Dr. Slaa tafadhali tumia busara tuiondoe CCM 2015

Dr. Slaa tafadhali tumia busara tuiondoe CCM 2015

Mheshimiwa dr Slaa tumia busara. Na fanya hili kwa watanzania. Kumbuka umepambana kwa muda mrefu kukijenga chama na histiria imeishaandikwa. Sasa twende wote tukamalizie mkia ili tuchukue uhuru kwa mara ya pili. Mzee rudisha moyo hii ni vita lazima tushirikiane na kwa kutumia mbinu ambazo adui yetu hakuzitarajia ili tushinde.

Pamoja sana mkuu
 
Ni ukweli usiopingika kama tutaingia kwenye uchaguzi tukiwa wamoja kiasi hicho ni dhahiri ushindi upo mezani lakini Dr. W. Slaa asipoondoa kinyongo basi atakuwa amegawanya ushindi wa UKAWA makusudi kabisa. Namba Dr. Slaa aelewe hilo kirahisi kuliko anavyorikiri.

Yes Dr Slaa will go down in history as a leader who abandoned Tanzanians in the hour of need and thus dashed our hope for a better tomorrow.
 
Last edited by a moderator:
Naamini Mwisho wa Siku Dr na Lowasa Watakua Jukwa moja wakirusha makombora kwa Ccm.....Hii ni Siasa!
 
hilo jambazi lilikaa miaka 7 kabla ya kujibu tuhuma zinazomkabili. kwani dr ana muda gani toka akae kimya? labda nae aliambiwa kama humkubali EL "shut up" Hizo akili mlizoshikiwa na kina mbowe zitakaporudiswa mtakua mmefilisiwa mpaka nguo za ndani
 
...... Binafsi Simkubali Lowasa, Ila Kwavile Lengo Ni Kuitoa Ccm, Nitafanyaje Sasa

Adui yetu ni CCM,Mie.Dr Slaa ndo alikuwa my first choice lkn.akihama asitegemee kuwa nitamfuata maana hapa hapa CDM ndo angalau kuwa dalili ya kuwang'oa CCM
 
hilo jambazi lilikaa miaka 7 kabla ya kujibu tuhuma zinazomkabili. kwani dr ana muda gani toka akae kimya? labda nae aliambiwa kama humkubali EL "shut up" Hizo akili mlizoshikiwa na kina mbowe zitakaporudiswa mtakua mmefilisiwa mpaka nguo za ndani

Jambazi huwa anadunda mitaani bila kukamatwa
 
Mpaka sasa hatma yako juu ya CHADEMA ni kizungumkuti, toka Mh Lowasa alipo jiunga na CHADEMA na kupewa form ya kugombea urais. Nikuombe Dr. Slaa tunaomba utoe msimamo wako ili kuiondoa sintofahamu hii. Pia msimo wako ujue kuwa Tanzania inahitaji ukombozi kwa njia yeyote toka mikono ya mfumo dhalimu na fedhuri wa CCM. Watanzania walio wengi wanasubiri msimamo wako wafanye maamuzi sahihi. Tahadhari hakuna adui wa kudumu hasa anapoungana nawe na kukusaidia kupambana na adui zako anao wajua fika either kwa kuwa pamoja nao. Tunakuomba usamehe yote kiongozi wetu mpendwa ili tuikomboe nchi. Urais ni taasisi, nina imani tutashinda tukiwa pamoja na tutashindwa tukigawanyika. Watanzania wanaimani sana na UKAWA hivyo ni muda wa kushikamana, kukubaliana na kupendana kuliko kipindi chochote kile. Mungu ibariki Tanzania na Ukawa

Ndaani ya Ukawa ni mtanange kati ya wasafi(wazalendo) Vs wachafu(mafisadi) ..safi sana Dr.Slaa usikubali shetani akuteke katika kuungana na wanafiki
 
Slaa anawaweka busy ccm ili wasahau kumnadi mgombea wao pombe. UKAWA SHIKAMOO
 
Naamini Mwisho wa Siku Dr na Lowasa Watakua Jukwa moja wakirusha makombora kwa Ccm.....Hii ni Siasa!

