitelekeza hivyo vitu maana ofisi zitakuwa zimefungwa.Hebu jipange basi mleta maada!

Ina maana hawezi kukabidhi kesho?
 
Najua wapo watakaobeza na hata kutukana lakini napata ushujaa wa kuyasema haya. Dk. slaa usiku huu anaingia makao makuu kukabidhi gari, kadi, walinzi na cheo. Anajitoa chadema. Naomba uzi huu uachwe hapa hapa ili baadaye nihukumiwe kwa haki.

Chanzo: mimi mwenyewe.

Manyerere wewe ni mwandishi mwenye heshima kubwa ktk jamii,
na heshima hii umeijenga kwa kuandika habari zenye weredi wa hali ya juu kwa kuzingatia maadili ya kazi yako.
Huu uvumi umekuwepo toka jana ukakolezwa na gazeti la Raia tanzania toleo la leo.
Tumeonyeshwa picha jioni dr slaa akiingia ktk ofisi za chama na kuomba radhi kwa kuchelewa.Kuonyesha kwamba wapo pamoja.

Wewe unatuletea habari za kukabidhi ofisi usiku huu, kitu gani kitatufanya tuamini habari yako?
kwa heshima uliyonayo jazia nyama habari yako au ulete mlolongo zaidi kinachoendelea.
 
nashawishika maana jamaa hajatokea hata leo pale Rais wa awamu ya 5 Lowasa anapochukua fomu.
ila tulimpenda japo binafsi naamini nguvu ya lowasa ni kubwa kuliko yake kwenye kugombea urais. yan mafanikio yapo karibu zaidi kwa lowasa kuliko kwa silaa na hata tafiti mbali mbali zilionyesha hivyo..Silaa ni mtu makin na akiondoka ji pigo pia ila ni bora akaondoka maana mtaji wa lowasa ni mkubwa kuliko wake.
namheshimu na ningependa abaki lakina kama hawezi hatuna jinsi ukweli ni kuwa tunadhamini mchango wake katika kujenga upinzani wa kweli lakini kwa kuwa inatakiwa itumike njia yoyote ile ili kuhakikisha ccm inaondoka madarakani na lowasa ni mtu sahihi zaid ya Silaa.
 
ikitokea hajafanya hayo uliyomtabiria wewe....tukuchukuliaje wewe.....??
 
..siwezi kuamini hadi iwe hivyo..ila kama ndivyo...basi nitaamini kuwa dr.Slaa si strategist mzuri....maana kama ataondoka ataua sana nguvu ya UKAWA...na lazima itajulikana kuwa nae alijali zaidi madaraka....na ata provekuwa Mbowe ni zaidi yake ki mikakati...maana Mbowe ameweza kukubali hali halisi kufatana na mazingira yaliyopo...na hata kuamua kugombea ubunge jimboni mwake....Kinachowazuia hawa kina Dr. Slaa kufanya hivyo ni nini???....

...Lazima Dr. Slaa atambue kuwa odds za yeye kushinda uchaguzi mkuu kama angepitishwa UKAWA ingekuwa ndogo sana..maana kwanza alishindwa mwaka 2010...kinacho mfanya afikiri angeshinda this time around dhidi ya magufuli ni nini???..Lazima awe strategist anaefanya maamuzi kwa kufatana na wakati..

...Nilianza kupoteza msimamo wangu dhidi ya Dr. Slaa tangu alipokuwa anaandamwa na ma kesi ya kifamilia....pale alimwacha mke wake wa zamani mama Rose Kamili na kumchukua mke wa mtu mama mshumbusi....Kwa hiyo lazima nae kabla hajafanya maamuzi ya kuondoka chadema atambue kuwa hakuna binadamu aliye perfect...na kwamba siasa hubadilika kutokana na mazingira (kama wanavyosema dynamics za kisiasa)....Mbona wenzak huko chadema wamekubali hali halisi???....napata mashaka na maamuzi yake (kama itakua hivyo)kuyafanya kwa kumsikiliza mamamshumbusi....Hatumtaki rais afanyae maamuzi kwa kumsiliza mkewe....Hata Lowassa aliombwa sana na mkewe asihame ccm lakini alifanya maamuzi magumu.....Maamuzi yaliyowafungua watanzania ma milioni toka vifungo vya kifikra....
 
kwa jinsi ninavyomfahamu Dr Slaa kamwe hawezi kuchukua hatua za kuondoka Chadema eti kwa sababu hatagombea Urais
acheni kumpakazia hasa wewe Manyerere Jackton wewe ni mtu usiye eleweka misimamo yako,kaa mbali na process zote zinazoendelea kwenye nchi yetu hufai hata kidogo kuwa mtoa taarifa za muhimu
Dr Slaa siyo mtu mjinga kiasi hicho ni mtu smart nimekuwa naye karibu kwa muda mrefu na namwamini sana


Unamfahamu mwandishi aliyetumika kumchafua Dk Salim Ahmed Salim?? basi huyu ndiye aliyejivika jina bandia baadae akagundulika!!!
 
Najua wapo watakaobeza na hata kutukana lakini napata ushujaa wa kuyasema haya. Dk. slaa usiku huu anaingia makao makuu kukabidhi gari, kadi, walinzi na cheo. Anajitoa chadema. Naomba uzi huu uachwe hapa hapa ili baadaye nihukumiwe kwa haki.

Chanzo: mimi mwenyewe.

Magufuli amekuwa sio news tena,
Kuua habari za Lowassa mnaleta za kuhama.

Anahamia wapi? Ethiopia au?
 
Back
Top Bottom