Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Dr Tulia Ackson Miaka yote aikuwa wapi?

Nyie wanyakyusa hizo siasa zenu za maji taka ndizo zinazowafanya muendelee kushika mkia. Badala ya kufurahia KWAMBA mmempata mtu influential, pia mwenye networks na exposure, mnaongea MAMBO yasiyo eleweka. Jifunzeni KUTUMIA talents mbalimbali kujiletea maendeleo YENU. Jifunze NAMNA ya kutumia elites, business people, influential people to form a composite team for betterment of area. Siasa za majitaka hazita wafikisha popote.
Ni beneficial kwa Familia yako na Ukoo wake, kwangu Mimi hana Jipya! Wanyakyusa hatujawahi kuwa wanafiki kamwe! So you better understand this.
 
Ni beneficial kwa Familia yako na Ukoo wake, kwangu Mimi hana Jipya! Wanyakyusa hatujawahi kuwa wanafiki kamwe! So you better understand this.

Sijaongelea issue za beneficial hilo moja. Mbili sijaongelea person but the entirety. KAMA hujaelewa soma upya hiyo post.
 
Ulinikigili ukaja nkafu. Usiamini unachoamini wewe ndio sahihi tu mengine sio. Kasoro yetu ni kuona kuwa mawazo yetu ndio sahihi na bora kuliko wengine. Ulinamanjele🙁🙁🙁🙁
Huyu mama namchukia sana hasa anavyojifanya kujua zaidi pia sura yake na urefu havinifirahishi zaidi anavyowaonea wabunge wa vyama vingine hasa chadema nikimuona tu kwenye luninga nahamisha channel
 
sifikirii kama wananchi watampa ubunge mama huyu..ila kwa kutumia nguvu ike waliyo tumia kinondoni na siha ndivyo vitakavyo mpa ubunge..over
 
Huyu mama namchukia sana hasa anavyojifanya kujua zaidi pia sura yake na urefu havinifirahishi zaidi anavyowaonea wabunge wa vyama vingine hasa chadema nikimuona tu kwenye luninga nahamisha channel
wana jamii mnajua kwanini serikali yetu haiwezi kuleta maendeleo au kuendelea?

Sababu ma PHD wengi mno wamo kwenye serikali.
Usidhani kuwa na PHD ndio mzuri kwa administration NO.
PHd zawo wakafanye research za kuleta maendeleo na siasa na administration wawaachie watu wengine.
 
Nadhani sasa mnaelewa Kwanini Jf inapigwa vita .
 
Nakala imfikie mchumi tumbo Trump 2 A.K.A Wandamba
 
Mimi sina chama lakini hamuoni kuwa mkiwa na wabunge wengi wa vyama vingine kuliko wa chama kuu nchi itakuwa na ubora zaidi? Kutakuwa na uwajibikaji zaidi?
 
Wakuu natanguliza salamu ,

Naomba kuweka wazi kabisa kwamba mimi ni mwenyeji wa Mkoa wa Mbeya , Wilaya ya Kyela , kijiji cha Kajunjumele ,utamaduni wa Kyela na Rungwe unashabihiiana kwa kiasi kikubwa sana , wakazi wengi wa Wilaya hii ni Wanyakyusa , japo kuna makabila mengine.

Tunazo ngoma za asili ambazo kwa uchache ni Mang'oma , Ipenenga , Samba nk , na tumecheza ngoma hizi kwa miaka mingi bila msaada wa hela ama chochote kutoka kwa yeyote , kama kuna aliyetoa chochote basi alitoa kama vile PDG Ndama Mutoto wa ng'ombe anavyowapa wanamuziki wa FM ACADEMIA .

Sasa cha kushangaza mwaka huu amezuka mfadhili wa ngoma za asili aitwaye Tulia Ackson , Huyu tetesi zinadokeza kwamba lengo lake si kufadhili ngoma za asili , maana alikuwepo miaka yote na alikuwa na uwezo kama huu wa leo , lakini hakufanya hivi , taarifa zinaonyesha kwamba amelenga kurubuni wakazi wa Rungwe ili achaguliwe mbunge uchaguzi ujao .

Mbinu hii ya kizamani haikubaliki , na naomba kuchukua nafasi hii kuwaasa wana Rungwe kumuogopa huyu mama kama ukoma .

Dr Tulia aliyeingia bungeni na kubebwa kwa mbeleko ya chuma hadi kwenye unaibu spika , amekuwa mstari wa mbele kudhalilisha na kunyanyasa wabunge wa upinzani , amezima mijadala mingi yenye tija ili kuokoa chama chake , huyu hawezi kuwa msaada wa Akina Mama wauza ndizi na maziwa wa ushirika au Kiwira , hafai hata kuwa Mwenyekiti wa kijiji cha Makandana , hafai .

Dr Ngunangwa aliwahi kuwauliza waliokuwa wanajipitisha kwenye jimbo lake huko Njombe na kutoa zawadi za baiskeli nk , kwamba WALIKWINA ? yaani kwa kiswahili , MIAKA YOTE WALIKUWA WAPI ?

Nakala ya uzi huu imfikie JOHN MWAMBIGIJA .
Tulistuka mapema sana ! Hakika mbinu za ccm ni za kiwango cha chini sana ! Hongera intelijensia ya chadema
 
Mimi sina chama lakini hamuoni kuwa mkiwa na wabunge wengi wa vyama vingine kuliko wa chama kuu nchi itakuwa na ubora zaidi? Kutakuwa na uwajibikaji zaidi?
CCM ni waoga sana , wanaogopa mno kulipiwa kisasi kwa unyama waliotutendea
 
Mara anataka jimbo la mbeya mjini, mara rungwe, atatokea mwingine aseme huyo mama anataka jimbo la maswa😀😀

Mwacheni dada afanye yake, hata makanisani mtu mzee akiokoka huwa haulizwi ujana wake alikuwa wapi kuokoka?. Anapojitambua na kuamka, muungeni mkono chamsingi anafanya watu wafurahi, wapate kipato, wafanyabiashara wachangamkie fursa.... watu wapunguze mawazo kwa kujumuika na kukutana na watu mbalimbali humo. Mambo ya majimbo ya kugombea hiyo ni ajenda yake km anataka mwache atake, na kila anayetaka afanye lolote naye ili washindane wakati ukifika
 
Huyu Tulia namshauri atulie aokowe ndowa yake tu, huku kwenye siasa amepotoka hana upako huo. Bora Ummy Mwalimu anao mvuto wa kike.
 
Back
Top Bottom