Kwamba nuru ikae na Giza? acheni Dr awatose kama mmeamua kumdhàlilisha ngoja ajiweke pembeni
 
Unawashwa eti ww ccm yanakuhusu nn mambo ya ukawa? Polen kama walikuaidi cheo serekalini jiandae kisaikolojia
 
Mpaka sasa hatma yako juu ya CHADEMA ni kizungumkuti, toka Mh Lowasa alipo jiunga na CHADEMA na kupewa form ya kugombea urais. Nikuombe Dr. Slaa tunaomba utoe msimamo wako ili kuiondoa sintofahamu hii. Pia msimo wako ujue kuwa Tanzania inahitaji ukombozi kwa njia yeyote toka mikono ya mfumo dhalimu na fedhuri wa CCM. Watanzania walio wengi wanasubiri msimamo wako wafanye maamuzi sahihi. Tahadhari hakuna adui wa kudumu hasa anapoungana nawe na kukusaidia kupambana na adui zako anao wajua fika either kwa kuwa pamoja nao. Tunakuomba usamehe yote kiongozi wetu mpendwa ili tuikomboe nchi. Urais ni taasisi, nina imani tutashinda tukiwa pamoja na tutashindwa tukigawanyika. Watanzania wanaimani sana na UKAWA hivyo ni muda wa kushikamana, kukubaliana na kupendana kuliko kipindi chochote kile. Mungu ibariki Tanzania na Ukawa
Unamdanganya Dk. Slaa....... adui wa kudumu ni Fisadi! Wanaosulibili msimamo wa Dk. Slaa ndio wafanye maamuzi wamekula wa chuya.....
 
Ukishazungumza Lowasa ni sawa na CCM. Ukizungumzia CCM huwezi mtoa Lowasa. Hapa CDM wamechemka. Hapa ni CCM A na CCM B. No more CHADEMA ndugu zangu. Tusidanganyike. Tena kwqngu mimi CCM wameonyesha kutubu kwa kuyamwaga majizi na sasa wamekuwa malaika. Sisi ndiyo tumeyakumbatia tena kwa tamaa zetu. Ikulu tungefika na Slaa tuu na si vinginevyo. Tumeshakuwa wachafu kuliko CCM mkubali mkatae.

Aliyekuwa nje ya CCM ni mpinzani wa CCM EL sasa ni mpinzani acha kupotosha watu mbona hata Dr. Slaa katokea CCM na akapokelewa vizur?
 
ccm kazi imekwisha tunasubiri october. kazi kwenu wanasiasa/wanachama/wapambe "wafa maji" bendera kufuata upepo! Naona maandamano yanaanzia jf. Kumsahau magufuli ni sawa na kusahau jina la baba yako mzazi.
 
Duniani hakuna aliye mtakatifu; haya aliyasema YESU KRISTO. Hivyo basi Dr. Slaa mwenyewe si msafi, angekuwa msafi angeendelea na Upadre hadi leo...! Kwahiyo hapa kinachohitajiwa ni kusameheana tu na kumwomba Mungu atuepushe na hali ya kujengeana uadui
 
Ndugu Dr Slaa ni kiongozi wa chama mwenye ushawishi hivyo ni sehemu ya ushindi na tunampenda sana.
Dr Dr Dr! Chonde chonde kama ni ukweli una mtazamo wa kuachana na siasa, tafakari upya tuwe wamoja kumwondoa ccm. Wewe ni mkristu hata kama umekosewa samehe tuuu. Tusiwape faida magamba wakati wewe ndio hasa umefikisha chama hapa kilipo.
 
Kwa niaba ya wana Rorya na wanachama wa chadema Rorya tunakuomba utoke mapumziko na urudi ofisini maana tunasikia uko mapumziko.Baba Tunakupenda sana,wewe ndiye taa,ndiye mwenye TOCHI yenye kutoa nuru kwa chama hiki ulichokijenga wewe kwa nguvu kubwa.

Mgombea wa chama tayari amepatikana,tunampenda.Tulimtuhumu kwa ufisadi wa richmond.Baba tumemsikia tena hadharani akisema suala la richmond ilikuwa ni agizo kutoka juu.Dr. agizo kutoka juu.Mimi ni mwanachama ulipo agiza chadema ni msingi hakika tulitembea ilaya yote kuwa andikisha wanachama wapya.Tulitekeleza hilo.

Dr.Katibu mkuu,tuko vitani na vita hii tuna shauku ya kushinda.Kaa katika kiti chako cha mamlaka na uamuru wanachadema woote kuongo mbele kuishinda ccm.Raha ya vita ni kushinda vita.Kushinda vita hii tunaweza maana adui kapoteza sight na target.Haoni tena na watu hawana tena imani na mtawala huyu.

Ongoza vita hii mashariki,magharibi,kaskazini,kusini na kushinda vita hii,ushindi wa Mhe.Lowassa ni ushindi wa chadema,ukawa na wananchi woote wa Tanzania.

Tunamwomba muweza wa mambo yote akuangazie na akushushie rehema zake na kukufanulia jukumu lako kwa chadema chama ambacho ningependa siku ukilala ikulaze mahali pazuri.

YESU KRISTO alitufanya wapatanishi.....alitufundisha kusamehe saba mara sabini.
 
Back
Top Bottom