Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Wakuu natanguliza salamu ,

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Kyela , kijiji cha Kajunjumele ,utamaduni wa Kyela na Rungwe unashabihiiana kwa kiasi kikubwa sana , wakazi wengi wa Wilaya hii ni Wanyakyusa , japo kuna makabila mengine.

Tunazo ngoma za asili ambazo kwa uchache ni Mang'oma , Ipenenga , Samba nk , na tumecheza ngoma hizi kwa miaka mingi bila msaada wa hela ama chochote kutoka kwa yeyote , kama kuna aliyetoa chochote basi alitoa kama vile PDG Ndama Mutoto wa ng'ombe anavyowapa wanamuziki wa FM ACADEMIA .

Sasa cha kushangaza mwaka huu amezuka mfadhili wa ngoma za asili aitwaye Tulia Ackson , Huyu tetesi zinadokeza kwamba lengo lake si kufadhili ngoma za asili , maana alikuwepo miaka yote na alikuwa na uwezo kama huu wa leo , lakini hakufanya hivi , taarifa zinaonyesha kwamba amelenga kurubuni wakazi wa Rungwe ili achaguliwe mbunge uchaguzi ujao .

Mbinu hii ya kizamani haikubaliki , na naomba kuchukua nafasi hii kuwaasa wana Rungwe kumuogopa huyu mama kama ukoma .

Dr Tulia aliyeingia bungeni na kubebwa kwa mbeleko ya chuma hadi kwenye unaibu spika , amekuwa mstari wa mbele kudhalilisha na kunyanyasa wabunge wa upinzani , amezima mijadala mingi yenye tija ili kuokoa chama chake , huyu hawezi kuwa msaada wa Akina Mama wauza ndizi na maziwa wa ushirika au Kiwira , hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Makandana , hafai .

Dr Ngunangwa aliwahi kuwauliza waliokuwa wanajipitisha kwenye jimbo lake huko Njombe na kutoa zawadi za baiskeli nk , kwamba WALIKWINA ? yaani kwa kiswahili , MIAKA YOTE WALIKUWA WAPI ?

Nakala ya uzi huu imfikie JOHN MWAMBIGIJA .
hivi wewe kila kitu unaweza kukifanya kwa wakati mmoja? huu ndiyo muda muafaka kwake kufanya hayo anayoyafanya hapo mwanzo kuna mengine alikuwa anafanya pia
 
Back
Top Bottom