WanaJF,
Kwa sasa Dr Slaa ametimiza miaka 70 rasmi lakini bado ameng'ang'ania nafasi kubwa ya kimaamuzi kwenye chama. Jambo ambalo ni hatari kubwa.
Kwa tafiti fupi iliyowahi kufanywa ilionyesha kuwa viongozi wengi waliowahi kuingiza nchi zao kwenye vita ni wale wenye umri mkubwa kama huo wa Dr Slaa.
Hivyo maamuzi ya CHADEMA kumtumia Dr Slaa mpaka sasa yanaweza kuhatarisha amani hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu kutokana na maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na Dr Slaa kutokana na umri wake.
Aidha, itakumbukwa miaka ya hivi karibuni Dr Slaa alikuwa akitoa kauli na ajabu ajabu na zenye viashiria vya kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Sasa pata picha hali itakuwaje kwenye uchaguzi?
Ningependekeza Dr Slaa apelekwe kwenye baraza la wazee la chama na nafasi yale ichukuliwe na Tundu Lissu ili kukipa uimara CHADEMA haswa kwenye kuelekea kwenye uchaguzi.
Kweli mkuu!Dr Slaa ni tishio kwa magamba, hata Sitta alikwishasema!
muulize Lowasa,Pinda,Dr.Bilal wana umri gani,hata Warioba wana umri ganiJuzi tuliambiwa Mh. Samwel Sitta ametimiza miaka 71, na jana kateuliwa kuwa mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge
Nenda kwenye histori ya Kenya Marehemu mzee Kenyatta alishawaambia wananchi wake pamoja na kua na umri wa miaka 75 lakini alichokua anamfanyia Mama Ngina usikua mpaka anaomba maji!miaka 70 na anaongeza mke, kweli nzi hufia kwenye kidonda.
Dr Slaa ni kijeba wa siasa
kwanza nimpe hongera dr.slaa kwa kula chumvi nyingi .. namtakia maisha marefu mzee wangu slaa. pili kwa jinsi taifa lilivyo na changamoto nyingi zinazolikabili namuomba tu apumzike mambo ya siasa na kujikita zaidi kuwa mshauri wa chama , pilikapilika za urais hataziweza kabisa zinahitaji vijana kama zito. mzee pumzika ule pensheni yako siasa zinakutesa tu
unajua kama Warioba ana zaidi ya 70?