Dr. Slaa tafadhali tumia busara tuiondoe CCM 2015

Hakikwanza

JF-Expert Member
Dec 11, 2010
4,034
1,003
Mpaka sasa hatma yako juu ya CHADEMA ni kizungumkuti, toka Mh Lowasa alipo jiunga na CHADEMA na kupewa form ya kugombea urais. Nikuombe Dr. Slaa tunaomba utoe msimamo wako ili kuiondoa sintofahamu hii. Pia msimo wako ujue kuwa Tanzania inahitaji ukombozi kwa njia yeyote toka mikono ya mfumo dhalimu na fedhuri wa CCM. Watanzania walio wengi wanasubiri msimamo wako wafanye maamuzi sahihi.

Tahadhari hakuna adui wa kudumu hasa anapoungana nawe na kukusaidia kupambana na adui zako anao wajua fika either kwa kuwa pamoja nao. Tunakuomba usamehe yote kiongozi wetu mpendwa ili tuikomboe nchi. Urais ni taasisi, nina imani tutashinda tukiwa pamoja na tutashindwa tukigawanyika. Watanzania wanaimani sana na UKAWA hivyo ni muda wa kushikamana, kukubaliana na kupendana kuliko kipindi chochote kile. Mungu ibariki Tanzania na UKAWA.
 
...... Binafsi Simkubali Lowasa, Ila Kwavile Lengo Ni Kuitoa Ccm, Nitafanyaje Sasa
 
...... Binafsi Simkubali Lowasa, Ila Kwavile Lengo Ni Kuitoa Ccm, Nitafanyaje Sasa

Ukishazungumza Lowasa ni sawa na CCM. Ukizungumzia CCM huwezi mtoa Lowasa. Hapa CDM wamechemka. Hapa ni CCM A na CCM B. No more CHADEMA ndugu zangu. Tusidanganyike. Tena kwqngu mimi CCM wameonyesha kutubu kwa kuyamwaga majizi na sasa wamekuwa malaika. Sisi ndiyo tumeyakumbatia tena kwa tamaa zetu. Ikulu tungefika na Slaa tuu na si vinginevyo. Tumeshakuwa wachafu kuliko CCM mkubali mkatae.
 
Sisi wa wanachadema tumeelewa nia njema ya viongozi wetu. EL sio mbaya zaidi ya mfumo uliopo wa ccm. Dr Slaa tumia busara tuiondoe ccm turejeshe matumaini kwa nchi yetu n mama yetu Tanzania
 
Mkuu sikubaliani nawe kwani serikali haita undwa na Lowasa peke yake.
 
Kama hili tatizo lipo nina imani uongozi wa CDM utalitatua bila kuathiri mafanikio yaliyopatikana mpaka sasa.
 
Ata akisusa kuna baadhi sie tushaamua tutapigia kura ata jiwe chadema ikilisimamisha kuliko CCM nataman watu wangekua na msimamo huu cha muhim ccm itoke kwanza haya mambo ya mtu kususa sijui nn baadaye
 
Wale mnaoshabikia matukio, na " imani kwa viongozi" mmeshawahi kujiuliza kuhusu ni itikadi gani mnaifuata katika kuleta mabadiliko ya uongozi wa nchi kupitia mfumo wa vyama vya kisiasa? Kwa mfano mnaamini katika kufuata maadili au hata jambazi anaweza kuwa Rais ili mradi atawapa ushindi? Kama jibu ni ndio, mnaifuata itikadi hiyo? Au ndio ule usemi kwamba hatuna akili? Tafakari!
 
Ukishazungumza Lowasa ni sawa na CCM. Ukizungumzia CCM huwezi mtoa Lowasa. Hapa CDM wamechemka. Hapa ni CCM A na CCM B. No more CHADEMA ndugu zangu. Tusidanganyike. Tena kwqngu mimi CCM wameonyesha kutubu kwa kuyamwaga majizi na sasa wamekuwa malaika. Sisi ndiyo tumeyakumbatia tena kwa tamaa zetu. Ikulu tungefika na Slaa tuu na si vinginevyo. Tumeshakuwa wachafu kuliko CCM mkubali mkatae.

Naumia sana Dr slaa kuchelewesha huu ukombozi.
Lowassa na ufisadi wake mbona Ccm ilishinda uchaguzi mwaka 2010 ikiwa na fisadi na kikwete akamsafisha akisema Lowassa jembe? Dr slaa nakuomba baba rudi Chadema unatuacha yatima. Msamehe Lowassa baba niko chini ya miguu yako, Tumsifu yesu kristo!
 
