Naona unaweka maneno kufurahisha nafsi, si kuboresha mjadala. Kuna cheo kinaitwa 'Katibu wa UKAWA'? Labda kama umekianzisha kwenye comment yako hii.
Soma kwa makini, conclusion ya Katibu Mkuu Dkt. Slaa haiko event-driven kwa kuangalia tukio la juzi pekee, bali trend ya chombo hicho. Ndiyo maana umekumbushwa kilichokuwa kikitokea wakati Dkt. Slaa alipokuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na mbunge mahiri bungeni, namna ambavyo TBC hawa hawa walikuwa wakifanya waliyofanya juzi.
Lakini pia conclusion hiyo haijafanyika kw akuangalia matangazo ya Bunge Maalum la Katiba pekee, bali trend ya TBC katika masuala mengi mengi ambayo si tu yanakwenda kinyume na matakwa na maslahi ya wananchi (mabadiliko) bali pia yanakinzana na taaluma, weledi na maadili ya uandishi wa habari. That's very serious kuliko unavyoweza kufikiri wewe.
Tunajua mathalani ambavyo siku hizi Waziri amekuwa akichagua nani na nani wahojiwe pale nje ya bunge au kwenye Kipindi cha Jambo asubuhi. Tunajua....tunajua...
Kama ni suala la fursa kwa vijaa, CHADEMA chini ya uongozi wa Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa, imekuwa mfano wa kuigwa kwa vyama na taasisi zingine nchini namna ambavyo kimetoa fursa na kujenga mazingira ya kuwakuza, kuwajenga na kuwatumia vijana kutimiza majukumu makubwa kwa ajili ya umma. Matunda yake yanaonekana.