Sio kila maamuzi ya chama yakufurahishe. Wenzio wameamua, unga tela. ViVinyongo
ya nini? Ccm iitokekwanza tubebe nchi
.
 
Ukishazungumza Lowasa ni sawa na CCM. Ukizungumzia CCM huwezi mtoa Lowasa. Hapa CDM wamechemka. Hapa ni CCM A na CCM B. No more CHADEMA ndugu zangu. Tusidanganyike. Tena kwqngu mimi CCM wameonyesha kutubu kwa kuyamwaga majizi na sasa wamekuwa malaika. Sisi ndiyo tumeyakumbatia tena kwa tamaa zetu. Ikulu tungefika na Slaa tuu na si vinginevyo. Tumeshakuwa wachafu kuliko CCM mkubali mkatae.
Wao wamesema lowasa kaja na mamilioni ya wanachama, sasa sijui wana wasiwasi gani?! Slaa ana kura yake moja tu! Ni mpumbavu tu anayeamini atakombolewa na hili fisadi, na Dr Slaa hawezi kuwa mmoja wa wapumbavu hao. Wasubiri waone matokeo ya upumbavu wao baada ya uchaguzi.
 
Mpaka sasa hatma yako juu ya CHADEMA ni kizungumkuti, toka Mh Lowasa alipo jiunga na CHADEMA na kupewa form ya kugombea urais. Nikuombe Dr. Slaa tunaomba utoe msimamo wako ili kuiondoa sintofahamu hii. Pia msimo wako ujue kuwa Tanzania inahitaji ukombozi kwa njia yeyote toka mikono ya mfumo dhalimu na fedhuri wa CCM. Watanzania walio wengi wanasubiri msimamo wako wafanye maamuzi sahihi. Tahadhari hakuna adui wa kudumu hasa anapoungana nawe na kukusaidia kupambana na adui zako anao wajua fika either kwa kuwa pamoja nao. Tunakuomba usamehe yote kiongozi wetu mpendwa ili tuikomboe nchi. Urais ni taasisi, nina imani tutashinda tukiwa pamoja na tutashindwa tukigawanyika. Watanzania wanaimani sana na UKAWA hivyo ni muda wa kushikamana, kukubaliana na kupendana kuliko kipindi chochote kile. Mungu ibariki Tanzania na Ukawa

Nani kakuambia kuwa wana imani na UKAWA? Sentensi sahihi ni BAADHI ya Watanzania...
 
Sisi wa wanachadema tumeelewa nia njema ya viongozi wetu. EL sio mbaya zaidi ya mfumo uliopo wa ccm. Dr Slaa tumia busara tuiondoe ccm turejeshe matumaini kwa nchi yetu n mama yetu Tanzania

Mheshimiwa dr Slaa tumia busara. Na fanya hili kwa watanzania. Kumbuka umepambana kwa muda mrefu kukijenga chama na histiria imeishaandikwa. Sasa twende wote tukamalizie mkia ili tuchukue uhuru kwa mara ya pili. Mzee rudisha moyo hii ni vita lazima tushirikiane na kwa kutumia mbinu ambazo adui yetu hakuzitarajia ili tushinde.
 
Tyranny of numbers won jubilee party an election ,yes politics is a game of numbers. Lowassa has the numbers to win UKAWA an election ,Daktari Slaa zingatia hili please.
 
Ukishazungumza Lowasa ni sawa na CCM. Ukizungumzia CCM huwezi mtoa Lowasa. Hapa CDM wamechemka. Hapa ni CCM A na CCM B. No more CHADEMA ndugu zangu. Tusidanganyike. Tena kwqngu mimi CCM wameonyesha kutubu kwa kuyamwaga majizi na sasa wamekuwa malaika. Sisi ndiyo tumeyakumbatia tena kwa tamaa zetu. Ikulu tungefika na Slaa tuu na si vinginevyo. Tumeshakuwa wachafu kuliko CCM mkubali mkatae.

Mkuu ata mimi iki kitendo cha kumkata slaa kisa ya mwizi kimeniuma kama slaa ataenda chama chochote mimi nitamfwata,asipohama chadema ni bora nisipige kura.
 
Ni ukweli usiopingika kama tutaingia kwenye uchaguzi tukiwa wamoja kiasi hicho ni dhahiri ushindi upo mezani lakini Dr. W. Slaa asipoondoa kinyongo basi atakuwa amegawanya ushindi wa UKAWA makusudi kabisa. Namba Dr. Slaa aelewe hilo kirahisi kuliko anavyorikiri.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom